Ushuhuda: Hatimaye ametiki

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Hatimaye Ametiki(Based on true story)
IMG-20210326-WA0017~2.jpg


Ilikua mwaka 2014 katika chuo cha elimu ya biashara(CBE) Tawi la Mbeya nilikuwa mwaka wangu wa pili nikichukua stashahada ya usimamizi wa biashara (diploma in Businesses administration). Nikiwa nimeketi kwa pembeni kipindi hicho ndo kuna wanafunzi wapya walio kua wanaripoti. Nilimuona binti mmoja ambaye alikuwa akitoka Eneo la utawala kufanya usajili lilikua ingizo jipya Chuo hapo, binti huyo yeye alikuwa mzuri mwenye kufanana na mabinti wa kimasai kulingana na mkao wake, tembelea pamoja na umbo na rangi yake.

Sikufuatilia sana nilimuona na kumfananisha na maasai.
Siku kadha kupita wakiwa wanaelekea siku za mwisho za Orientation binti huyo nilimuona amekaa peke yake sehemu nikaona si vyema kumuacha nikasigea karibu yake na kuanza mazungumzo japo kidogo.

Mimi: Mambo vipi sister

Yeye: Safi (Aliitikia salamu huku akiniangalia na kuonyesha nusu tabasamu nusu kuchukia kama nimevuruga mpango wake wa kukaa peke yake yaani sikumuekewa)

Mimi: samahani kwa kukuingilia je, itakuwa dhambi kwa mimi kukaa na wewe hapa?

Yeye: Hapana

Mimi: Samahani wewe ni mwenyeji wa Arusha eti

Yeye: Ndio mimi mwenyeji wa Arusha wilaya ya Karatu.

Nilimuuliza maswali hayo sababu akifanania na maasai. Nikaanza kwa kumuuliza Jina akagoma kunitajia, Nikaona hapa niende direct kuomba mawasiliano ikabidi nimfungukie unaweza nisaidia mawasiliano yako.
Yeye alikataa katukatu na kusema hawezi nipa Mawasiliano yake nilijitahidi kumdanganya akasema labda yeye achukue namba zangu nami bila hiyana nikamupatia.

Hapo tunapiga stori kidogo nikaachana nae nikawa nimemuacha amekaa. Siku zilipita ilikuwa nadra kumuona sababu lecture rooms tulitofautiana na wala hakuwahi nitafuta kwenye simu. Siku zikaenda kama mwezi mmoja yupo chuo nikaonana naye alikuwa amekaa alipenda kukaa peke yake mara nyingi nikamfata nikampasa salam akaitikia.
Nikauliza mbona kimya hata hukunitafuta akasema nitakutafuta muda bado haujafika. Basi nikamuuliza tena Jina akasema mda ukifika nitamfahamu alidai mda bado.

Tulipiga story kidogo akanyanyuka kuondoka nikamuuliza mbona unaondoka akasema anawahi kipindi nami nikamuacha.
Kama bahati CR wao alikuwa ni jamaa tulie fahamiana kwa mda mfupi sababu akitoka mkoa mmoja na mimi hivyo tulishare Kabila. Ilibidi nimtumie yeye kumfuata na kumueleza kua anisaidie kupata namba za binti fulani nikamuelekeza sifa za huyo binti ili ajaribu kupata mawasiliano yake, alisema atamtafta ili amfahamu. Baada ya siku kadhaa alisema amemuona sema hajapata kumfahamu Jina wala hajapata mawasiliano yake maana binti yupo serious sana.
Siku zikapita CR akasema amepata namba zake hivyo atanipatia.

Dahh kwakweli nilifurahi sana ilibidi nikomae na huyo CR ili nipate namba.
Siku moja nipo geto CR akanitumia namba 075XXXXXX4 Akaniambia Jina kanaitwa ka Adelina.


To be continued...
 
Siku akimaliza waugwana naomba mnitag maana tushachoka na hizi story zisizoisha.
 
Back
Top Bottom