USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Hi stori ina walakini sana. Ni stori ya kusadikika zaidi.
Sasa hivi Hizi kampuni hazileti meli za mafuta.
Utaratibu unaotumika ni kuwa kila quarter kuna bulk importer mmoja ambaye analeta mafuta. Sio oil com wala world oil au babake yoyote anae agiza mafuta kutoka nje.
Utaratibu uliopo ni kuwa bulk impoerter analeta mafuta na yanashushwa yote kwenye deport ya tipper.
Huyu anaye shunda tenda ndie anaelipa ushuru kwa mafuta yote ysnayo ingia.
Na tangu utaratibu huu kutumika hakuna local company ilo shinda tenda hii..
Makampuni ya ndani yananua mafuta kutoka muagizaji mafuta ambayo yameshalipiwa ushuru wa kuingiza wao hawahusiki na hizo taratibu za kubadilisha Jet na diesel.
Utaratibu huu ndio ulowezesha EWURA kuweza kuweka bei ya mafuta kwa mlaji kwa sababu wote hawa wananunua bei ile ile kutoka kwa bulk importer...serikali inachukua chake yakkingia tu.
Hivyo ni uongo wa mchana kusema kuna meli imeagizwa na oil com au babako nani...
Hizi ni chuki kwa warabu kwa sababu ndio umetanguliza hayo.
Na world wenyewe ni wwswahili walo amka wachapa kazi.
Mafuta yanayo enda nje ya nchi huagizwa na nchi husika na makampuni ya hapa hushughulika na usafirishaji tu.
Hivyo stori sijui alikua ashushe meli diesel lakini imeandikwa jet 1 ni yauongo.

Kama kuna ulaji katika mita basi mchezo anacheza bulk importer ..usiootoshe watu kwa sababu za chuki binafsi

Inaonekana umechukia sana... WHHHHYYYYY....KWANINIIII???? au nawee ni jipu? hhahaha natania mkuu
 
Hatari, hii nchi inatafunwa kila upande.
God bless Tanzania, Amen!
 
Inaonekana umechukia sana... WHHHHYYYYY....KWANINIIII???? au nawee ni jipu? hhahaha natania mkuu
Sijachukia ..ila sipendi wivu...watu wengine wana wivu na wenzao ambao wamefika
na wapo wana chuki za biashara na wengine wana chuki za udini hivyo nachukulia kila taarifa za aina za kuchochea dhidi ya auna fulani kwa tahadhari.
Kuna wakati tulikua na matatizo ya uchakachuaji...na Ewura wakafanya kazi ya kupitia vituo vungi na hapa dar vingi vilifungiwa na tatizo hili halikua la oil com wala camel oil..wao walikua wakupiga vita sana kwa kulikua na wakati kule rwanda wakiyakataa haya mafuta..sasa ikawa usumbufu..wafanya biashara wakaibana serikali kuweka ushuru zaid kwenye mafuta ya taa ambayo ndio yalio kuwa yakitumika uchakachuaji. Serikali ikawa unagoma mpaka Rwanda ilipowakamata madereva zaidi ya 30 kwa kosa la kuingiza mafuta machafu ndo ikakubali kuweka bei ya kerosene karibu sawa na disel.
Lakini kuniuliza nani alikua behind uchakachuaji ule ? Ukweli ni polisi na madereva wa tankers na wafanya biashara mijizi ya mkoa wa morogoro ambao wengine umijikita kwenye ccm na bunge hawa ndo kinara.
Gari inatoka dar feshy ikifuka maeneo kunazia kongowe mpaka visiga askari wanakuwepo tayari wana i wave gari kuingia pembeni kituo cha petrol wanafanya yao na dereva amakatiwa chake.
Hapa wasafiri shaji ndio wanao pigwa bao na mtandao huu ni mkubwa sana hawakuweza kuupiga vita.
Hivyo matatizo yapo ila unapo kuja na stori ambayo unaipanga kumu attack mtu zaidi badala ya ku base on issues na ushahidi wenye kueleweka...
Mtoa mada anasema haya mafuta yalikua kwa ajili ya export ..ik sawa sasa unajiuliza kwanini ahanga ike nayo haya wakati haya hayana ushuru..yeye role yake ni kuyahifadhi na kusafirisha kwa nchi husika? Hapo ndo unajua mhh hapa sio sawa kuna kitu
Pili anasema mzee gani sijui akapiga simu wale jamaa 10 wote wakaitwa na kupewa million 80 !! Ukijumlisha ni 800m . Hivo huyu jamaa akitegeshea camera ta licha yote mpaka mzigo akaujua ulikua na amont hio? Hivi ni rahisi sana kupata 800m ndani ya saa? Haya hywezi jua kama na wewe hukupata ule mgao.
Uta ona story inakosa mshiko kwa sababu hizo ...na zaidi mzigo wa export hauna ushuru hana haja ya kufanya deal la kufanya deal.
Mwandishi huyu ..amefungua uzi mwengine dhidi ya oil com
 
Do hii ni hatari.... yaani mpaka nimeogopa.... 80m
kila mmoja cash! !..... inahitaji moyo kuzikataa.... na hawa wanajua hakuna atakae kataa.... inahitajika total overhaul ya utaratibu wa mafuta hapa nchini....
Hata ningekuwa mimi hiyo Ml. 80 ningelamba.....inahitaji moyo mgumu...eee Mungu tusaidie!
 
