Ushuhuda: Mchemsho niliokunywa, haikupita nusu saa nikawa fresh mpaka nikawa naona furaha ya kupumua

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,615
32,719
Habari watanzania na wanaafrika mashariki kwa ujumla.

Nimeona tushare namna mbalimbali tulivyopambana na hii nimonia inayobadilikabadilika kwa lengo la kushtuana ili wengine nao wajifunze.

Naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi, lakini shuhuda za wengine ni muhimu pia. Huu ugonjwa nilianza kuusikia sana mwezi ule wa 3 mwaka jana lakini sikutilia maanani mpaka tuliposimamishwa kazi kwa wachina kwenye kampuni ya ujenzi kwa sababu ya hili gonjwa ndipo nikaanza kuwa na hofu, ukizingatia kipindi hicho watu wengi walizingatia mwongozo uliotolewa wa kila mtu kuchukua hatua ya kutumia vitakasa mikono pamoja na kuvaa barakoa.

Tulisimamishwa kazi nikakaa nyumbani na familia mpaka mwezi wa 5 ndipo mwanangu akaanza kuugua kikohozi kikavu kiasi kwamba alikohoa mpaka akawa amedhoofu... Nilimpeleka hospitali akaonekana hana ugonjwa wowote ikabidi apewe dawa za kikohozi tu ambazo zilimsaidia akapona.

Wakati mwanangu anatumia dawa kikanishika mimi na mke wangu pia lakini hatukwenda hospital bali tulipona bila kutumia dawa.
Hivyo awamu ya kwanza ikapita ambapo iliambatana na kuumwa kichwa, kukohoa kusiko na mafua, kupoteza ladha na harufu.

Awamu ya pili ilinikuta mwenyewe maana mke na mtoto walisafiri. Awamu hii ilikuwa mwezi wa 11 mwanzoni ambapo yalianza mafua ya ghafla mara kesho yake nikaamka nipo hovyo, joto la mwili limepanda na kichwa kikawa kinauma. Nilivunga tu nikaona nitapona maana nina kawaida siendi hospital mpaka nizidiwe... Siku ya pili nikawa nimezidiwa zaidi alafu nikawa naumwa kila mahali alafu maeneo ya kiunoni kukawa kumekufa ganzi, miguu ikawa inauma hatari na kichwa kikawa kinauma, koo likawa limevimba alafu kavu kinoma huku naharisha!

Hofu ikatanda nikawa nakula malimao na pombe kali nikawa nawaza kesho lazima niwahi hospital. Kesho yake nilizidiwa zaidi nikawahi hospitali asubuhi nikamweleza doctor hali yangu, akashtuka akakaa mbali kidogo tukawa tunahojiana mwisho akaniambia nikafanye vipimo chumba cha pili.

Nilichukuliwa vipimo vya damu, mkojo, kinywani niliangaliwa kukaonekana kuna dalili ya vidonda alafu kumevimba, nikapimwa kifua lakini majibu yakaonesha nina typhoid tu.

Niliandikiwa dawa nyinginyingi ambazo sikuzielewa bahati mbaya nikawa sina hela ya kutosha maana hela niliyokuwa nayo iliishia kwenye vipimo nikabaki na buku tano tu, ila nilipotaka kuondoka bila dawa daktari akaniuliza una Tsh ngapi nikamjibu nina Tsh 5,000, akanipa azuma kipaketi kimoja akanitaka niendelee kutumia alafu nikanunue dawa ningine zilizobaki.

Nilipofika home nikameza kwa utaratibu wa daktari kesho yake nikaamka vizuri kabisa nikawa nimebaki na mafua tu... Nikaendelea na ile azuma bila kununua dawa nilizoelekezwa mpaka nikapona kabisa na haikuchukua hata wiki.

Awamu ya tatu ndio hii iliyonishika juzi kati hapa mwanzo wa mwezi huu wa pili! Hii ilianza na mafua tena lakini ni kali kuliko zote maana nilifika hatua mpaka kupumua ikawa napumua kwa shida. Yalianza mafua mchana, usiku nikawa na dalili za malaria, asubuhi ya saa kumi na moja nikawa napata tabu hadi nikawa napumua kwa mdomo pamoja na pua/yaani ilibidi nilale chali alafu nikaacha mdomo wazi maana niliona pua hazitoshi!

Pamoja na kuacha mdomo wazi bado pumzi zilikuwa hazitoshi alafu nikawa nikipumua nasikia kifua kinakoroma kwa ndani.
Nikawasha marijuana nikavuta lakini wapi... Kutokana na tanzia nilizokuwa nazisoma humu Jamiiforums, moja kwa moja nikawaza hii ni zamu yangu!

Kadri nilivyokuwa nawaza itakuwaje ndivyo hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya maana mpaka kufika saa kumi na mbili asubuhi nilikuwa nikipumua nasikia kifua kinapiga mluzi kabisa.

Nikaamka nikakaa huku mwili wote ni mzito kama jabali.
Wakati nawaza nikakumbuka kuna habari niliisoma humu sikumbuki aliileta nani, ambapo ilikuwa inaongelea ule mchanganyiko wa NIMR.

Kwa kuwa kazi yangu nauza matunda na viungo mbalimbali/genge la matunda), niliamka muda huohuo nikawahi kibandani nikakusanya matirio ambapo ni;

Malimao mawili

Kitunguu saumu kimoja kikubwa

Tangawizi yenye kitu kama g100 pamoja na kitunguu maji cha wastani chekundu.

Kitu nilichokuwa sina kibandani ni pilipili kichaa ambazo kwa mujibu wa NIMR zinatakiwa pia ziwemo.

