Usiku huwa kuna ninii

Usiku huwa kuna ninii

Iyo hali inanitokeaga mimi pia, japo mimi uwa naweza kuji-control na kuamuka mapema..yaani inakuwaga ni kama nataka kuamuka kimwili lakini akili bado imelala

Huwa najitaidi sana ku-focus kuamuka na sio kulala mwisho hali inaondoka yenyewe.

Nakushauri iyo ni hali ambayo inaukuta mwili pale unapokuwa umelala bila mpangilio (hovyo hovyo) hivyo jitaidi kufatilia ulalaji wako labda unalala vibaya ndomana mauzauza hayaishi,make mie hali unitokea pale napolala kwenye kochi au kitandani kama nimelala vibaya....

post using my macbook air using jamiiforums app
 
pole sana !kunakipindi nyuma na mm iliwah nitokea nadhan nikiwa na miaka 15!nikapelekwa hosp nikaonekana na malaria nyingi sana !since hapo hakuna kitu! sana sana nawaota kina l.i.p.u.m.b..a tu .....mxiew zao!

pole!jaribu kwenda hospt!
 
Suluhisho la hiyo kitu kwanza ni kusali na kulala na kitabu cha Imani yako, Pili na muhimu usilale Chali kamwe (Chunguza utaona mara zote unapotokewa na hiyo hali ni pale unapokuwa umelala chali) na mwisho chunguza Godoro unalolalia kama limechoka badilisha
Hii si kweli,mda mwingine utakuta mtu amekaa kabisa kitandani, ila anapata hyo force ya kumlazimisha kulala,hayo madude machafu tu mkuu,huamini cause hujapatwa au kushuhudia.
 
Juzi kati hapa nilishtuka usiku saa saba,nililala mapema sana,nikahisi kuchoka kulala nikaenda kulala kwenye kochi sebuleni,nikapitiwa usingizi kidogo mara nikafumbua macho utafikiri nimeamshwa hivi,,nikafumba macho tena ili nisinzie ile nataka kupitiwa tu nikaona kama nimepitiwa na giza usoni paa nikaamka tena nikaapuuzia nikalala ile hali ikajirudia ya kitu kama giza kinapita ,halaf kukawa na nguvu fulan sijui ilikua inatoka wapi inanilazimisha nipate usingizi mzito kweli wakati mi nikitaka kuamka lakin kuamka nashindwa ,,hiyo hali inanitokea huku naongea kimoyo moyo

. ,,nikaanza kusali wapi hakuna kitu,,mwili unaishiwa nguvu nakua najitahidi kuchezesha mguu ili nipate nguvu niamke lakin wapii,,,halaf nikawa siutaki ule usingizi kwani nakua naona napelekwa sehemu siijuii halaf inatisha
wakati nazidiwa kupata usingizi wa lazima nikasikia kitu kinanipuliza sikioni huku nikipata maumivu makali hapo hapo nikaamka tena nikakaa ,,nikajirudia zangu chumbani nikaona niende chumba cha ndugu yangu nilale nae maana mwanzoni nililala chumba kingine

Nimelala na huyu ndugu ,huwezi amini nikifumba macho nakua naona kama naonyeshwa kwenye tv,naona pote hadi nje kule ,kule sebuleni napaona halaf mwili ukawa unatetemeka napata maumivu ambayo sio makali sana nikaendelea kusali lakin hakuna kitu,,yaan sikulala jamani nikalzimishwa ule usingizi nikawa naona watu wawili wana giza kubwa wananirukia kwenye mwili wangu wanarudia kile kitendo ,,kumbe vile nahangaika nilikua nimvuta yule ndugu yangu anisaidie baadae nikashtuka nikaona nikae macho tu sasa,,asubuhi ilipofika yule ndugi yangu akaniambia leo ulikua unaning'ang'ania miguu yangu,,nikamwambia kuwa leo nimehangaika kulala tu ,,nikaona kazi kumsimulia

