Ushuhuda: Mchemsho niliokunywa, haikupita nusu saa nikawa fresh mpaka nikawa naona furaha ya kupumua

Fafanua hoja yako usijifiche, wataalamu wote wanajua si rahisi kupata dawa ya magonjwa yanayosababishwa na virus, hivyo wanasisitiza kutumia vyakula vinavyoongeza kinga ya mwili

wewe mtaalamu wa JF em tuelezee ni dawa ipi ina uwezo wa kupambana na virus?
Hutakiwi kusubiri corona ili ule balanced diet! Hili ni suala lilipo tangu zamani na kwa sababu ya maradhi yote na siyo corona pekee. Usipokula vyakula vyenye kusaidia kuongeza kinga basi magonjwa mbalimbali yatakuandama. Tatizo lenu mnapiga tarambeta kuwa hivyo vyakula ni ''dawa ya corona''.
 
Hawa wote ni wafuasi wa mjinga mmoja wanajaribu kukebehi watu. Watu wanakufa wao wanasema ni hofu. Watu wanakufa wao wanatudanganya tujifukize na madawa ya ujinga ambayo yanasababisha mapafu kuathirika zaidi. Kwendeni zenu
Wenye hofu ni wao halafu wanasingizia wananchi kuwa na hofu...
 
Mimi ni tofauti kidogo, japo hali yangu ya kiafya ilikuwa kama yako.

Nilichemsha mwarobaini nikachanganya na tangawizi iliyosagwa, baada ya muda mfupi nikanywa aiseee mwarobaini ni hatari imefika jioni nipo good kabisa

Naiman covid19 nimeitokomeza amebaki huyu covid21(uchumi wa kati)
 
Mkuu yaani hayo maelezo yako ni exactly what happened to me Disemba mwaka jana na Februari this year. Mimi kwanza niliji isolate halafu kujifukiza na hiyo mixture ya malimau...
Mwanzo sikuamini nilikuwa mbishi kama jamaa zangu humu ndani lakini nilipokuja kutumia huu mchanganyiko ndio nilipata majibu.

Nashauri watu wasiwe wabishi sana wawe wanajaribu kwanza kabla ya kukosoa
 
Hutakiwi kusubiri corona ili ule balanced diet! Hili ni suala lilipo tangu zamani na kwa sababu ya maradhi yote na siyo corona pekee. Usipokula vyakula vyenye kusaidia kuongeza kinga basi magonjwa mbalimbali yatakuandama. Tatizo lenu mnapiga tarambeta kuwa hivyo vyakula ni ''dawa ya corona''.
Mkuu kama mtu ameitumia na ikamsaidia tunaiitaje?

Hizo dawa za hospitali unazoziamini zina guarantee ya kutibu na kuponyesha? Namaanisha mtu akimeza mseto ni lazima apone malaria?
 
mi ni tofauti kidogo,japo hali yangu ya kiafya ilikuw kama yako.

nilichemsha mwarobaini nikachanganya na tangawiiz iliyosagwa.baada ya muda mfupi nikanywa aiseee mwarobaini ni hatari imefika jion nipo good kabsa

naiman covid19 nimeitokomeza amebaki huyu covid21(uchumi wa kati)
Ni wakati sasa wa kuziamini dawa zetu ambazo mababu zetu wamekuwa wakizitumia miaka na miaka
 
Kwahiyo dawa gani ni sahihi?
Wabongo tuna tatizo la kuwa wavivu kusoma na kufuatilia habari za maana. Mpaka sasa corona haina dawa ya kutibu! Ina dawa za kusaidia mtu ku-recover lakini siyo kutibu. ndiyo maana umekuwa ugonjwa unaotesa dunia yote na sehemu nyingine watu kujifungia.
 
Kama unalitambua hilo kwanini unawashangaa wanaotumia malimao Kulicover?
 
Ndugu yangu mmoja yuko kagera, mmewe amefariki kwa ugonjwa huu. Baada ya mazishi yeye na wanae wakaanza ugua sana. Anadai kilichomsaidia ni huo mchanganyiko lakini ulcers zimemsalia baada ya kutumia.
 
Mkuu kama mtu ameitumia na ikamsaidia tunaiitaje?

