Usifanye mchezo na pesa

Usifanye mchezo na pesa

Za asubuhi wana MMU.

Jamani nilichokiona jana nimeshindwa kukiamini ila inabidi tu niamini.

Kuna rafiki yangu ana mpenzi wake kiukweli walipendana yaani hata mimi niliyapenda mapenzi yao hadi wakaanza kufanana, ila yule msichana amesoma hadi form 4 akapata zero na jamaa yeye aliishia la saba kwa hiyo maisha matamu hapo.

Shetani mbaya sana kutokana na uzuri wa msichana kuna babu mmoja ambaye ukweli pesa anazo akija ni full mashauzi kila siku gari mpya za hatari sana suti zisizogusika na mengineyo! kamposa msichana na hatimaye amemuoa.

Siku ya ndoa vijana wa karibu na rafiki yetu tulipata kazi ya kujitolea maana ilibidi tulipwe jamaa kataka kuanzisha bonge la vurugu harusini na alivyo kipande kumzuia shughuli pevu.

Ila hatimaye ndoa imefungwa mke kachukuliwa jamaa kabaki analia kama mtoto gheto.

Jamani pesa nimeivulia kofia.
likikukuta wewe unafanya nini maana jamaa anataka ushauri jinsi gan atamrudia mpenzi wake.

Nawasilisha

Mwambie atafute hela, ndio mpango mzima. Mambo ya kupigana yameshapitwa na wakati.
 
amrudishe wa nini? nyie si ndio mnasemaga wanawake wengi tu? au wamepungua ghafla?

Hahaha, dah DEMBA ,majibu yako tu mimi hoi, kweli kui hakukosea kusema majibu yako mafupi lakini nguvu yake si mchezo!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: kui
Mtoa thread ndio ametoka jeshini anajiandaa kwenda chuo. Anyway nenda chuo katulie usome kwa bidii weka mapenzi kando
poa nakusubiri baada ya miaka minne na wewe uweze kufika nakuombea kwa mungu sawa mkuu!!!
 
Pesa sabuni ya roho, hiyo ndo fact, hakuna cha ziada cha kumshauri huyo
 
Mapenzi yanauma sana jamani sumu yake ni kali kushinda hata ya nyoka,inakumaliza ndani kwa ndani,ila huyo mwanamke hakuwa na msimamo ni tamaa ya pesa ila hatofaidi ndoa maana hizo pesa zina mwisho wake.
Duh kama namuona jamaa anavyo ugulia maumivu,malipo ni hapa hapa duniani na kama demu alimkimbia mshikaji kisa hela basi akumbuke huko alikokimbilia kuna mawili anaweza akawa anafaidi pesa za huyo jamaa au akawa hana amani na ndoa yake na pesa zote akaziona sikitu,mshikaji atulie tu amuombe mungu yote yatapita na atapata mwenye real love kwake
 
Hahaha, dah DEMBA ,majibu yako tu mimi hoi, kweli kui hakukosea kusema majibu yako mafupi lakini nguvu yake si mchezo!
haa haa mkuu hapa ndipo watu waelewe maana ya mapenz wanawake wanaweza kuwa wengi lakini huwezi kumpenda kila mwanamke!!!!
 
Last edited by a moderator:
sio kama hatafuti pesa noo!!! anatafuta ila mipango haijakaa sawa kwa nn usimvumilie mbona wao wanawavumilia sana!!!

lini mlituvumilia wakat mnachepuka ovyo, mipango ya wenzie ilikaaje sawa yake isikae sawa??? tukiwavumilia mnabweteka, tafuta pesaaa
 
Back
Top Bottom