FortJeasus
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 604
- 399
Ni dhahiri,upo upungufu wa uelewa na ufahamu juu ya maana na nafasi ya Shahada ya Uzamivu za Heshima.
Hii ni kwa kuzingatia maneno na matendo ya watunukiwa na wadau wengine kwa upana wake.
Shahada hiyo kamwe haiwezi na haitakuwa sifa ya kitaaluma wala kuongeza uwezo wa kufikiri wala utendaji wa muhusika.
Kadhalika,kutokana na sababu zilizotajwa punde, Shahada hiyo si kigezo cha kupanda vyeo mahali pa kazi.
Kwa sababu hizo na nyingine nyingi,wahusika hawana haja ya kuratibu na kuendekeza vitendo vya ulaghai kwa kujitangaza pasipo sababu.
Mwanahabari mmoja aliyetunukiwa Shahada hiyo hivi karibuni haelekei kuelewa hivyo na kwa kweli tutarajie,kutoka kwake na wengine watakaofuata,usumbufu mkubwa katika siku za usoni.
Katika mazingira ya aina hii,Taasisi za Udhibiti wa Elimu ya Juu zitimize wajibu wake kwa kutoa suluhisho la kudumu juu ya suala husika.