Usia wangu kwa Zitto na washirika wake

Usia wangu kwa Zitto na washirika wake

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,209
Ndugu zangu,
Watanzania tuna usemi usemao "Mungu hamfichi mnafiki". Usemi huu umethibitika kupitia malumbano ambayo yamekuwa yakiendelea kwa siku kadhaa hapa JF. Kwa muono wa haraka haraka tunaweza kutambua kwamba wote wanaolumbana ni wasaliti kwa CHADEMA na wamekuwa siku zote wakijipambanua kama wapiganaji wakati kwa hakika walikuwa ni wanafiki na wasaliti wakubwa wa watanzania wanaiangalia CHADEMA kama chama mbadala kwa ukombozi wa nchi yetu. Nashawishika kuamini kwamba CHADEMA ina Mungu, na Mungu hajataka hawa akina Ben na kundi lake waukwamishe mpango wa Mungu. Hatimaye ameamua kuwaweka peupe na kuwafanya wafarakane wao kwa wao. Kwa hakika hii ni hatua mhimu sana katika kuelekea kuwa na CHADEMA yenye umoja na malengo ya aina moja ya kushika dola na kuwakomboa watanzania. Maana kama hawa wanafiki wangeendelea kuwepo hadi 2014, ni dhahiri wangekwamisha juhudi nyingi za kuiwezesha CHADEMA kuchukua madaraka katika serikali za mitaa na hata nchi mwaka 2015.
Nimezisoma kwa umakini mkubwa sana hoja zote za upande wa Ben, na ule wa akina Machange. Na nina mambo kadhaa ambayo nimeyaona hapa, na ningependa niseme machache kutokana hoja hizi.

Katika mabandiko ya Ben na Mamuya, wote kwa pamoja wanakubali kwamba Ben alikuwa ni mmoja wa waasi na alishiriki kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza mipango na mikakati ya kukihujumu chama na hasa uongozi wa juu wa chama (mwenyekiti na katibu mkuu wa chama), lakini baadaye akajiondoa kwenye hili kundi na kuanza kulipinga. Katika bandiko la Mchange na Mwampamba wao kwa pamoja wanaonyesha kwamba Ben ndiye aliyekuwa mwanzishaji wa hili kundi lililolenga kukivuruga chama. Na inaonekana alifanya hiyo kazi kwa kutumia kiasi kikubwa sana cha pesa. Lakini hawasemi baadaye ilikuwaje na ni kwa vipi walishindwa au walifanikiwa kutekeleza hiyo mipango ya Ben Saanane. Lakini hoja hizi zinaonekana kuwa hazina uzito kwa kuwa tayari Ben alishakiri kwamba alikuwa ni msaliti kwa chama. Kwa hiyo Ben amewawahi (pre-empty) akina Mwampamba katika hili kwa kuwa tayari tunafahamu ushiriki wa Ben katika haraka za kumhujumu Heche na hata uongozi wa juu wa CHADEMA.

Lakini la pili, ukisoma kauli za akina Mchange, Juliana, Mwampamba na mtu anayeitwa Taswira, inaonekana kwamba Ben Saanane alikuwa anatumwa na Dr Slaa kwenda kuunda hilo genge la kukihujumu chadema na uongozi wa juu wa CHADEMA. Hii hoja haileti maana kabisa. Sidhani kama hata mtoto mdogo anaweza kukubaliana na upuuzi huu kwamba Dr. Slaa alimtuma Ben akaandae kikundi cha kumhujumu yeye Dr. Slaa. Huu ni ulimbukeni uliopindukia. Na katika hili, nafikiri ant-Ben, wamekoboa. Hawana hoja ya msingi hapa. Ni wazi kwamba Dr. Slaa anatamani kubaki na jina lililosafi mbele ya jamii na atakuwa ni mwendawazimu iwapo ataamua kuandaa kundi la kuchafua yeye mwenyewe. Hapa hamjanishawishi bado. Mkatafute sababu nyingine.

