Usifanye Makosa haya pale uhusiano wako wa kimapenzi unapofikia mwisho

Cybercurex

Member
Jan 19, 2023
76
177
Kuachwa huleta hisia za maumivu, hasira na uchungu moyoni. Hisia hizi hutofautina kati ya mtu na mtu, hutegemea jinsi hali hii itamuathiri vipi na hatua zipi atachukua kupona maumivu haya.

Leo ningependa tujadili makosa yanayofanywa na wengi baada ya kuachwa yamkini hata wewe uanayesoma. Makosa hayo ni kama ifuatavyo;

Kujilaumu na kuona ulifanya makosa sana,hali hufanya mtu kujiona na hatia, kujitenga na kuwa mpweke, kujichukia, na hata kujidhuru kimwili au kujaribu kujiua. Kubadilidha wanaume/wanawake ili kusahau maumivu ya kuachwa au kumkomoa aliyekuacha, tabia hii ni hatari kwasababu humuweka mtu kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya zinaa.

Kutangaza kwenye mitandao ya kijamii, kwa kutia huruma mitandaoni au kumpiga vijembe, kumtukana sana aliyemuacha kwamba amepoteza mtu wa maaana au kumtabiria ugumu wa maisha aliyemuacha. Kutumia pesa nyingi ili kushawaishi warudiane au kumdhuru aliyemuacha au mwenza mpya aliyenaye. Matumizi pombe kupita kiasi, madawa ya kulevya, bangi na sigara ili kutuliza maumivu ya kuachwa.

Kuingia kwenye mahusiano mapya haraka haraka ili kuondoa maumivu na matokeo yake ni kuwa na mtu asiyempenda au kuwa na mahusiano yanayoyumbayumba. Kutangaza siri za aliyemuacha kila sehemu ili kumchafua kwa marafiki zake na watu wake wa karibu mfano mtu mwenyewe ana kibamia, mara mchawi, dume suruali na mengine mengi kwa lengo la kutoa sifa mbaya.

Hata hivyo tabia hizi hazina faida yoyote zaidi ya kuchochea hasira, uchungu, chuki na maumivu moyoni, wivu kupita kiasi, kukosa furaha na magonjwa yatokanayo na zinaa au magonjwa kama vidonda vya tumbo, presha, magonjwa ya akili, kuzorota kwa utendaji kazi, na hata kugombana na kila mtu.

Ni vema zaidi kumuona mtaalamu wa afya ya akili kama utashindwa kujidhibiti mwenyewe.
 
Hizo ni dalili za depression. Hii sio kitu nzuri mtu asipo dhibiti
 
Tabia ya Kiswahili sana hii
Sana ..
Kuna wengine anakufata page yako ya insta...au kama ana picha yako anakupost na Kuku tag huku anakumwagia matusi ...
Yaani unabaki kushangaa ...wanaokujua wanakwambia tumeona insta ..au ingia insta..
Unaweza kuta wewe hata huko insta hujaingia mwaka mzima lakini ushapostiwa na ushatukanwa vya kutosha..
 
Back
Top Bottom