Ushuru wa maegesho sasa mpaka ufukweni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushuru wa maegesho sasa mpaka ufukweni

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Jan 15, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280

  Ushuru wa maegesho sasa mpaka ufukweni

  Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 14th January 2011 @ 23:30  KAMPUNI ya Maegesho ya Taifa (NPS), imeanza kukusanya mapato ya uegeshaji katika eneo la ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Coco, Oystebay katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kufuatia agizo lililotolewa na halmashauri ya Jiji.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Hassan Khan, utaratibu huo umeanza rasmi Januari 7 mwaka huu baada ya kupata za kimaandishi, ikiagiza kampuni hiyo kuanza kukusanya mapato kutoka eneo hilo kama ilivyo kwa maeneo mengine ya Jiji.

  Khan alisema kuwa, wakati huu ambapo kampuni yake ikiendelea na shughuli zake kama kawaida za ukusanyaji mapato maeneo ya katikati ya Jiji, wamepokea barua hiyo ikiwataka kuifanya kazi hiyo eneo la Coco kwa muda wa saa nne kwa siku.

  “Ni vyema wananchi wakatambua kuwa kuanzia sasa kampuni hii ya maegesho itaanza kukusanya ushuru wa uegeshaji katika eneo hilo katika hatua ya utekelezaji wa agizo la halmashauri ya Jiji ndani ya mpango wake wa ukusanyaji mapato,” alifafanua Khan.

  Aidha Khan amewataka wananchi kujihadhari na watu wanajifanya kuwa ni wafanyakazi wa kampuni hiyo na kujishughulisha na ukusanyaji wa mapato huku wakitumia tiketi bandia zinazofanana na tiketi zake na kujipatia fedha kwa njia hiyo.

  Katika hatua nyingine, kampuni hiyo imeanza kutumia mashine zake mpya maalumu kwa ajili ya ukataji tiketi za maegesho huku ikielezwa kwamba, zitasaidia kudhibiti mapato yatokanayo na ukusanyaji wa ushuru huo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Mwisho wake hata maegesho ndani ya nyumba ya mtu itabidi uwepo ushuru.........ninasema hili kwa sababu utadaije ushuru kwenye maeneo ambayo hujayawekeza wewe mwenyewe.........Hivi kuna uwekezaji wowote wa kuyarusu magari yapakiwe hapo kwenye fukwe tajwa?

  it is time citizenry rises against this arch-typical tyranny.......................
   
 3. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Ushuru wa parking ulitakiwa usimamiwe na serikali za mtaa/wilaya.ili faida za mapato yake yatumike localy,sasa huu ni uzushi,wanataka tuwe tunaenda beach na miguu,no sweti tutakuwa tunapaki mitaa ya pembeni then tunakuja kwa tz 11
   
Loading...