Usikate tamaa kijana mwezangu

Makau Js

Member
May 25, 2017
93
233
Leo tarehe 2 June 2017,naomba kijana mwenzangu usikate tamaa kwa jambo lolote lile ,nusu mwaka tayari siku ya leo ya Ijumaa ,kuelekea katika kutimiza malengo yetu ,Mwenyezi Mungu ametupa uzima na afya.

Usiogope kutafuta ajira yako kwa kuogopa kutofahamu kwa ufasaha lugha ya Kiingereza ,Bibi yangu ,Esther Mahlangu alizaliwa ,November 11, 1935 huko Middelburg, Mpumalanga-South Africa kwa sasa ana miaka 81 ,anaongea vyema kabila lake la Ndebele na hajui lugha ya kiingereza hata kidogo.

Bibi yangu ,Esther Mahlangu kupitia karama yake ya uchoraji , mnamo mwaka 1991 aliweza kubuni na kuchora [patterns] gari aina ya BMW 525i na kuwa gari ya kwanza kutoka katika company ya [BMW-Bavarian Motor Works] kuchorwa na mbunifu toka Africa kuipitia kitengo chao cha BMW Art Car.

Mwaka 1997 ,kazi ya Esther Mahlangu ilitumiwa na shirika la British Airways kuchora mkia [Tails] wa ndege zao,na mbinu na ubunifu alio utumia kuchora BMW 525i , ubuniu wake uliwafanya kampuni ya Fiat,kumpa nafasi ya kuchora gari yao aina ya Fiat 500 katika mji wa Turin mwaka 2007.

Coach wa timu inayoshiriki ligi kuu ya England -EPL Watford Football Club ,Walter Mazzarri ,alikuwa hawezi tengeneza sentensi hata moja ya lugha ya kiingereza -sababu yeye alikuwa Muitaliano ,yaani Shilole a.k.a Shishi Babe anazungumza kizungu kizuri kuliko ,Walter Mazzarri .

Watford Football Club walitizama , utashi wake na maarifa yake ndio wakampa kibarua na kuiwezesha Watford kushika nafasi ya 17, wakati Muingereza aliyekuwa anafundisha club ya Sunderland David Moyes ,anayeongea kiingereza kizuri na kwa ufasaha na ameishusha timu yake ya Sunderland.

Darasa- Jifunze toka kwa Bibi yangu,,Esther Mahlangu na Walter Mazzarri .Usilingie cheti chako au ubora wa kuongea kiingereza kwa ufasaha ,badala yake jivunie hazina yako ya maarifa na kipaji chako ,sababu kipaji kilichopakwa mafuta kinafuatwa na lugha zote ili kuleta flava na ubora.[HASHTAG]#Kiswahili[/HASHTAG]

3030a766c1132b678eadbaf560838c19.jpg
ba3d544acd4c72f902df16e29b9a3120.jpg
5ed3f044ef761c5ce3842bb5d2164067.jpg
2bd5672dc5e1be0dd919ea08554dd879.jpg
 
Darasa- Usilingie cheti chako au ubora wa kuongea kiingereza kwa ufasaha ,badala yake jivunie hazina yako ya maarifa na kipaji chako ,sababu kipaji kilichopakwa mafuta kinafuatwa na lugha zote ili kuleta flava na ubora.[HASHTAG]#Kiswahili[/HASHTAG]
Hapa ndipo tulipofeli kama Taifa, tunadhani elimu ni Kiingereza na Kiingereza ndio elimu, yaani ukiongea Kiingereza hata kama ni pumba unaonekana msomi bab kubwa mwenye ufahamu mkubwa, kiasi kwamba, shule za Academy zimekuwa dili siku hizi, bila kujali ubora wa elimu wanazotoa. Pia tunathamini sana vyeti bila kuangalia hazina ya maarifa iliyo kwenye kichwa cha mhusika. Masikini nchi yangu TZ...
 
Makau Js said:
Darasa- Usilingie cheti chako au ubora wa kuongea kiingereza kwa ufasaha ,badala yake jivunie hazina yako ya maarifa na kipaji chako ,sababu kipaji kilichopakwa mafuta kinafuatwa na lugha zote ili kuleta flava na ubora.[HASHTAG]#Kiswahili[/HASHTAG]
Mkuu, ninaomba niitumie article yako kama reference kwa ajili ya kufanya analysis ya wasanii wetu wa Tanzania na namna wanavyopoteza fursa muhimu kwa kigezo cha kutojua Kiingereza. naamini itanisaidia sana...
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Thanks brother.
I will never let you down.
SITAKATA TAMAA MWANZO MWISHO.
 
Back
Top Bottom