Tatu, Mchange anasema, Ben alikuwa anamtafuta Zitto ili akifadhiri kikundi, wakati Mwampamba anasema Ben alikuwa anamtafuta Zitto ili ampe sumu. Hapa kuna mchanganyo tayari. Inaonekana hata hamjajipanga na kuelewa ni nini mnataka kukiwasilisha kwa jamii. Katika hili Napata hofu kwamba hili kundi la akina Mchange lilikuwa linamlisha Zitto maneno ya fitina na uchonganishi dhidi ya Ben kwa kuona kwamba Ben amejitoa kutoka kwao. Zitto, ni vema ukayachunguza kwa umakini mkubwa maneno ya hawa akina mchange na mwampamba. Anayetaka kukulisha sumu hawezi kufanya kazi ya kukutafuta mchana kweupe. Atatumia njia nyingine yoyote lakini siyo kuja uso kwa uso anakutafuta. Hivi unataka kusema kama Ben alikuwa amepewa pesa ya chama ya kuhakikisha anakuua angeshindwa kukutafuta popote? Hata Dodoma angekufuata ukiwa bungeni. Kama hawa jamaa zako walikuwa wanakuambia haya, ni dhahiri yana walakini.

Nne, wakati Mchange na Mwampamba wakidai kwamba Ben ndiye aliyekuwa analifadhiri kundi la kukihujumu chama na kuwachafua viongozi wa chama. Ushahidi wa kimazingira unaonyesha kwamba Tuntemeke and company walikuwa wapo busy kuzunguka kwenye mitandao ya kijamii (facebook, jf etc) kumchafua Dr Slaa kwa maneno ya hovyohovyo, na kuwauzia akina Nape siri za ndani za chama na za Slaa, ili kumfanya Slaa adharirike na kupoteza mvuto ndani ya chama na kwa jamii kubwa ya watanzania. Lakini ni bahati mbaya kubwa kwamba hakuna popote nilipoona Ben akimkashifu kiongozi yeyote, si Zitto wala Slaa au kiongozi wa juu wa CHADEMA. Kama kwa hakika Ben ndiye aliyekuwa analifadhiri hili kundi la uasi ni vipi tena kundi hili likaifanya kazi ya Ben kiufasaha, na kumsafishia Zitto njia ya kuelekea kwenye Uraisi ilihali halikubaliani na hoja za Ben. Hapa kimantiki haiwezekani. Hili kundi lilikuwa linafanya kazi ya mtu mwingine, tofauti na Ben Saanane.

Tano, ukiuangalia mwanzo wa migogoro hii yote ni Zitto kuutaka urais. Na hili kundi linaloongoza propaganda za kumchafua Slaa na kumsifia Zitto lina nia moja tu ya kumuwezesha Zitto kupata Urais. Hili kundi linamwona Slaa ni tishio ndani ya chama kwa nafasi ya urais, na hivyo linajaribu kuibua kila aina ya propaganda ili kumfanya Slaa aonekane hafai kwa nafasi hiyo ya urais. Kama tatizo siyo urais, kwanini kundi hili halimchafui Tundu Lissu au Mabere, au Prof Safari, au Mnyika au Mbowe? Tatizo ni Slaa kwa kuwa ana potentials za Urais. Kwa ushahidi wa kimazingira, Zitto ndiye anayelifadhiri hili kundi la akina Mwampamba, Mchange na wenzake wanaoendesha propaganda mbaya dhidi ya Dr. Slaa, ili kumuwezesha yeye Zitto kukubalika zaidi kwa wanachama. Katika hili hamuwezi kujinasua.

