Wanawake: Funguka jinsi ulivyopigwa matukio wakati wa mahusiano

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,514
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Kama kuna kipindi ambacho kinakuwa kina matamu na machungu ni kipindi hiki Cha mahusiano ya mapenzi kwa wadada.

Nasema kitamu kwakuwa ni kipindi ambacho mdada anakuwa anakutana na mkaka ambaye anampenda..

Wanaingia katika mahusiano ya mapenzi na mapenzi yanakuwa motomoto.

Hapa kuna kuwa na hali ambayo mdada anajisikia moyoni mwake ya furaha.

Hii ni kulingana na kuwa na hisia za mapenzi kwa huyo mkaka.

Kinakuwa kichungu tena kipindi hiki ambapo dada atakutana na mkaka ambaye anampenda lakini kaka huyu anakuwa anampendea utamu wake.

Uchungu unaanzia hapa maana dada anapompa tu utamu kaka anatoka nduki na kumuacha mwanadada na uchungu..

Hiki ndio kipindi ambacho wanawake wanakuwa hawajui nani ambaye ni sahihi kwake hivyo anakuwa macho juu juu.

Matukio mbalimbali ambayo wanayopitia wanawake katika kipindi hiki wanayajua wao wenyewe.

Kama sio kumpenda mtu asiyekupenda basi ni kuzalishwa na kuachwa na kama sio hivyo ni kutembea na wanaume wengi.

Hayo ni baadhi tu nimeweka najua yapo mengi ambayo yapo..

Nimeona nilete Uzi huu kwakuwa wahanga wa kubwa wanakipatapata katika kipindi hiki ni wanawake.

Wanapigwa matukio na wanabaki na maumivu makali, ambayo hata baadae wanaolewa ila mioyo imejeruhiwa..
 
Back
Top Bottom