mwananthropolojia
JF-Expert Member
- Oct 6, 2012
- 956
- 658
Wadau mm nina umri wa miaka 26 now, nimemaliza Sheria Chuo Kikuu Mzumbe ila sijabahatika kupata kazi bado. Imetokea nimependana sana na dada mmoja ambaye ni Kaimu Mchumi wa Halmashauri fulani ya Mji, tatizo ni kwamba ana umri wa takribani miaka 35 sasa, na wkt namuapproach moja ya sababu iliyopelekea asite kunikubalia ni age difference ila at last nikafanikiwa kumshawishi...washkaji na kaka zangu wananionea wivu sana wanadai huyu dem ananilea na kuna tetesi kwamba anapata mshahara mkubwa sana coz ameajiriwa zamani na ana masters degree.
Mara nyingi nalala kwake, nimebahatika kumiliki usafiri(gari) mapema so nikiamka nampeleka kazini asubuhi then narudi zangu maskani. Juzi kati nikamuuliza kwa kumtega kwamba nataka anipe mtoto akakubali! Jana nikamwambia nataka nimuoe akakubali! Ana uzuri wa kawaida tu ila ni mstaarabu sana, muwazi, hana mambo mengi na ananiheshimu sana ingawa kanipita umri! Nafikiria kumuoa mara tu nikipata kazi, je kuna tatizo lolote hapo wajameni?
Kumuoa hakuna tatizo ingawa kwa heshima na maadili yetu ya kiafrika, unatakiwa uwe unakumbuka kumpa "shikamoo" yake kila asubuhi maana ni dada yako mkubwa.
huna adabu kweli mwambie aseme shikamoo mama;;;hiyo miaka alioandika kakuheshmu tu mkuu hao ndio vijana wetu oohKumuoa hakuna tatizo ingawa kwa heshima na maadili yetu ya kiafrika, unatakiwa uwe unakumbuka kumpa "shikamoo" yake kila asubuhi maana ni dada yako mkubwa.
Mtu unaye lala naye hawezi kuwa mama yako, shangazi yako, wala dada yako !Mwanamke yeyote usiye na nasaba naye basi aweza kuwa mkeo, bila kujali umri !Hakuana mwanamke yeyote asiye na nasaba na wewe aweze kuwa na sifa za wanawake wenyewe nasaba na wewe !Umri si kitu, la msingi wakati mwingine kula jambo unaweza kosa kama vile watoto (kama mwanamke amepitisha umri wa kuzaa) kwani hata Bi Kidude ni halali kumuoa na akawa mke !Hawezi (Bi Kidude) kuwa Mama yako wala Bibi yako !Kumuoa hakuna tatizo ingawa kwa heshima na maadili yetu ya kiafrika, unatakiwa uwe unakumbuka kumpa "shikamoo" yake kila asubuhi maana ni dada yako mkubwa.
Maneno msumari !Kwa thread hii umeonesha hujiamini na hufai kuwa na familia'Kama ungekua unajiamini usingekuja hapa,kusema unaonewa wivu ni dalili ya kushindana na woga ulio ndani mwako'Pia kelele za rafiki zako zinakuchanganya sana'Halafu inaonekana vitu vya huyo dada ndo vimekuchanganya zaidi maana hapa hujazunguzia chochote kuhusu hisia wala mapenzi yako kwa huyo dada'I feel sory for her!
Hamna hoja hapo !swali la busara la kujiuliza mkuu ni kwamba kwann ana umri wa miaka 35 na hajaolewa? pia kama aliwahi kuolewa kwann aliachika na hujaeleza kama ni MJANE, take care bro magonjwa mengi
Moja ya faida za umri ni kutulia !umri si tatizo kama tu unahisi anavigezo ambavyo wewe unavihitaji kaka! ila tafakari kwa makini ndipo uchukue maamuzi!!!!
Chukua jiko ww, umri ni namba tu kama namba zingine
Kumuoa hakuna tatizo ingawa kwa heshima na maadili yetu ya kiafrika, unatakiwa uwe unakumbuka kumpa "shikamoo" yake kila asubuhi maana ni dada yako mkubwa.