Ni baada ya mjadala mrefu tuliokuwanao kuhusu "Imani za Kishirikina na Mahusiano ya Kimapenzi" ndipo nilipofikia uamuzi wa kuileta mada hii hapa.
Nukuu za wachunguzi wa masuala ya mahusiano ni kuwa:
1. Wanawake wanaongoza kwenda kwa waganga kuzidi wanaume.
2. Wanawake wazuri kwa sura au umbo siku hizi ndiyo wanaongoza kwenda kwa waganga wa kienyeji ukilinganisha na wale wa kawaida.
3. Dawa zinazoongozwa kutafutwa ni; Kummiliki mpenzi, Kumrejesha mpenzi wa zamani na Kusafisha nyota ya mapenzi.
4. Hata wanawake wasomi (walioko vyuoni na wale wa makazini) wanashiriki ushirikina huu sana tu.
(Kwa lugha nyepesi ni washirikina sana)
Nilipoanza kufuatilia kiini chake ni nini, nimegundua yafuatayo:
a. Hawajiamini
b. Wanajazana ujinga kufikiri kuwa "uzuri wao" ndiyo maisha.
c. Wanashindwa kuelewa kuwa mapenzi ni zaidi ya uzuri wa umbo.
d. Wakihisi uzuri wao unapungua hufanya viroja na ni wepesi kukata tamaa (kauli zao, iwe katika utani au akimaanusha, huwa zinaakisi kilichopo mioyoni mwao)
Tafadhali nakaribisha maoni yako.