Usifanye mchezo na pesa

Usifanye mchezo na pesa

The End..

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
4,362
Reaction score
3,846
Za asubuhi wana MMU.

Jamani nilichokiona jana nimeshindwa kukiamini ila inabidi tu niamini.

Kuna rafiki yangu ana mpenzi wake kiukweli walipendana yaani hata mimi niliyapenda mapenzi yao hadi wakaanza kufanana, ila yule msichana amesoma hadi form 4 akapata zero na jamaa yeye aliishia la saba kwa hiyo maisha matamu hapo.

Shetani mbaya sana kutokana na uzuri wa msichana kuna babu mmoja ambaye ukweli pesa anazo akija ni full mashauzi kila siku gari mpya za hatari sana suti zisizogusika na mengineyo! kamposa msichana na hatimaye amemuoa.

Siku ya ndoa vijana wa karibu na rafiki yetu tulipata kazi ya kujitolea maana ilibidi tulipwe jamaa kataka kuanzisha bonge la vurugu harusini na alivyo kipande kumzuia shughuli pevu.

Ila hatimaye ndoa imefungwa mke kachukuliwa jamaa kabaki analia kama mtoto gheto.

Jamani pesa nimeivulia kofia.
likikukuta wewe unafanya nini maana jamaa anataka ushauri jinsi gan atamrudia mpenzi wake.

Nawasilisha
 
Atamrudiaje mke wa mtu.....?......akaze moyo........maisha mbona bado matamu sana........
 
yaani anataka ushauri amrudie mke wa mtu.
Mi namshauri atafute hela tu.
 
Atulize moyo apampata mzuri kuliko huyo, wazuri ni wengi sana labda kutokana na kutokutembea ndio maana hawaoni. Huyo hakuwa na mapenzi ya dhati kwake.
 
Yesu mwenyewe aliuzwa kwa pesa,sembuse huyo....acha afate patamu bhana.
 
Atulize moyo apampata mzuri kuliko huyo, wazuri ni wengi sana labda kutokana na kutokutembea ndio maana hawaoni. Huyo hakuwa na mapenzi ya dhati kwake.

Hata akimpata mzuri, bila kumpa pesa ni sawa na kuwa na uwalaza bila elimu.....utaishia chomwa jua tu
 
ushauri wa nini sasa hapo ni kukaza roho tu na mwenye kosa sio hiko kibabu ni huyo X wake
 
Hata akimpata mzuri, bila kumpa pesa ni sawa na kuwa na uwalaza bila elimu.....utaishia chomwa jua tu

jamani lakini pindi mnaanza mapenzi si huwa mnakubaliana sasa inakuwaje mnaumizana tena!!!!
 
Hiyo imetoka.....Mlivyoambiwa m/Mme kazi ndio utafute pesa.
 
Mwambie atafute pesa tu maana ndo silaha tosha.... huyo sio mke wake tena.. mdada mwenyewe kafanya bila kusurutishwa... aendelee na maisha tu mana majanga kama hayo yapo yeye sio wa kwanza... asiumie sana
 
me namshauri akatafute pesa tu, ikibidi akaombe kazi kwa mzee, mzee akitoka anajikumbushia na mpenzi wake......

mmmh patamu hapo!!
 
me namshauri akatafute pesa tu, ikibidi akaombe kazi kwa mzee, mzee akitoka anajikumbushia na mpenzi wake......

mmmh patamu hapo!!
yaah!! umeongea point tabibumtaratibu ni bora akatafute kazi kwa yule yule mzee ili picha lianze upya!!!!!
 
pesa just peace of paper bt ina nguvu ya kubadilisha mfumo mzima....

yule mke wa mutu yeye atafute mnyonge mwenzie

pia mwambie atafute demu wa type yake mtoto anahitaji pesa yeye hana watoto wazuri ataishia kuwaita shemeji

sasa hivi atafute pesa sana
 
Mwambie atafute pesa tu maana ndo silaha tosha.... huyo sio mke wake tena.. mdada mwenyewe kafanya bila kusurutishwa... aendelee na maisha tu mana majanga kama hayo yapo yeye sio wa kwanza... asiumie sana

asiumie sana!!!!!!!!!!
watu mpaka walianza kufanana mkuu usifanye mchezo!!!!
hali inakuwa mbaya pale atakapotaka kufanya kitu ambacho alifanyiwa na mwenzie halafu anakumbuka hayupo!!!
jamani mapenzi haya!!!!
 
Back
Top Bottom