Sita, namfahamu Zitto tangu akiwa kiongozi wa DARUSO pale UDSM, ninamfahamu kama ni mtu mwenye misimamo na asiyeyumbishwa na kitu chochote. Ni mtu anayejiamini, asiyemwogopa mtu wala matokeo ya misimamo yake. Lakini pia namfahamu kama ni mtu mpenda madaraka sana. Na hili limejionyesha pale alipoanza harakati za kuutafuta uenyekiti wa CHADEMA, na baadaye kuutafuta urais. Ni dhahiri akibahatika kuwa Rais wa Tanzania atautaka pia Urais wa Africa Mashariki, Africa na hatimaye urais wa dunia kama utakuwepo. Mimi sipingani na uchu huo wa madaraka ilimradi anaamini kwamba anao uwezo wa kuongoza, maana hiyo ndiyo demokrasia. Lakini sikubaliani na approach yake ya kuutafuta urais, wenzake wote wanaoutafuta urais hata wale wa ndani ya CCM hadi hivi leo hawajajitangaza, yeye amejitangaza ili kiwe nini kama si kwa nia ya kujenga haya makundi ya akina Mchange? Zitto usipokuwa makini, hata kama utapata urais, unaweza kuwa Rais mbovu kumshinda hata Kikwete. Na unaweza ukaua kabisa matumaini ya watanzania dhidi ya vyama vya upinzani.

Lakini zaidi ya yote, Zitto una bahati mbaya sana kwamba watu uliowachagua kukupigia debe au kukubeba kuelekea huko unakotaka kufika ni weupe mno katika uwezo wa kuchambua mambo. Hili nimeshakuandikia mara kadhaa. Hivi watu kama akina Mchange, Mwampamba na Juliana utawalipa fadhira gani utakapotokea kuwa Rais? Nadhani hata kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya tu hawawezi kufit, kwa jinsi wasivyojua kupembua mambo. Hawa watu uliowatuma wakupigie debe na kumkashifu Dr. Slaa ili apoteze mvuto mbele ya jamii na akose sifa ya kugombea Urais ili wewe ugombee, wamekosa maarifa ya kufanya kazi hiyo. Badala ya kukupigia debe wenzako wanakisambaratisha chama. Ni mwendawazimu tu atakayeanza kulivunja daraja kabla hajavuka mto. Wewe unautaka urais halafu daraja la kukupeleka kwenye urais unawatuma akina Mchange na kundi lake walivunje. Kwanini usingetulia, ukashirikiana na wanachama wenzako, mkajenga umoja wa chama, mkakitangaza na kukikuza chama kwa bidii, na baadaye watu wakuone kwamba unaweza, na wakupe hiyo nafasi? Kwanini usifanye mambo mazuri ndani na nje ya chama ili sisi tukuone kwamba unatufaa kuwa rais? Rejea kauli ya Butiku pale Nkurumah.

Zitto, kwa sasa huna sifa za kuwa Rais. Ukishaona unajiandaa kuingia kwenye mpambano halafu mpinzani wako anakusifia, basi ujue huna kitu wewe. Ni ajabu sana kwamba akina Nape, Le Mtuz na January Makamba wanakusifia wewe na kumkashfu Slaa. Kwa mazingira haya tu, ni dhahiri kwamba Slaa ndiyo tishio kwa CCM na si wewe. I am sorry, lakini huo ndiyo ukweli. Nadriki kusema kama nia ni kupata Rais kijana, basi John Mnyika au Tundu Lissu wanaweza kuwa macandidate wazuri zaidi kwa nafasi ya urais kuliko wewe. Ni vema ujitafakari, na uangalia misimamo na determinations za hao niliowataja, halafu jilinganishe na wewe.

Mwisho, napendekeza kwamba, kwa kuwa unafiki wenu umeshawekwa wazi, basi yavunjeni haya makundi mliyoyaunda ya kummaliza Dr Slaa kisiasa, mrudi chamani mkaombe radhi kutokana na ushiriki wenu wa kukihujumu chama na hatimaye mrudi katika harakati za kukijenga chama ikiwemo kushiriki kikamilifu katika vuguvugu la mabadiliko linaloendeshwa na CHADEMA hivi sasa. Miaka mitatu iliyobaki inatosha sana kujijenga kisiasa na kurudisha imani ya watanzania kwenu. Pengine japo mtaambulia ubunge. Kwa kuwa tumeshayaskia mengie yatokayo kwenu, napendekeza pia, tuishie hapa, turudi kwenye vikao tukayamwage yote, na kukubaliana juu ya njia nzuri ya kujenga umoja wa chama kwa maslahi ya watanzania. Kuendelea kuleta watu wajiandikishe kwenye JF na kuleta ushahidi wa uongo kwa sasa hautasaidia tena. Ushahidi wa kimazingira upo wazi kwamba kuna hujuma dhidi ya Dr. Slaa.

Lukolo

Dar es salaam

Hongera Lukolo, kwa good and balanced analysis.

Naomba kuboresha kidogo kwa ruhusa yako; Matatizo haya ya Prezzo au Dogo au Zitto hajaanza na harakati zake za urais, Yalianza zaman/ mbali, nafikiri baada tu ya ishu ya Buzwagi. Muda huu tunachoona ni matunda ya mbegu aliyoihangaikia kwa damu, jasho na muda wake! Hayo ni ya muda mrefu na ndio maana alikuwa anajenga milki yake ktk ngazi mbalimbali ndani na nje ya CHADEMA mfano BAVICHA, viti maalum nk

Sijui ni kipimo gani unachotumia ndugu yangu, lakini kwangu mimi Zitto hana nusu ya sifa za kiongozi mzuri/bora.
He seems to be a fluke just in a right time (politically). You who know him normally overrates him, mleteni huku kwetu ghafla ni mwepesi mno!

Kuna kitu mnaki ruka naona.
Ben anasema walianzisha PM7 ili iwe vuguvugu la mabadiliko kwa vijana nje ya chama. Ila alipoona PM7 inatumika kutukana viongozi ndipo alipo amuia kuhasi na ameongeza kule kuwa kazii ya kuvunja kundi kimya kimya aliianza siku nyingi chini ya ushahuri wa Kitila.

SOURCE: VIJANA WANAOMHUJUMU DR. SLAA HAwa HAPA

VIJANA WANAOTUMIWA KUMUHUJUMU DR. SLAA.
Nimesikitishwa sana na vijana wenzangu kutumika kisiasa kiasi cha kuudhalilisha utu wao. Kijana aiitwaye EDO MWAMA LALA, aliyekuwa katibu wa BAVICHA mkoa wa Mbeya na Adam CHEGULANI (diwani wa jiji la mwanza aliyenyang'anywa kadi),wote hawa walifukuzwa Chadema kwa kutokuwa waadilifu. Wapo kwenye kibarua haramu cha kuhakikisha wanawashawishi vijana (hasa BAVICHA)kutoa matamko ya kumhujumu Dr. Slaa kisiasa kupitia vyombo vya habari.

