Usiende kumdai mtu pesa kama hauna pesa mfukoni

vibesen xxx

JF-Expert Member
Jul 23, 2022
2,668
5,278
Kama ulimkopesha mtu pesa iwe kubwa au ndogo usiende kutaka dai lako kama wewe hauna pesa mfukoni

Unapoenda kudai pesa yako huku wewe ukiwa hauna pesa mwisho siku hauwezi kuwa mzuri. Unaweza kushindwa kujizuia mkaingia kwenye mgogoro mkubwa

Na usikopeshe pesa hovyo mkopeshe mtu
Aliyefiwa
Anayeuguliwa
Mwenye njaa/aliyekosa chakula
Anayehitaji dhamana polisi
 
Daa umenena jambo kubwa sana.Nilisafiri mwende wa nauli ipatayo 50,000/- kwenda na kurudi kufatilia shilingi zangu angalau zilikuwa M. hivi na point.Nafika namkuta mdeni wangu anamachungu mengi,kuongea naye anasema mama yake kalazwa na yeye ndo kichwa na hana hata kumi ya kulipia dawa!
Kama nisingekuwa na kitu mfukoni sijui!
 
Ni kweli deni linatia hasira kwasababu unajua ni haki yako kulipwa kwa wakati wowote,akili huwa na matarajio ya hali ya juu kupata deni lako

Ikitokea tofauti kama hauna akiba mfukoni mnaweza kuingia kwenye mgogoro mkubwa ambao si nzuri

Na wewe usingekuwa na akiba mfukoni usingesikiliza unayemdai kwamba anauguliwa
Daa umenena jambo kubwa sana.Nilisafiri mwende wa nauli ipatayo 50,000/- kwenda na kurudi kufatilia shilingi zangu angalau zilikuwa M. hivi na point.Nafika namkuta mdeni wangu anamachungu mengi,kuongea naye anasema mama yake kalazwa na yeye ndo kichwa na hana hata kumi ya kulipia dawa!
Kama nisingekuwa na kitu mfukoni sijui!
 
Ndugu msomaji,,,, pitia hapa uwasilikilize Wakopeshwaji wanasemaje...

Nlienda kumdai mama mmoja aliekopa kwenye ofc yetu mazngira nlyomkuta ilbid mm ndio ntoe hela mfukon kumsaidia wakat nlijiandaa kwa shar, tuko apo mtoto wake kaletwa na walim kaanguka shule na hyo n kwasababu toka walvyokula jana yake mchana hawajala tena
 
Madeni ni mtihani sio kwa anayedai tu hata anayedaiwa
Ndugu msomaji,,,, pitia hapa uwasilikilize Wakopeshwaji wanasemaje...

Ipo hivyo pesa ya kukopesha ni kama ya kulipa ada ya mwanafunzi inaweza ikarudi au usirudi
Nlienda kumdai mama mmoja aliekopa kwenye ofc yetu mazngira nlyomkuta ilbid mm ndio ntoe hela mfukon kumsaidia wakat nlijiandaa kwa shar, tuko apo mtoto wake kaletwa na walim kaanguka shule na hyo n kwasababu toka walvyokula jana yake mchana hawajala tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom