Ushuhuda: MUNGU bado anatenda miujiza,asante MUNGU

don xxx

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
1,111
1,018
Wakuu salaam,

Napenda kutumia fursa hii kumtukuza Mungu na pia kushare nanyi furaha niliyonayo moyoni mwangu kwa kuwa Mungu amenitendea mambo makuu sana.

Ndugu zangu, katika maisha ya ujana vijana wengi tumekuwa tukiishi katika maisha ya starehe na anasa hasa uasherati.Mimi ni mmoja kati ya kundi hilo.

Miaka mitatu iliyopita nilikutana na binti mmoja mrembo udenda ukanitoka nikaishia kumtongoza ,akakubali.

Baada ya kukwichi kwichi naye mara kadhaa binti akanasa ujauzito.

Baada ya miezi 9 mtoto akazaliwa kuangalia kadi ya kriniki nakutana na sehemu inayoonesha tarehe mama wa mtoto alipoanza kutumia ARV.Kwa kweli nilichanganyikiwa sana kusoma neno ARV kwenye kadi ya mwanangu kwani nilijua wazi binti yule atakuwa anaishi na virusi vya ukimwi na atakuwa ameniambukiza.

Kumuuliza kama kweli anaishi na virusi vya ukimwi akaniambia ni kweli na anatumia ARV. (Lakini namshukuru MUNGU binti yangu hajaambukizwa VVU).

Baada ya hapo nimekuwa nikiishi maisha ya kukata tamaa kwa kudhani kuwa nami nitakuwa nimeambukizwa virusi vya ukimwi bila hata kupima kwa kuwa nimekwichi kwichi mara nyingi na huyo mzazi mwenzangu.

Kutokana na taarifa hizo; nikawa ninaishi kwa stress sana,kazini ufanisi wa kazi ukawa unashuka siku hadi siku ,kuna wakati nikawa siendi kazini natoa visingizio tu.Mbaya zaidi nikadevelope tabia ya kunywa pombe kupita kiasi suala lililonipunguzia umakini kwa wanawake.Mara kadhaa nimejikuta nikikwichi kwichi kavukavu na wanawake ambao nina uhakika wanaishi na VVU zaidi ya wawili na zaidi ya mara moja kwa kujua nimeathirika.

Juzi nimekwenda kupima nikaambiwa sijaambukizwa virusi vya ukimwi.Sikuamini masikio yangu kwa taarifa za vipimo

Wakuu, hili lililonitokea mimi ninaliona ni MUUJIZA na ninaamini MUNGU kanipa the second chance. Hivyo, sina budi kumshukuru MUNGU kwa wema wake na pia nishare na nyie mambo niliyojifunza kwenye kadhia hii:-

1.Tumia condom

2.Tumia condom

3.Tumia condom

4. Msianze kukwichi kwichi mbichi na mwenza wako kabla ya kupima.

5. Sio kila ukigundua umekwichi kwichi na muathirika wa VVU ujihesabu ameathirika. Pima kwanza vinginevyo utaishia kuwa frustrated, utakuwa kitombi hadi kuambukizwa VVU au hata kupoteza mwelekeo wa maisha.

6.Ukigundua umeambukizwa VVU usikate tamaa.Muombe sana MUNGU akupe uimara pia zingatia ushauri wa wataalam.Mzazi mwenzangu anaishi na VVU zaidi ya miaka 8 na ukimtazama huwezi hata kumhisia, ana furaha wakati wote.Wataalamu wanasema anayeishi na VVU anaweza kuishi zaidi ya miaka 30 akifuata taratibu bora za afya.

7.Fanya ufanyayo lakini omba sana MUNGU. Hayo yote niliyoyaorodhesha hapo juu hayana maana wala msaada kama huombi ulinzi na neema za MUNGU.MUNGU pekee ndie amezihuisha ndoto zangu tena.

ZABURI 107:1-2
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele! Semeni hivyo, enyi mliokombolewa na Mwenyezi-Mungu, watu ambao aliwaokoa katika taabu.
 
Urudi kwa Mara ya pili baada ya miezi mitatu ukahakiki afya yako. Then baada ya miezi sita malizia vipimo kwa mara ya tatu. Ukimaliza njoo JF haraka utoe ushuhuda tena. Hapo bado upo kwenye kipindi cha matazamio. Asante
 
Story nzuri sana. Ila sijaona miujiza hapo. Una uhakika asilimia ngapi kama huyo mtoto ni wako? Ulishamuuliza huo ugonjwa aliupatia wapi,kabla ya kuwa na wewe au baada?
 
Urudi kwa Mara ya pili baada ya miezi mitatu ukahakiki afya yako. Then baada ya miezi sita malizia vipimo kwa mara ya tatu. Ukimaliza njoo JF haraka utoe ushuhuda tena. Hapo bado upo kwenye kipindi cha matazamio. Asante
Window period haipo hapo. Amekwichi hadi mtoto. Viral load ya mama ilikiwa chini sana kiasi kwamba hakuambukizwa. Baba imba mapamnio ya sifa na kuabudu hadi sauti ikauke. Bwana apewe sifa sana.
 
mungu ni mwema ila adui ulikuwa wewe mwenyew na uhuni wako
siku zote mnaambiwaga wanawake hawakomolewi umalaya ndo unawaponza kila sketi mnataka kuivua aya
 
Back
Top Bottom