Duh njia pekee ya kuzia haya ni serkali kubeba jukumu la kuingiza mafuta yasisafishwa/mafuta ghafi(crude oil)na serkali pekee ndo iwe na mitambo ya kusafishia.
 
Nimshukuru mleta mada, kwani ina hasi na chanya.

Niongezee kwa hoja ya AVEROES kwanza kurusha mwanga kidogo kwa uzalishaji wa hii NAPTHA. NAPTHA huzalishwa kwa wingi kutokana na usafishaji mafuta ghafi (crude oil) ambapo, crude oil hutiwa ktk kinu cha moto au joto kali inayopelekea kuzalisha mafuta na gesi tofauti ktk layers tofauti.

Layers hizi hutofautisha mafuta na gesi tofauti yaani PETROL, KEROSENE (mafuta ya taa), DIESEL, mpaka chini kabisa kunapatikana LAMI.

Hali kadhalika gesi aina tofauti kama butane, propane, nakadhalika hupatikana hapa. NI VYEMA pia nikawajuza Watanzania kuwa hii gesi ya kupikia majumbani, iitwayo Liquefid Petroleum Gas au LPG, inayosambazwa katika mitungi kama ORYX, MIHAN, CAM GAS, LAKE GAS nakadhalika hutokana na mchanganyiko wa PROPANE NA BUTANE kupata LPG. Huingizwa nchini kutoka nchi zinazozalisha mafuta na kusambazwa hapa nchini katika mitungi ya gesi ya kilo 3, 6, 15, 38, na hadi mitungi mikuuubwa ya kilo 500, 1000 nakadahlika.

Sasa tofauti za mafuta haya huja kwenye parameters tofauti kama boiling points, flammability rates, viscocity, density nakadhalika nakadhalika.

Refineries tofauti duniani huenda wakazalisha bidhaa Fulani na Fulani zaidi kulingana na mikakati yao , mfano huenda akaset kupata petro zaidi.

Ama nikirudi kwenye NAPTHA, hii imeegemea zaidi katika PETROLI na tofauti zinakuja kwenye parameters kama nilivitaja hapo juu. Nirejee kusema

Kabla sijahama kutoka uchimbaji wa mafuta ghafi (crude oil) na usafishaji wa mafuta yaani petroleum refinery, NIWAKUMBUSHE Watanzania refinery tuliyokuwa nayo ya TIPER ambayo kwa leo ni mali ya kampuni ya ORYX. Refinery hii ilitumika miaka ya nyuma kusafisha mafuta, kwa maana mafuta ghafi yaliingizwa nchini, na uzalishaji au usafishaji wa mafuta kama nilivoeleza awali ulifanyika hapa nchini. Refinery hii ilikufa kifo cha mende, ingawaje ki uchumi ilikuwa na faida.


Katika uchimbaji wa NATURAL GAS, pia hupitia process kama ya hapo juu, ila hapa huingizwa kwenye mtungi mkuuubwa kwanza wa High Pressure Separator, ambapo GAS ASILIA huchujwa, ikielea juu kwa sababu ya uwepese wake (density), na chini yake kubaki CONDENSATE. Hii condensate, hukamuliwa maji (water) na kutolewa na albaki kuingizwa tena katika Low Pressure Separator. Hali kadhalika hupatikana maji na mabaki kuwa aina tofauti za kinachofanana na mafuta ghafi. Zao hili sasa, huwekwa ktk treatment tofauti kupata kitu gani mzalishaji anataka….ambapo, pamoja na mengineyo hupatikana NAPTHA.


Hii NAPTHA sasa hupitia pia michakato tofauti kama vile kuiondolea sulfur na treatments nyinginezo zinazoweza kukupatia PETROL.

Vile vile, kutokana na NAPTHA, tunaweza pata SOLVENTS, sabuni za maji au cleaning fluids, diluents (nimekosa neon la Kiswahili hapa) za rangi, varnish, asphalt, pamoja na bidhaa kama solvents katika makampuni ya mpira (rubber) , viberiti vya gesi, hata mali ghafi katika dry cleaners na kutengeneza mbolea.


Sasa basi, Watanzania tunapotezwa sana katika propaganda kuliko kuelewa vitu, na kuchangamkia FURSA. Kuliko kumshambulia OILCOM, hapa naona fursa nyingi, nyingi, na nyingi ambazo OILCOM aliona baadhi, na sio kwa U-HASI BALI KWA U- CHANYA.

