Usife kibwege kama Ted Jorgensen

Usife kibwege kama Ted Jorgensen

Ofcoz ni makosa makubwa sana kumtelekeza mwanao wa kumzaa no matter what....kama shida mpate...na kama ni raha mle wote......ni damu yako na we ndie ulie fungua milango ya damu hiyo kuja duniani....

Yote Tisa kumi........hata kama mzazi kakosea vipi wew utabaki kuwa shahawa yake tu...Yani kwa kifupi umetoka kwenye kiuno chake.....hakuna mtu ambae atasimama mbele yangu na kuverify kitendo Cha kumuignore mzazi wake no matter amekufanyia mabaya kiasi gn.......!!!!

Yote kwa yote Mipango ya Mungu ni lazime itimie kwa kiumbe na mwanadamu yoyote yule.
 
Hata pia simulizi ya muanzilishi wa Apple Mr Steve Jobs nayo inataka kufanana na hii maana baba yake mzazi alikuwa ni Mwarabu wa Syria na alienda US kwa masomo ndo kukutana na mama yake Steve na Steve akawa adopted akiwa mdogo kabisa
 
Kila mtu na hatma yake,hatma ya jeff ilikuwa ni kulelewa na baba mwingine ili afikie mafanikio aliyonayo
 
Ilikuwa lazima Yuda amsaliti Yesu ili unabii utimie...Yuda hakuwa na kosa sababu ilikuwa imeandikwa.
Mtoto angelelewa na babaake angeishia kuwa mlevi tu kama babaake na angeachiwa duka la baiskeli.
True
 

AKIWA Kijana, alifanya tukio. Hakujuta. Na akasahau. Akaishi miaka 44 mingine. Ndipo akatokea mtu akamkumbusha kile alichokifanya. Akaumia. Akatamani asahihishe makosa yake. Hakupata fursa hiyo. Miaka mitatu baadaye akafariki dunia akiwa mwenye huzuni kubwa.

Zingatia, ujana ni tapeli mkubwa wa maisha. Ujana utakulaghai na kukufanya uone maisha ni hayohayo uliyonayo katika wakati uliopo. Ujana unaweza kukughilibu na kukusahaulisha ujio wa kesho. Ujana hufumba macho na huziba masikio. Si walisema ujana maji ya moto?

Ted Jorgensen, alipokuwa na umri wa miaka 17, alikutana na binti mrembo, Jacklyn Gise, aliyekuwa na umri wa miaka 16. Wakapendana. Wakaanza safari ya mapenzi.

Jacklyn akanasa ujauzito.
Wakati Jacklyn anashika mimba, alikuwa mwanafunzi wa high school. Ted alikuwa mcheza sarakasi aliyekuwa na ndoto za kufanikiwa kwenye mchezo huo.
Januari 12, 1964, mtoto akazaliwa. Jeffrey ndilo jina walilompa.

Jeffrey alipozaliwa, Ted alikuwa ameshatimiza umri wa miaka 18, Jacklyn miaka 17. Na sababu ya mtoto na malezi, ndoto za masomo zikayeyuka. Ted na Jacklyn wakafunga ndoa.

Maisha ya ndoa yakawa magumu. Ted alikuwa mlevi kupindukia. Mara arudi nyumbani alfajiri au asirudi kabisa. Ted alikuwa na kipato kidogo lakini hakukitumia kulea familia, bali starehe zake binafsi.
Baada ya miezi 17 ya ndoa, Jacklyn akaomba talaka. Ted akakubali. Wakaachana. Jacklyn akarudi kwa wazazi wake. Miaka miwili baadaye, Jacklyn akapata mwanaume mwingine, Miguel Bezos.

Wakafunga ndoa. Bezos akaomba kumuasili Jeffrey awe mwanaye kisheria. Ted akasaini nyaraka zote kuhalalisha mtoto wake atwaliwe na Bezos.

Mwaka 2012, mwandishi Brad Stone alipokuwa anakusanya taarifa ili aandike kitabu “The Everything Store” kilichohusu maisha ya bilionea mmiliki wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos, alimfikia Ted. Akamuuliza kama alikuwa na habari kuhusu mwanaye aliyezaa na Jacklyn mwaka 1964.
Ted akavuta kumbukumbu, kisha akajibu: “Nimekumbuka. Hivi yule mtoto bado yupo hai kweli?” Brad akamjibu: “Yupo hai. Ndio huyu bilionea mmiliki wa Amazon.” Ted akasikitika, lakini akakiri hakuwa baba bora kwa Jeffrey wala mume mzuri kwa Jacklyn.

Kuanzia hapo, Ted alianza kutafuta nafasi ya kuonana na mwanaye Jeffrey, angalau wazungumze, japo amtambue. Nafasi hiyo angeipata wapi?

Mwaka 2014, Ted aliumwa sana. Akaandika barua nyingi kwa Jeffrey, kumjulisha hali yake na kiu yake ya kumuona kabla hajaaga dunia. Hakupata majibu.
Hakuna ajuaye kama Jeffrey aliziona hizo barua na kumkaushia au hakuziona kabisa. Ila ni uhakika kuwa alitambua kuwa baba yake mzazi alikuwepo.

