USHUHUDA: Vifurushi vya Internet vya Airtel ndiyo vya ukweli.Wengine wezi tu

USHUHUDA: Vifurushi vya Internet vya Airtel ndiyo vya ukweli.Wengine wezi tu

Airtel wako vizuri sana vifurushi vyao hasa vya internet.

MB hazipukutiki haraka kama walivyo wezi Vodacom na Tigo.Huku ni moto mbaya.

Airtel laini ya chuo ukiweka TZS 6'000 kwa mwezi inatosha sana. Unaenjoy sana.


Ni kweli kabisa mkuu yani airtel ni mtandao bora kuliko mitandao mingine yote
 
Kuna vocha za chuo pia 600 unapata gb1.2 hata mikoani tunatuma
 
Airtel hata bure na kifurushi cha milioni 10 sichukui.

Siku nilikua na update OS toka android 6 kwenda 7, only 1GB airtel ilimaziza masaa 5 hata MB 100 haijafika na niko hapa mjini, sina hama nao.

Nilipoweka Voda 4G haikuchukua hata dakika 5.

Kuna mitandao ya sim hata bure situmii, jaza ujazwe na airtel.

Binafsi sijawahi kuona mtandao wenye internet ya kasi kama Vidacom, Halotel pia sio mbaya sana.
 
Hawa wanatangaza bundle lao la buku unapewa GB 1 siku mbili lakini waaapi wamebakisha 2000 GB 2.5 kwa siku 1
 
mb hazitembei fasta kwa kuwa kwanza hawana 4g sehemu kibao,sasa mtandao kama tigo ukiwasha 4g ukadhani mb zitaenda kidogo utakuwa unajidanganya
Mkuu hii imenitokea kwenye vifurushi vya Halotel vinatembea fasta sana nikawa nasema hawa jamaa wananiibia, kumbe sababu net iko fasta na kifurushi kinaisha fastaaaa
 
Airtel wabovu kwenye huduma za pesa hiyo Airtel Money ni dolo sana yaani ukikosea kutuma pesa tu imekula kwako hakuna kuongea na mhudumu sa ndo nini. Voda kwenye M-Pesa ndo nawapendaga ( in Mobeto's hub voice)
 
Bila 4G huniambii kitu wala kunishawishi. Hivi ni kwanini Airtel hawataki kwenda 4G? Mizengwe au..??
 
Back
Top Bottom