Nicas Mtei katika mambo ambayo nimeweka msisitizo katika maisha yangu yote na katika safari zangu za kufikia pale ninapotaka kufikia msamiati wa Kukata Tamaa nimeufuta.
Naamini katika kupambana na naamini katika kuamini kuwa kila jambo linawezekana na hakuna sehem imeandikwa kwamba ukienda na njia hii utashindwa hivyo nikate tamaa. Naamini kuwa kila jambo linawezekana so long umeweka juhudi zako na kumtanguliza Mungu mbele. Naamini hakuna suluhisho jepesi katika mambo magumu na njia ya kuyafanya magumu yawe mepesi ni juhudi binafsi na bila kukata tamaa.
Kukata tamaa popote ni mwiko na wala si maneno wala sio kejeli kutoka kwa yeyote zitakazoweza kunifanya niachene na kile ambacho nimepanga au natarajia kukifanya. Nitafanya kile nilichopanga hadi mwisho na iwapo nitaishia njiani kuna kitu kinasemwa at least alijitahidi at least alionyesha nia ya kufanya na sio kukata tamaa mwanzo wakati hata kuonyesha dalili za kufanya kitu hicho hujaonyesha
Kukata tamaa ni adui katika kila jambo huwezi kuanza kujenga nyumba na ukaanza na mawazo sijui nitaimaliza au sijui nitapata pesa za kuimaliza hiyo ni dalili ya kushindwa tayari. Unapoanza msingi wa nyumba yako jiambie moyoni mwako hii nitaimaliza na nitajenga nyingine kama hizi nyingi tuu.
So naamini katika kutenda na kujaribu kutenda na kujaribu kufanya kile ambacho kiko kwenye mipango bila kuwa na wasi wasi kuwa katikati ya kile nilichoppanga kunawez akuwa na vikwazo ila vikwazo vipo ili kukufanya uendelee mbele na sio kurudi nyumna na ujifunze mbinu mbadala kuvikwepa vikwazo hivyo
Asante sana mkuu