Na wameanza mpango wao na kwa kiasi kikubwa wameanza kufanikiwa, kwani wamefanikiwa kumshawishi katibu wa BAVICHA mkoa wa MWANZA, ndugu SALVATORY SHUKURU MAGAFU kutoa tamko kwenye vyombo vya habari kuomba chama kimfukuze Dr. Slaa chamani. Pia leo hii tayari wanaye kijana mwingine maarufu wa chadema, atakae toa tamko muda wowote kuanzia sasa, kijana huyu wamemlipia hoteli moja maarufu iliyopo hapa jijini na kumpa fedha za kutosha ili atoe tamko kali la kumlaani Dr. Slaa.
Wengine ni: Usiwasahahu Juliana Shonza, Grayson Nyakarungu, Habib Mchange, Ben Saanane… tunawafahamu wote na mtu wanayemtumikia ndani ya Chadema… acha hao kina Nape!!
Kwasbabu lengo sio kulumbana wenyewe kwa wenyewe, wakae tu wakifahamu tunawafahamu na muda ukifika kuhangaika nao tutahangaika nao!!!!@ Alex by SeriaMtoto WikiLiks Tumainiel
Wenye nia ya dhati watabaki… wenye nia ovu watajionesha hadharani na wataungwa mkono na waovu wengine!!
Kwa huu mpango (walioupa jina la MWISHO WA SLAA) ulivyo watajitokeza vijana wengi sana watakaotoa matamko kumlaani Dr. Slaa kwa kutumia mwavuli wa BAVICHA imesema. Kwa akili zao zilivyofupi kama maisha ya funza wanadai wanadhamiria kumuua kabisa Dr. Slaa kisiasa. Na vijana wengi wamekuwa wakishawishika na upumbavu huu wa EDO na ADAM kwasababu ya fedha nyingi wanazopewa baada ya kukamilisha kazi hiyo.
Mpango huu unaofanywa na EDO MWAMALALA na CHAGULANI nyuma yake unafadhiliwa na BERNARD MEMBE, MWIGULU NCHEMBA, NAPE NNAUYE, kwa taarifa nilizo nazo na za kuaminika vijana hawa wanalipwa fedha nyingi sana na viongozi hao waandamizi wa CCM na SERIKALI ambao wamekosa sera na kuamua kuingia kwenye siasa za taarabu.
Kwa Binafsi yangu napenda nitoa tamko rasmi la kulaani kwa nguvu zote vijana wote wa BAVICHA wanaoendekeza njaa mbele na kuweka masilahi ya chama kando kuacha mara moja mchezo huu mchafu. Waache kuwa na akili za Samaki na hatimaye wajitegemee kisiasa. Na niwaombe viongozi hawa wa CCM waache kutumia tatizo la umasikini wa vijana hawa kuwarubuni na kuwatumia wenzao kama mipira ya mapenzi.
Ili kuepuka siasa hizi zisizo na tija kwa jamii niwaombe viongozi wenzangu wa BAVICHA kuachana na kujibizana na hawa wapumbavu, kwani ukijibizana na mpumbavu na wewe pia utakuwa mpumbavu, dhumuni lao tutumie muda mwingi kujibizana nao na tupuuze kujadiliana mambo ya msingi kwa mustakabali wa TAIFA.
CHADEMA tutaendelea kuwa na nguvu na kamwe hatuwezi kupunguzwa nguvu na siasa laini kama hizi. Kinachoshangaza ni kuona anayefadhili ushenzi huu ana ndoto za kuwania Uraisi katika nchi yetu, kweli kwa siasa laini hivi uraisi atauweza?
Imekuwa ni kama tabia yake ya kuwatumia vijana kutimiza malengo yake, kwani ni wazi katika mkutano mkuu wa CCM uliofanyika mkoani Dodoma alituhumiwa na wajumbe wenzie kutumia vijana kusambaza vipeperushii vilivyokuwa vikiwaomba wajumbe wa mkutano huo kumkataa Mwenyekiti wao kwa kisingizio cha kumpunguzia majukumu.
Sasa kashindwa huko anakuja kuingilia siasa za CHADEMA kwa kuwatumia vijana wetu wasiokuwa waadilifu; nimwambie kwa upendo tu kwamba CHADEMA TUKO IMARA KAMA CHUMA.
Na. Alex Nicholaus Thomas MUSHI,
Mjumbe wa Baraza kuu la CHDEMA-Taifa,
Mjumbe wa kamati tendaji BAVICHA-Taifa.
UONGOZI WA CHADEMA MAKAO MAKUU IFANYE UCHUNGUZI WA KINA NA KUCHUKUA HATUA KALI NA MWAFAKA JUU YA WANAOTAJWA HAPO JUU INAONEKANA HAO HAWATUMIWI NA CCM TU INAONEKANA WENYE UCHU WA MADARAKA NDANI YA CHADEMA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS 2015 WANATAKA KUGAWA CHAMA KTK VIPANDE KWA KUMDHOOFISHA DR. SLAA KWANI WENYEWE WANAMUOGOPA, KUWA NDIYE MGOMBEA BORA WA CHADEMA WAKIHOFIA KUWA CHAMA CHAKE KITAMSIMAMISHA TENA 2015 KM ILIVYOKUWA 2010 NA AKATULETEA USHINDI MNONO WANACHADEMA.
BAVICHA PIA IWE MACHO MPAKA SASA SIJASIKIA MATAMKO ILIYOTOLEWA NA BAVICHA KUPINGA NA KUDHIBITI UTOMVU HUU WA NIDHAMU UNAOFANYWA NA VIJANA TENA WENGINE WAJUMBE NA VIONGOZI WA BAVICHA WANAOTUMIWA KM CONDOMS NA WAGOMBEA WA URAIS 2015 KUTOKA KTK VYAMA MBALIMBALI WAKIPEWA HELA CHAFU!!
 
Huko kwenye vikao wataongea kitu gani kipya? Hakuna walichobakiza, yote wameshayaongea humu. Iliyobaki ni wao kukutana kwa mara nyingine, waende kwa sangoma wao wakavunje Kamati. Bila kuvunja kamati wataendelea kushambuliana mitandaoni!
 
Hili nalo lina ukweli. Wakati nimeshamaliza kupost ndiyo nashituka kuona kumbe na Juliana keshaleta thread ya kuendeleza mapambano dhidi ya Slaa. Kazi ipo!
 
Hii ipo mahali fulani
 
kwa haya yanayoendelea hivi sasa, Zitto anajimaliza kisiasa.
 
Mkuu LIKOLO uchambuzi wako umetulia naweza soma hata mara mbili tatu,wahusika kama wanaweza waufanyie kazi.kazi ya ukombozi si lelemama kama nilivyokuwa nawaza
 
Utamsamehe msaliti na mnafiki?no way siku zote ataendelea kukufitini tu!dawa ni kufukuza tu,wakaunde chama chao!
 
Hongera Lukolo, kwa good and balanced analysis.

Naomba kuboresha kidogo kwa ruhusa yako; Matatizo haya ya Prezzo au Dogo au Zitto hajaanza na harakati zake za urais, Yalianza zaman/ mbali, nafikiri baada tu ya ishu ya Buzwagi. Muda huu tunachoona ni matunda ya mbegu aliyoihangaikia kwa damu, jasho na muda wake! Hayo ni ya muda mrefu na ndio maana alikuwa anajenga milki yake ktk ngazi mbalimbali ndani na nje ya CHADEMA mfano BAVICHA, viti maalum nk

Sijui ni kipimo gani unachotumia ndugu yangu, lakini kwangu mimi Zitto hana nusu ya sifa za kiongozi mzuri/bora.
He seems to be a fluke just in a right time (politically). You who know him normally overrates him, mleteni huku kwetu ghafla ni mwepesi mno!
 
Hii ipo mahali fulani
Jabulani unaweza kuipost hiyo story bila quotation? Natamani kuiongeza kwenye thread ya msingi kule lakini nashindwa kuicopy kwakuwa ipo kwenye quotation.
 
Tatu, Mchange anasema, Ben alikuwa anamtafuta Zitto ili akifadhiri kikundi, wakati mstari wa Nne, wakati Mchange na Mwampamba wakidai kwamba Ben ndiye aliyekuwa analifadhiri kundi la kukihujumu chama na kuwachafua viongozi wa chama. sasa hawa vilaza mbona wanajichanganya kwy kauli zao, mara waseme ben ndio ana fadhili, mara anamtafuta zitto ili afadhili kikundi. sasa tuwaelewe lipi au ndio kuchanganyikiwa? chama chukue maamuzi magumu hawa ni kuwafukuza tu hakuna cha mchange, mtela, shonza, nyakarungu, gwakisa wote ni kuwa sack out.
 
Back
Top Bottom