Zipo sheria za OSHA zinazosimamia athari au maelekezo ya viwango vya matumizi ya NAPTHA. Na sheria nyingine nyingi katika hili. Kwa faida yako, pia kasome kidogo kuhusu MSDS

Mwisho nimuulize ndugu yetu huyu mtoa mada, alikuwa wapi toka OILCOM anaanza biashara miaka ya tisini? Vyombo husika vyote vililala? Na je mbona hatujasikia magari ya wateja wa OILCOM yakiharibika miaka yote hiyo? Mbona hii story inakuja baada ya baadhi ya watu kukosa tenda ya kununua CONDESATE? Na baadhi ya makampuni kutumbuliwa majipu ya kodi?


Labda pia nieleze kidogo hapa. TPDC ilitengaza tenda ya kuuza CONDESATE. Wadau mbalimbali waliomba na aliyeshinda akapewa. Bahati mbaya mshindi huyu alipigwa chini baada ya muda kwa sababu siwezi zieleza hapa. Mimi sio mchafua watu bhaaana!!!!


Hivyo ndugu, ninapenda kuamini kuna motivation ya kuagizwa kupewa vijisenti kuchafuana ila tufahamu, Watanzania walio makini hawaangalii propaganda na maneno hewa, ila scientific facts, na uhalisia. Tanzania ya leo inahama kutoka enzi za kuamini udaku, fitna na wauza maneno. Ila tuwapatie WATANZANIA uchambuzi wa hoja na scientific facts.

Ahsanteni na siku njema.
 
Hizi mada ndizo zinazoleta afya ya kufikiri na kutatua matatizo ya nchi yetu
 
Hii mada mtu anatafutwa kwa udi na uvumba!! Max bana hivyohivyo tusije kutoana macho bure!!!
 
Huko Bandarini na TRA ni majipu SHUPAVU,, kila kona ni DILI tu,, kwenye magari ya mnada kule handarini Pia Kuna DILI linapigwa Kati ya Hao Bandari ,, TRA na Dalali wao.
 
MFICHUA MAOVU anatafutwa kwa udi na uvumba.

Hakika hii nchi si salama kuanzia kiuchumi, kiutamaduni , kifikra , kiuongozi na imejaa kila aina ya hila.

Walaaniwe WATAWALA kwa dhambi hizi.
 
Unalamba milioni 80 na kazini bado unadunda, huku moyoni ukimcheka 'mtukufu' kwa mbwembwe na hila zake dhidi ya wadanganyika.

SHAME Tanzania
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.

Juzi nimefungua uzi wenye kichwa cha habari, "USHUHUDA: Jinsi kampuni za mafuta zinavyokwepa ushuru" nikatoa mfano mmoja wa kampuni ya OILCOM inavyokwepa ushuru. Kuna watu wameni-inbox vitisho.

Sasa natoa mfano mwingine wa OILCOM hiyohiyo.

Baada ya gas ya songosongo kuanza kuchakatwa ( Gas processing). Kampuni ya OILCOM ilipata tender ya kununua Naptha ambayo ni byproduct ya gas processing. Hii naptha ni mojawapo ya condensate katika Natural Gas Liquids (NGL) ambazo huwa zina-liquify katika surface separator. Kwa wasioijua hii Naptha ni ile thinner inayotumika kuchanganyia rangi. Sasa hii naptha inatumika katika viwandani kutengenezea Rangi. Sasa OILCOM ndio Dealer mkubwa wa hiyo naptha pale songosongo. Huwa anapeleka meli pale songosongo na kupakia mzigo wa kutosha na kuja kuushusha kwenye depot yake pale kurasini. Kwa mkataba wake OILCOM ni kwamba anaiuza kwenye viwanda vya rangi vya hapa nchini na nyingine ana-export nje ya nchi.

Anachokifanya kwenye depot yake pale kurasini ni kui-blend na Petrol (PMS) kwa ratio nzuri na kuongeza na octane boosters ili afikie viwango vinavyohitajika vya AKI (Anti Knocking Index) na anatuuzia kwenye service station zake kama petrol.
Parameter anayoi-monitor kwenye hii petrol anayotu-blendia ni hiyo OCTANE number tu kwa sababu anajua kuwa akikosea hiyo atauwa injini za magari yote yanayotumia petrol na effect yake watu wataiona immediately wakijaza kwenye station zake.

Parameter nyingine kama oxygen content na vapour pressure hashuguliki nazo kwa kuwa effect zake zipo kwenye ulaji wa mafuta wa injini na kutoa moshi. (Effects of low and high oxygen content)
Hii petrol yenye naptha ya songosongo tumeuziwa kwa muda mrefu sana na wakuu wanajua kuanzia ewura hadi TRA. Yupo afisa mmoja wa TRA wa kitengo cha mafuta ambaye alikuwa ndio kama Resident custom officer pale oilcom anaitwa GEORGE, yeye ndio alikuwa kiunganishi wa OILCOM kwenye haya magumashi
Alafu polisi inamlazimisha mtu amtaje mtoa taarifa. Baada ya kushughulika na kashfa hiyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom