Usikimbilie ndoa

Mungu akubariki sana mkuu[emoji122][emoji122]
 
Katika vitu ambavyo ni vigumu kufanya ni pamoja na kuyakumbuka mazuri pale akili inapomchoka mtu na mara nyingine ni kwa sababu za kipumbavu. Binadamu tunachokana na hiyo ni kawaida maana mkamilifu hakuna lakini ukitaka kujua upendo wa dhati ni pale unapokumbuka mazuri ya mtu pale ambapo unahisi huwezi kumsamehe na kupata sababu za kuwa karibu naye pale unapoona hana jipya la kukupa au kukufurahisha. True love ipo lakini ni kwa wale wenye kujua kuwa binadamu ni dhaifu na inapaswa kumuwekea nafasi ya ubinadamu wake katika kukosea.
Ndoa za nyingi siku hizi ni kama kuolewa ama kuoa mke au mume wa mtu. Mtu anaingia katika ndoa kwa sababu zake ilhali moyo wake upo pengine
 
Ukiona mtu anatumia akili sana katika mahusiano yake bhasi ujue moyoni haupo. Mungu angeruhusu tutumie akili zetu bhasi wanaume wengi wasingekuwa na vigezo vya kuoa na wanawake wengi wasingekuwa na vigezo vya kuolewa. Hisia huwa hazijali na ndicho chanzo kikuu cha uvumilivu, hisia ikizidi huishinda akili na ndil hufidia madhaifu ambayo pengine akili yako inayaona wazi kwa mwenzi wako.
Kila siku watu wanakuja na thread za kutokutoshelezwa lakini ni watu hao hao huwa hawawezi kuondoka na ndio maana huomba msaada, hiyo ndio nguvu ya upendo yaani pamoja na madhaifu ambayo mtu mwingine asingeweza kuyavumilia, unavumilia kwa sababu unampenda mtu kweli kweli
 
Biblia inasema tuishi naa kwa akili
 
"Nchi ya kusadikika" ni Mme Bwege pekee ndiye hatathubutu kushika na kukagua simu ya Mkewe.
 
Hata mimi km wewe tuu hapo mwisho [emoji38][emoji38]
Nikikapata najilipua (sijui ka kiume kanaitwaje[emoji50])
 
Futa haraka hii SMS yako, shemeji niko naye hapa tunaperuzi huu uzi[emoji87]
 
Ukweli mtupu
 
Biblia inasema tuishi naa kwa akili
Bila shaka maana hata ukienda kujisaidia haja ndogo ni lazma utumie akili la sivyo utachafua choo kizima. Hata mfanyakazi wako wa ndani pia yapaswa uishi nae kwa akili yaani huwezi kuishi na mtu pasipo kutumia akili. Mwanamke ni kiumbe mwenye kutumia hisia zaidi katika maamuzi kuliko akili na wanaume tukaumbiwa kutumia akili zaidi kuliko hisia, hii ni balance asilia kwa maana hisia mara nyingi hujali kuwa "Comfortable" na akili hujali "kitu sahihi". Hivyo kama mwanaume unapaswa kuishi na mwanamke kwa akili ili kuweze kufanyika maamuzi sahihi na ndio maana baba akaitwa kichwa cha familia, kichwa chenye akili ya kutoa maamuzi sahihi ila mama akapewa kuwa mlezi maana huweza kutoa mawazo ya kumfanya mtu apate comfort. Hii ndio sababu mama hupendwa kuliko baba maana maamuzi yake ni nadra kumuumiza mtoto
 
Well done
 
So Mungu alikosea sana alipotuagiza Me"tuishi kwa akili na Ke zetu"?
 
Hapana mkuu nilichokazia ni kuwa akili hutumika popote.Pia akili ni muhimu hasa katika mahusiano maana mwanaume ameumbiwa kutumia akili zaidi kuliko hisia ili atoe maamuzi sahihi hata kama yatamuumiza mtu na mwanamke akaumbiwa kutumia hisia zaidi kuliko akili ili apate kuwa mfariji na safekeeper wa nyumba. Hii ndio sababu watu wengi humpenda mama na kumuelezea shida zao yaani hata kama hana uwezo wa kuwapa msaada kwa sababu ni mfariji. Hata wewe ukiwa na mwanamke anayekupenda kweli, kukujali na kukutia moyo bhasi unaweza kuvishinda vikwazo vingi katika maisha na kufanikiwa kutokana na faraja yake.
So Mungu alikosea sana alipotuagiza Me"tuishi kwa akili na Ke zetu"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…