Usiache kuijua kiundani hii nchi ya Brunei

Usiache kuijua kiundani hii nchi ya Brunei

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
images

pbl-sir-noel-brunei-darussalam-4-638.jpg


1. Brunei ukipenda iite 'Darusalaam' ama nyumba ya amani ni nchi ambayo raia wake hawalipi kodi yeyote (All citizens in Brunei, including expats, do not have to pay for taxes, for it is absolutely free.), Hata maisha ya wananchi wake ni mazuri na mshahara wa chini kabisa ni dola 25 kwa saa (Tshs 50,000) huku ukosefu wa ajira ukiwa ni wastani wa 5% tu. Serikali inalipa gharama zote muhimu, mpaka chakula kinalipiwa ruzuku. ukifanya kazi kule hakuna income tax (There is no personal income tax or capital gains tax). Sultani anasimamia vizuri sana export ya mafuta na gesi na wanachi wanakula bata watakavyo.
GDP ya Brunei imepanda hadi 56% kuwa nchi ya tano duniani (16.11 billion USD in 2013) na IMF wanasema nchi hiyo haidaiwi HATA MIA....

GDP-and-GDP-growth1.png

2. Sultan wa Brunei Mohammad Hassan Bolkiah ndiye Raisi tajiri kuliko maraisi wote duniani, Maarufu kwa utumiaji wa dhahabu kwa kila kitu, hali ila na vijiko vya dhahabu, na nguo anazo vaa zimepambwa kwa dhahabu na fedha. Huyu anamiliki Jumla ya MAGARI 5000 YA KIFAHARI (tazama kasri na moja ya gari lake lake la dhahabu tupu pichani) .Sultan huyu anamiliki pia ndege aina ya Boing 747 thamani yake ikiwa ni dola milion 100 ambamo pia nakshi pekee ni dola milioni 120 humo utakuta vyoo na vyumba vya dhahabu, pia anamiliki ndege ndogo sita na helicopta moja. Arusi ya mtoto wa Sultan wa Brunei ilifanyika kwa muda wa siku 14 kwa gharama ya 5 milion dolla huku watu wote walioalikwa wakila na kunywa na kusaza, na kuhudhuriwa na zaidi ya maraisi 25.
sultanMS2107_468x464.jpg


3. Elimu ni Bure kabisa na watoto chini ya miaka 12 HUTIBIWA BURE huku watu wazima wakilipia dola 1 tu kwa Matibabu. Kadhalika ukioa tu unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiano mkubwa wa watu na magari (1:209)-Ikiwa hakuna tiba ya ugonjwa wako Brunei unapelekwa nje ya nchi hasa Malaysia na Singapore kwa gharama za serikali
Scholarships+in+Brunei.jpg


4. Pombe imepigwa marufuku kabisa kisiwani Brunei ingawa wageni wanaweza kuagiza kiwango chenye ukomo na Hakuna NOA/NGURUWE hata mmoja nchi nzima....................
5. . Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada kuonesha kitu. Kidole gumba tu hutumika kupoint kitu na ni Lazima kuvua viatu unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei
6. Hii inatumia mfumo wa SHARIA ambapo 'Wezi hukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe'. Mwaka 2014 ilipitisha sheria ya kupigwa kwa mawe hadi kufa yeyote atakayebainika anafanya USHOGA (Homosexual) lakini kwa uthibitisho wa mashahidi WANNE.....Unaweza kusherehekea Noeli (X-mass) lakini si kwa kuweka mapambo yake..........
images


7. Ingawa Kisiwa cha Brunei Kina BUNGE lakini nchi hiyo HAINA UCHAGUZI......Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 1962, kuna chombo kimoja tu cha habari kinachomilikiwa na Serikali...ni aghalabu sana kwa media kuipinga serikali
pbl-sir-noel-brunei-darussalam-11-638.jpg



8. 93% YA WATU WOTE WAMEENDA SHULE KWA KIWANGO CHA LAMI (Degree)
upload_2016-8-7_16-28-7.png


MODS KINDLY STICK HUU UZI TOKA VYANZO MBALIMBALI IKIWEMO JF YENYEWE ....
 
Nimefukuzia scholarship huko, ila bado sijakata tamaa
 
[emoji23] [emoji23] nimecheka hapo mwisho eti kiwango cha rami. Ila nchi kama inahudumia wananchi wake vyema kuna haja gani tena ya Demokrasia? Na usiwepo tu huo uchaguzi maana huku kwetu tunachaguana kila uchao ila ni masikini wa kutupwa.

Kwa nini tusimuongezee muda Magufuli na sisi.
 
[emoji23] [emoji23] nimecheka hapo mwisho eti kiwango cha rami. Ila nchi kama inahudumia wananchi wake vyema kuna haja gani tena ya Demokrasia? Na usiwepo tu huo uchaguzi maana huku kwetu tunachaguana kila uchao ila ni masikini wa kutupwa.

Kwa nini tusimuongezee muda Magufuli na sisi.
demokrasia sie inatudidimiza zaidi
 
Na huwa nachukizwa sana na kauli za kusema Magufuli anakandamiza Demokrasia mbona JK aliiacha itambe lakini bado tupo palepale?
sijamgusa magufuli hapo kwa makusudi kwa sababu pia nimemaanisha pisitively na negatively, kama watu wanadai demokrasia kuandamana tu muda wote ama kulumbana na serikali kadhalika akija rais mpole anaitwa dhaifu akiwa mkali anaitwa dikteta
 
[emoji23] [emoji23] nimecheka hapo mwisho eti kiwango cha rami. Ila nchi kama inahudumia wananchi wake vyema kuna haja gani tena ya Demokrasia? Na usiwepo tu huo uchaguzi maana huku kwetu tunachaguana kila uchao ila ni masikini wa kutupwa.

Kwa nini tusimuongezee muda Magufuli na sisi.
Achana na uchwara wewe
 
Dah! watu tunaishi lkn tunaishi kwa kutofautiana
 
Labda na sisi gas na mafuta vitatusaidia tuwe zaidi ya Brunei
 
Natamani ningepata uchambuzi kama huu huu ila kwa Tanzania.....
 
Back
Top Bottom