Ushuhuda wa namna nilivyopungua uzito

Ushuhuda wa namna nilivyopungua uzito

whang

Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
80
Reaction score
68
Habari wakuu.

Niende moja kwa moja kwenye mada. mimi nilikuwa muhanga wa uzito mkubwa nilikuwa na kilo 87 na urefu 161cm na sasa nina kilo 77.5, hata BMI ilikuwa inasoma obesity
yaani (34).

Kilichonifanya nije kuandika huu uzi ni kuwaambia siri niliyotumia mpaka nikapungua. Aisee asikudanganye mtu kupungua ni rahisi sana kama ukiwa na nia ya dhati, usije kudanganywa na madawa ya kununua yana madhara sana kimwili.

Nini nilichofanya mpaka nikapungu? ilikuwa tarehe 15 march ndio nilianza safari ya kupungua mpaka tarehe hii 14 april ndo namaliza safari yangu ya kumaliza mwezi kuhusu uzito,kwa kupungua kilo 9.5 tu.

Intermittent fasting (kufunga), hii ndo njia pekee ya kupungua yaani ukishindwa zote basi fanya hii hutojutia. zipo njia mbili za kufunga yaani 1) kufunga masaa 16 kula masaa 8 2) kufunga masaa 20 kula masaa 4. Mimi nilikuwa nafunga masaa 16 na kula masaa 8. Mfano nilianza kula saa 6 mchana hadi mwisho saa 1:59 jioni tu.baada ya hapo sili hadi kesho saa 6 mchana bali nakunywa maji tu tena mengi.

Iko hivi kipindi nilivokuwa nafunga nilikuwa nakula vyakula vya aina vyote sichagui hadi chipsi kwahiyo usidanganywe na mtu eti uchague chakula. Ila tu kula kwa kiasi sio mpaka tumbo lihisi limebeba kitu hiyo ndo mbaya.pia wakati wa kufungua unatakiwa ufungue na chakula laini na sio kigumu yaani hiyo saa 6 unavyoanza kula unatakiwa kabla hujala wanga anza kula matunda au protein nyingi na mboga za majani.ndipo uanze kula wanga.

Pia kwenye kufunga kunywa maji mengi usiwe mvivu wa kunywa maji ndipo utapungua vizuri.Pia ukitaka kupungua vizuri amka asubuhi fanya mazoezi ya aerobics kama kutembea km 2 au unaweza kukimbia pia lakini kama huwezi mazoezi sio lazima. Nimepumzika kwa kipindi hiki bado nitaendelea nayo siku zijazo.

NB: hii sio diet bali ni kufunga kama wenzetu waislamu wanavyofunga na hii intermittent fasting imefanyiwa utafiti huko Marekani na imekubalika.
Nawasilisha.

Tujikinge na corona.

Sir dreamcheaser
 
nitajaribu hiyo,sasa hivi nimepunguza kiasi cha chakula na ninakula mara mbili tu kwa siku,asubuhi na mchana
 
Kupungua kwa mfungo bado unasafari ndefu

.mm nilitoka 95 to 72 huu mwaka na nusu nimeweza kumantain uzto wangu

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
 
Mimi binafsi ni mkongwe kwenye mazoezi kwa wale ambao sio wazoefu kwa mazoezi Kula asubuhi na mchana ,mimi mpaka sasa pamoja na wenzangu tunaamua sasa tuongeze uzito na sasa tupunguze uzito kimsingi sio uchawi NIDHAMU ya ulaji na mazoezi hivyo usifanye mazoezi kwa kuiga ooh jirani ohh sijui mjomba,fanya wewe kama wewe ,ila ukiwa fit rahaa sana
 
Mimi binafsi ni mkongwe kwenye mazoezi kwa wale ambao sio wazoefu kwa mazoezi Kula asubuhi na mchana ,mimi mpaka sasa pamoja na wenzangu tunaamua sasa tuongeze uzito na sasa tupunguze uzito kimsingi sio uchawi NIDHAMU ya ulaji na mazoezi hivyo usifanye mazoezi kwa kuiga ooh jirani ohh sijui mjomba,fanya wewe kama wewe ,ila ukiwa fit rahaa sana
Hiyo nayo nzuri mkuu

Sir dreamcheaser
 
Formula ya dr.boaz mkumbo

Yani jinsi ulivyojipunguza ww siku ukagusa tu wali ,ugali bahati huna

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
Mkuu dawa ni kula pale unapohisi njaa

Sir dreamcheaser
 
Nataka nifike kilo sabini kumbe wengine mnataka kuzishusha chini ya sabini!! Wakati Mimi nakomea 69.0 halafu mtu ana 72 anataka ashuke😂😂
Kweli hatufanani
 
Nataka nifike kilo sabini kumbe wengine mnataka kuzishusha chini ya sabini!! Wakati Mimi nakomea 69.0 halafu mtu ana 72 anataka ashuke[emoji23][emoji23]
Kweli hatufanani
Mkuu unene haupendezi asikwambie mtu na corona hii ikikupata kama mtu mnene hatari sana.ila wengine tunatamani tuwe wakawaida.

Sir dreamcheaser
 
Kula asubuhi ,mchana na jioni ,kwenye safari zako zote panda bodaboda [emoji16]
[emoji3][emoji3]na asije akajaribu kufanya mazoezi yaani arelax tu asiwe mtu wa mawazo.

Sir dreamcheaser
 
Safi Kabisa. Njia nzuri sana, unaishi maisha yako ya kawaida, unarekebisha idadi ya milo na ujazo wa chakula, ukiongeza na mazoezi kidogo, hapo utapungua bila shida na bila ya kuhofu kuongezeka uzito.

Mambo ya diet maalumu ya kupunguzuza uzito utasikia J'3 supu ya kuku na kiazi 1, J4 mtindi na mbogamboga, J5 matunda na samaki wa kuchemsha - huo niuongo sababu unaishi maisha ya kuigiza ambayo yana mwisho na utarudi kulekule kwenye kufakamia miugali na ubwabwa.
 
Back
Top Bottom