Mwaka 2015, Ted alifariki dunia bila kuonana na mwanaye wa damu, Jeffrey. Aliishia kumsoma na kumuona kwenye vyombo vya habari kama watu wengine.
Kuhusu maisha ya Ted; baada ya kuachana na Jacklyn, aliendelea na mitikasi yake ya kucheza sarakasi na ulevi. Miaka 10 baadaye, akagundua maisha aliyokuwa akiishi hayakuwa na kesho nzuri. Akaacha ulevi. Akafungua duka la kuuza baiskeli. Hiyo ndio ikawa kazi yake mpaka alipofariki dunia.

Ted baada ya kuachana na maisha ya ulevi, alimuoa mwanamke mwingine, jina lake Linda. Hakupata mtoto mwingine. Mkewe, Linda, alikuwa na watoto wanne.

Miaka miwili baada ya kifo cha Ted, taasisi ya utafiti wa mali na utajiri duniani ya Forbes, ilimtangaza Jeffrey kuwa tajiri namba moja duniani. Akimpita tajiri namba moja wa muda mrefu duniani, Bill Gates.
Kwa sasa, Jeffrey ana utajiri wa dola 183.6 billioni, ambazo ni sawa na Sh242.4 trillioni.

Jeffrey anatambua kuwa Ted ni baba yake, kwani cheti chake cha kuzaliwa na kumbukumbu zote za hospitali zinamtaja Ted ndiye baba yake.

Hiyo ni stori kuhusu tajiri namba moja duniani, Jeff Bezos na baba yake mzazi, Ted Jorgensen. Story kuhusu ujana na utapeli wake.

Ted angejua? Maskini hakujua. Alikufa akijuta. Angejua Jeff ndiye mwanaye wa pekee, angekubali kumwacha kwenye mikono ya baba mwingine? Angefunuliwa kuwa Jeff angekuwa tajiri namba moja duniani, unadhani angemtelekeza?
Hata hivyo usimlaumu sana Ted.

Alitapeliwa na ujana. Siku zote elewa hili, ujana ni tapeli mkubwa mno kwenye safari ya maisha.

Luqman Maloto
Hata kama angemlea, asingemfikisha alipo fika Jaff. yamkini angekuwa mcheza sarakasi Kama baba yake!! mambo ya silini ni ya Mungu!! ulishawahi kujiuliza?? vipi Kama Baraka Obama asingetelekezwa huko Hawaii! vipi Kama Babaake angelinchukua mamaake na kuja nae Kenya Obama angekuwa rais wa marekani?? siangekuwa mjaluo kama wajaluu wengine??? yamkini angesoma Kenya!! angeiga siasa za Kenya nk!!
Ni mtazamo wangu!
 
Ukija kwa kijana wenu tu hapa hapa Tanzania, Nassibu Abdul unadhani babake angejua kijana angefika hapa unadhani angemuacha?
Hkn asiyependa. Kukaa na mwanae Duniani.kufanikiwa kwa mwanae hata asipompa kitu.But
Ki mama kili ngangania kutambaa na nasibu.
Kikapotelea kusikojulikana sas je! Km hupendi asonge mbele kimaisha ulimzaa wa nini? Wkt kuna vidonge vya majira?
Hkn atakae kujali Dunani km Baba na Mama baaaaas!
 
Nimeingia wikipedia hili jambo limenishangaza sana,anasema mara ya mwisho kumuona mwanae ni wakati akiwa na miaka mitatu tu....yaani only three years hata alipoulizwa tena kama anajua mtoto wake anafanya nini saa hizi anasema hajui kama mwanae amepata kazi au ni jobless au kama amekufa,hivi hawa jamaa huwaga wanajitambua kweli?!

Ajabu sana hii.
 
usilolijua ni sawa n usiku wa giza pia kil jambo linatokea kwa wakati wake uendaa ikawa jeff asingekuwa Tajiri kam angelelewa n baba ake mzazi
Je kwenye maono ya Jeff na kisa hiki akitambua haya maono Hadi kuwa anamkwepa baba yake au ni ego za ubinadamu kwamba baba alinitelekeza?
Maana nahisi huyu tajiri Ana maono ya kutomsogelea baba yake Ili kulinda mali zake kwa sababu katika Hali ya kawaida hangeweza kumsaidia kidogo dingi yake hata kama alimtelekeza
 
Yote kwa yote kama mimi ningetambua ukweli nisingeacha kumtunza mzee, wote tunafanya makosa.
Mashaka yangu ni kwamba bwana tajiri alipewa maono ya kiapo au kwamba aliambiwa siri ya utajiri ni kukaa mbali na mzee la sivyo atarudi umaskini maana kwa Hali ya kawaida kibinadamu angeweza kumsaidia japo kidogo
 
Ilikua lazima Yusuph achukiwe na kaka zake, auzwe Kama mtumwa Misri ili ndoto yakua mtawala itimie.
Na Hali hiyo ilikuja kuwaokoa familia na Taifa
Kimsingi haya maisha na hatima ya Kila mtu anapanga Mungu ni beyond one's control
Sio Kila jambo baya kwako limekuja kwa ubaya bali lina kusudi la Mungu ko tusipende vya kulaumu Sana tufanye sehemu yetu na tumuambie Mungu atimize kusudi na mapenzi yake japo kibinadamu naumia
Yaani dizaini ya Yesu aliposema hiki kikombe kukinywa ni mziki but kwa makusudi yako acha nipambabe Mungu atamshindia na ndivyo ilivyokuwa
 
Back
Top Bottom