Hii mim hunitokea mara nyingii yaan sio mara ya kwanza kunitokea na hunitokea nakuwa najijua kabisa ila mwili unakuwa hauna nguvu,,,na mara nyingine huwa hadi naona natolewa nje huku moyoni nakua nasema Mungu wangu napelekwa wapii mie nikisali sali naashtuka
Siku zingine nalala tu tu vizurii,siku nyingine nakuwa hivyo
Je ni kuwangiwa au nin maana wengine husema uchawi hakuna cc Nyani Ngabu
Je wengine huwa mnalala tu vizuri au wengine mnahangaika kama mimi nifanyeje ili hii hali niiepuke kwa waganga siwezi kwenda kabisa ,,so usinishauri habari za waganga wala kwenda kanisani

Kuna siku napo nililala ikanitokea hivyo nilisikia napigiwa kelele masikioni kwa nguvu mpaka nikaamka,,siku nyingine najikuta napiga ukuta sijijui yale maumivu yananiamsha kiganja kinauma tatizo nakuwa najijuaa kabisa
Hizo ndoto tu..usije ukafikiria eti unarogwa! Mwenyewe huwa inanikuta baadhi ya siku, sometime napiga mpaka makelele na kuruka kitandani...
Ila nikishajua ni ndoto nacool down na kuendelea kulala!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahaaha unanikumbusha kuna dent aliruka kutoka kwenye deka usk had chini puh! akaendelea kulala!ni miaka imepita ila huwa sisahau! inaitwa sleeping walking! pole sana
 
Iyo hali inanitokeaga mimi pia, japo mimi uwa naweza kuji-control na kuamuka mapema..yaani inakuwaga ni kama nataka kuamuka kimwili lakini akili bado imelala

Huwa najitaidi sana ku-focus kuamuka na sio kulala mwisho hali inaondoka yenyewe.

Nakushauri iyo ni hali ambayo inaukuta mwili pale unapokuwa umelala bila mpangilio (hovyo hovyo) hivyo jitaidi kufatilia ulalaji wako labda unalala vibaya ndomana mauzauza hayaishi,make mie hali unitokea pale napolala kwenye kochi au kitandani kama nimelala vibaya....

post using my macbook air using jamiiforums app
Kulala vibaya aje ,mbona huwa nalala vyema tu
 
Ila mie nishawahi kulala katikati ya kulala nakua kama nimepaliwa na mate na mtu ananikaba basi nashtuka nakohoa mapigo ya moyo yananienda mbio naonaga kama vile kifo kilee nilimuhadithia mama akasema nalala bila kusali then nisilale chali nilale na biblia saiv hainitokei tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapenzi nafanya lakin kuna muda nakuwa sitaki kabisa sitaki kuguswaa

usifikiri huko mwaya utajikuta kila siku kwa waganga wa kienyeji! hyo kukosa hamu ni kawaida hatujawa mambwa tutake kila mara! me mtu anieleze habari za majini mahaba namuona yy mwenyew ni mahaba jini
 
Hii si kweli,mda mwingine utakuta mtu amekaa kabisa kitandani, ila anapata hyo force ya kumlazimisha kulala,hayo madude machafu tu mkuu,huamini cause hujapatwa au kushuhudia.
Huwa naambiwa nna maruhani itakuwa ni yenyewe ndio yananifanya hivyo
 
usifikiri huko mwaya utajikuta kila siku kwa waganga wa kienyeji! hyo kukosa hamu ni kawaida hatujawa mambwa tutake kila mara! me mtu anieleze habari za majini mahaba namuona yy mwenyew ni mahaba jini
Hebu niambie nini hunitokea usiku,,,umesoma uzi ?
 
Kulala vibaya aje ,mbona huwa nalala vyema tu
Try kujichunguza maybe ndo tatizo,ukiona unalala vizur basi tatzo inaweza ikawa maybe stress..!

Je unaonaga movie za kutisha labda...?

post using my macbook air using jamiiforums app
 
Back
Top Bottom