Baada ya kuchukua vitu hivyo nikarudi magetoni nikavikwangua kwenye kikwangulio kwa kuwa sina Brenda, nikaweka maji nusu lita alafu nikakamulia humo Malimao nikachemsha.

Baada ya dakika chache nikaepua nikachuja alafu nikanywa karibia nusu ya chupa alafu nikafanya vimazoezi vidogovidogo kama kurukaruka, kurusha ngumi, kujinyooshanyoosha na baada ya hapo nikatulia.

Hamuwezi kuamini haikupita nusu saa nikawa fresh mpaka nikawa naona furaha ya kupumua.
Nilikuwa mwepesi kabisa kichwa kikapoa, mwili ukawa fresh nikawa nimebaki na mafua tu ambayo nayo yalianza kukauka kesho yake. Kumbuka huu mchemsho nilikunywa tena mchana kidogo, jioni kidogo na usiku nikamalizia.

Mpaka muda huu ninavyoandika hapa mimi ni mzima kabisa ila sijui itakaporudi itakuwa na nguvu kiasi gani.

Nilichojifunza kwenye huu ugonjwa ni kwamba una tabia ya kurudi kwa nguvu zaidi au kwa dalili za ziada.

Naomba kwa waliougua wakapona waweke shuhuda zao ili wengine wajifunze pia... Haijalishi umepona kwa dawa zipi, ziwe za hospitali au za kienyeji, wewe weka tu huwezi kujua utaokoa wangapi.

Kumbuka huu ugonjwa kila unaempata unakuwa na dalili za tofautitofauti japo kuna dalili za msingi ambazo hufanana kwa wote.
Nasema hivyo kwa sababu hapa mtaani kuna ambao nimeona wakipatwa na huu ugonjwa sauti inapotea kabisa mpaka ukiongea nao wanaongea kwa ishara tu.
 
Umeelezea vizuri sana mkuu
Ushuuhuda wangu mimi
Ni hvi karibuni nimepigwa na covid na ila ile ya mwezi wa tano mwaka jana ndo ilikuwa kiboko
Ila mara ya pili sasa hivi mpk muda huu bado sijakaa sawa ila haikuniathiri saaana kutokana na mambo mawili makuu

Kwanza Uzoefu wa kuumwa mara ya kwanza
hvyo dalili ziliponijia tena za COVID nilichukua hatua mapema za kuandaa limau na tangawizi bila kusahau MWALOBAINI kujifukiza zilihusika ila safari nikawa napiga sana peps baridi ninapokuwa na joto na homa wakati mwingne homa ikiwa kari zaidi nilikunywa MUALOVELA
na kikinijia kile kichwa cha COVID nikisema kichwa cha COVID waloumwa huu ugonjwa wananielewa mana bichwa linakuwa km sio lako macho km yanataka kung'oka bichwa zito km umevaa helmet basi nilikuwa najipumzusha sehemu yenye hewa nzuri yaan kutwa nzima nakuwa natamani kulala tu

Na jambo la pili lililonisaidia mpk haikunichukua sana ni HOFU kwakweli awamu ya kwanza nilikuwa na hofu sana iliyokuwa inapelekea mpk presha inapanda ikawa inanisababishia matatizo sana ktk upumuaji
Lkn awamu hii ya pili niliweza kuishinda hofu ndio mana niliweza kukabiliana nayo changamoto ya kupumua vizuri kabisa
Nitaelezea baadae mbinu gani niliyokuwa natumia kupambana na changamoto ya upumuaji naamini itawasaidia wengi
 
Hawa wote ni wafuasi wa mjinga mmoja wanajaribu kukebehi watu. Watu wanakufa wao wanasema ni hofu. Watu wanakufa wao wanatudanganya tujifukize na madawa ya ujinga ambayo yanasababisha mapafu kuathirika zaidi. Kwendeni zenu
Acha upumbavu!
Ingekuwa wanaathirika zaidi basi mimi ningekufa.

Sio ajabu umeugua hizihizi dawa zikakuponya
 
Umeelezea vizuri sana mkuu
Ushuuhuda wangu mimi
Ni hvi karibuni nimepigwa na covid na ila ile ya mwezi wa tano mwaka jana ndo ilikuwa kiboko
Ila mara ya pili sasa hivi mpk muda huu bado sijakaa sawa ila haikuniathiri saaana kutokana na mambo mawili makuu

Kwanza Uzoefu wa kuumwa mara ya kwanza
hvyo dalili ziliponijia tena za COVID nilichukua hatua mapema za kuandaa limau na tangawizi bila kusahau MWALOBAINI kujifukiza zilihusika ila safari nikawa napiga sana peps baridi ninapokuwa na joto na homa wakati mwingne homa ikiwa kari zaidi nilikunywa MUALOVELA na kikinijia kile kichwa cha COVID nikisema kichwa cha COVID waloumwa huu ugonjwa wananielewa mana bichwa linakuwa km sio lako macho km yanataka kung'oka bichwa zito km umevaa helmet basi nilikuwa najipumzusha sehemu yenye hewa nzuri

Na jambo la pili lililonisaidia mpk haikunichukua sana ni HOFU kwakweli awamu ya kwanza nilikuwa na hofu sana iliyokuwa inapelekea mpk presha inapanda ikawa inanisababishia matatizo sana ktk upumuaji
Lkn awamu hii ya pili niliweza kuishinda hofu ndio mana niliweza kukabiliana nayo changamoto ya kupumua vizuri kabisa
Nitaelezea baadae mbinu gani niliyokuwa natumia kupambana na changamoto ya upumuaji naamini itawasaidia wengi
Apo kwenye bichwa la covid nimecheka mpk. Yaani mpk unajiuliza utapona kweli..... macho hata mwanga hayataki...
 
Back
Top Bottom