Kifo cha mzazi wako wa kiume kinavyoweza kupandisha au kushusha hatma yako ya maisha wewe mtoto wa kiume

Walker Water

JF-Expert Member
Aug 23, 2022
785
2,953
Kwanza nianze kwa kusema kuwa "baba" ndiyo cheo cha juu sana katika familia.Cheo hiki kinaweza kurithiwa na mtoto wa kiume (halali wa baba) kabla baba yake hajafariki,lakini kamwe hawezi kuapishwa "kiroho" kuchukua cheo hicho mpaka pale baba yake anapofariki.

Ninachotaka kusema ni kuwa, mtoto wa kiume kuwa makini sana pale baba yako mzazi anapofariki. Baba yako mzazi anapofariki anaachia nafasi ya roho zilizokuwa ndani yake kwenda kwa mtoto mmojawapo wa kiume "kama anao wengi".

Roho hizo zinaweza kukushusha kabisa na kupoteza hatma ya maisha yako au kukupandisha viwango vya juu sana katika hatma ya maisha yako,hii hutegemea roho zilizokujia.

Katika familia kama baba anawatoto wengi wa kiume "wakwake kwa damu",roho hizo humjia kwa nguvu zaidi mmojawapo na huyo huwa ndiye mbeba nembo ya kizazi cha familia kinachofuata.

Wengine hujiwa na roho ndogondogo tu ila zina madhara kidogo au faida kidogo.Huyu mbeba nembo huchaguliwa na baba mwenyewe kabla hajafaiki au kama hakufanya hivyo,roho hizo huchagua zenyewe japokuwa mtoto wa kwanza hupewa kipaumbele zaidi.

Sasa inapotokea katika familia mojawapo kuna mtoto wa kiume ambaye si wa halali wa baba wa familia (mama yake alizaa na baba mwingine), ikitokea baba mzazi wa mtoto huyo akafariki bila hata yeye mtoto na baba yake mlezi kujua na ukute yeye ndiye mbeba nembo ya kizazi cha familia, hizo roho zitamjia bila kujua na usiombe uone vurugu zake atakazoleta katika familia!.

Ghafla utaona anaanza kumdharau baba yake mlezi au kupata hekima na bushara kumzidi baba yake mlezi na kupambana nae mara kwa mara maana naye tayari atakuwa baba rasmi tena kwa kiapo juu.

Mwisho,kwa mwanaume "baba" ambaye amefariki bila mtoto wa kiume anapoteza uridhi mkubwa sana na urithi huo unaweza kwenda kwa mkwe mmojawapo wa binti zake kama anao.(Urithi wake anautwaa mtu mwingine).

Kama amefariki bila mtoto hata mmoja ndiyo habari yake imeisha hiyo,hii hutokea sana kwa watu waliofanya maovu mengi na yakutisha sana.
 
Nini ujumbe wako hasa? Kwamba ulitaka kusema nini?
Ujumbe wangu haswa ni watoto wa kiume kuwa makini pale kinapotokea kifo cha baba yake na kujichunguza ili kujua ni roho gani zimemjia,kama nzuri aendelee nazo na kama ni mbaya azikatae.

Pili,kuwa makini na watoto wa kiume watakao wabadilikia baba zao ghafla na kujua huenda si wa hapo na kuepusha migogoro ya familia isiyo na ulazima.
 
Ujumbe wangu haswa ni watoto wa kiume kuwa makini pale kinapotokea kifo cha baba yake na kujichunguza ili kujua ni roho gani zimemjia,kama nzuri aendelee nazo na kama ni mbaya azikatae.Pili,kuwa makini na watoto wa kiume watakao wabadilikia baba zao ghafla na kujua huenda si wa hapo na kuepusha migogoro ya familia isiyo na ulazima.
Atazijuaje
 
Back
Top Bottom