Hizo dawa za hospital unazoziamini zina guarantee ya kutibu na kuponyesha? namaanisha mtu akimeza mseto ni lazima apone malaria?
Kwa kifupi ni hivi. Watu wengi wanaogua corona hawafi. Kwenye hili kundi ambalo watu hawafi kuna ambao wanakuwa hawana dalili kabisa, kuna wenye dalili kidogo na wanapona na kuna wenye dalili kali na wanapona. Tuchukuwe kwa mfano kuna watu elfu moja wamepata corona watu mia tisa na tisini na tano wakaangukia kwenye kundi nililoeleza na watano wakafa. Tuseme tena kuwa hawa watu elfu moja nilioelezea walikuwa wameshauriwa na rais wao wajifukize wakiona wana dalili za corona na wote kweli walijifukiza. Hapa ina maana wale mia tisa na tisini na tano waliojifukiza watadhani dawa waliyojifukiza nayo ndiyo imewafanya wakapona. Je, itakuwa kweli ni ile dawa imewaponyesha? Madaktari na watafiti wamejaribu kuunganisha uhusiano wa kujifukiza na kuua virus ambaye ameingia kwenye cell za mwili wako wakaona hakuna uhusiano. Wewe mpaka ukaue virus kwa mvuke wenye joto hizo cells za mwili wako zitakuwa salama? Kufukiza kunaweza kusaidia labda kama wale virus wamekuletea mafua hivyo ule mvuke ukasaidia njia ya hewa kufunguka, kama watu wanavyofanya kwenye mafua ya kawaida. Sasa hapa uwe makini: Usidanganye watu kuwa kujifukiza kumemaliza corona.
 
Kama unalitambua hilo kwanini unawashangaa wanaotumia malimao Kulicover?
Kwa sababu ni uposhaji. Mpaka sasa kuna dawa zinazojulika zinasaidia ku-recover lakini malimao siyo moja na wanasanyansi wameshasema hayasaidii kwa namna yanavyotumika. Huku kwentu tunambiwa tusijali chochote kuhusu corona bali tujifukize na kula tangawizi na malimao. Huoni ni uposhaji huo?
 
  • Dislike
Reactions: len

ndio maana kule juu nilikuuliza hoja yako ni ipi, nilitaka unielezee mtu akiugua corona afanye nini,

Je anatakiwa akae tu atapona mwenyewe?

au unashauri nini mkuu?

nataka nijue unajua kitu gani kinaweza kua msaada kwa watanzania wenzako na dunia kwa ujumla wake.
 
Kwa sababu ni uposhaji. Mpaka sasa kuna dawa zinazojulika zinasaidia ku-recover lakini malimao siyo moja na wanasanyansi wameshasema hayasaidii kwa namna yanavyotumika. Huku kwentu tunambiwa tusijali chochote kuhusu corona bali tujifukize na kula tangawizi na malimao. Huoni ni uposhaji huo?
Hiyo dawa inayosaidia kulicover imetengenezwa nchi gani mkuu? na imeisaidia vipi hiyo nchi kupunguza vifo vitokanavyo na hawa virus?

Tashukuru ukileta takwimu za vifo vya kabla ya dawa na baada ya dawa
 
Binafsi nimeshuhudia watu kadhaa waliopona baada ya kutumia mchanganyiko huu na kujifukiza. Kuna jamaa yangu mmoja hali yake ilishakuwa tete sana, hata alikuwa anapumua kwa taabu sana. Tulipopata taarifa tu tukamshauri mkewe amtengenezee huu mchanganyiko. Hali yake ilibadilika sana baada ya kuanza kutumia na sasa ni mzima kabisa.
Hapa mtaani kuna jirani yangu naye ilimpata, yeye naye alikuwa mbishi kutumia mchanganyiko huu, akitumaini zaidi dawa alizopewa hospitalini. Lakini hali yake ikazidi kuwa mbaya mno. Hapo akawa hana namna ila kukubali kujaribu kuutumia. Sasa hivi na yeye anaendelea vizuri sana.
Nilichojifunza ni kwamba, bado Watanzania wengi ni wagumu mno wa kuelewa na ni wabishi mno. Suala la kujifukiza haliko tu Tanzania, tumeona katika mataifa watu wanajifukiza na wanasaidika, lakini bado kuna watu kwa chuki zao na serikali wanabisha.
Hebu sasa tuambieni nyie mnaobisha, ufumbuzi wa janga hili nini?
Ni kujifungia ndani? Huko walikojifungia corona haiwasumbui?
Tutajifungia mpaka lini?
Halafu tukifungia tutakula nini?
Leteni majibu ya maana na sio matusi
Matusi yanaonyesha tu namna gani mtu ni mweupe kichwani
 
Back
Top Bottom