Usiache kuwa na shukrani

Usiache kuwa na shukrani

Mmiskiry

Member
Joined
Mar 1, 2018
Posts
55
Reaction score
21
*Vigezo vilivyokuwezesha wewe ukapata kazi, ndivyo vigezo alivyonavyo mwenzako lakini akakosa kazi.*

*Dua uliyomuomba Allah na ukajibiwa ni hiyo hiyo anayoiomba mwenzako lakini hajajibiwa.*

*Barabara upitayo kwa salama kila siku ndio hiyo hiyo inayowaua wenzako kwa ajali.*

*Sehemu unayoabudia na ukaneemeshwa ndipo hapo hapo wenzako wanapoabudu na bado wakawa na dhiki.*

*Kitanda ulicholazwa hospitali na ukapona na kutoka ndicho hicho hicho wenzako walichofia.*

*Mvua iliyorutubisha shamba lako ndiyo hiyo hiyo iliyoliharibu shamba la mwenzako.*

*Kuwa na shukurani kwa ulichojaaliwa, kwani hayawi kwa nguvu zako wala uhodari wako bali ni kwa idhini ya Mola wako.*
*Kumbuka yeye ndie mtoaji wa kila ulichonacho.*
ZINGATIA

#Like, #Share, #Comment
_*USIACHE KUWA NA SHUKURANI.*_
 
Back
Top Bottom