Ushirikiano mpya wa upinzani kuzaliwa DeFront

Ushirikiano mpya wa upinzani kuzaliwa DeFront

Mbona Chadema mnalilia sana ushirikiano........Zitto amewashika pabaya?!!
Chadema mnahangaika mno na Maalimu hadi kinyaa/kichefuchefu
Watashirianaje na Zitto 'msaliti' waliyemtenga 2015 na wanampa kila jina baya hadi leo??
Machadema yanalia..."eeh Zitto utufungulie safina.....eeh Zitto utufungulie safina.."

Sent using Jamii Forums mobile app
Pamoja na wakala wenu mueneza na mchochea tofauti miongoni mwa wapinzani, ndugu Yericko Nyerere, napenda kuwajuza kwamba, hii nia yenu ya kuwagawa wapenda mabadiliko haitatimia!
 
Nimekubali huu muungano, utasaidia pakubwa kupatikana democracy, wengi wanavyo fahamu democracy ni siasa tu, wakati democracy katika siasa ni sehemu ndogo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu utakuwa muungano au umoja wa vyama vya siasa? Vyote vinawezekana lakini vyama vitakavyo ungana au Kuunda umoja vitabaki na haki na uhuru wa kugombea nafasi mbali mbali za uchaguzi kuanzia kitongoji, kijiji, kata, wilaya hadi taifa. Katika uchaguzi wa 2015, UKAWA kwa wengi kilieleweka kuwa ni chama cha siasa. Wapiga kura wengi walighafirika kutoona jina la UKAWA kwenye orodha ya vyama vya siasa ambavyo vilikuwa na wagombea. Wapiga kura waliojiandaa kupiga kura kwa wagombea wa ukawa walilazimika kubadili maoni ya nani wa kumpigia kura. Kura nyingi ziliharika na kwa upande mwingine CCM alinufaika. Kama kutakuwa muungano mwingine uwe UKAWA au De-Front itabidi utoe elimu ya kutosha kwa wanachama wake na wapiga kura dhana, madhumuni na matarajio ya umoja huo. Pia itabidi kubadili katiba zao kutambua chombo hicho. Mchakato huu utakuwa mrefu. Kwa kuzingatia kuwa vyama haviruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara, uchaguzi wa Serikali za mitaa utakuwa kama 2015 na uchaguzi mkuu 2020 inawezekana usiwe na mabadiliko. Suluhu ni kuunda chama kipya au kubadili kati ya UKAWA na De-Front kuwa chama cha siasa. Muda upo wa kusajili na kutafuta wanachama ambayo itakuwa fursa ya kujitangaza wakati wa mchakato huu bila hivyo hali itakuwa kama 2015.
 
Kikwazo kitaletwa na Chadema.
Kama kuna mtu anabisa asubiri aone kwenye uchaguzi wa muhimu sana wa serikali za mitaa ambao Chadema wamelala kama vile hakuna kitu kiko mbele yao. Uchaguzi wa serikali za mitaa ni wa muhimu kuelekea uchaguzi mkuu.
Matokeo yake tunaona Wabunge tuliojua ni Makamanda wanaonyesha upimbi mkubwa kabisa wakionyesha hadharani ubinasi wao na kushiba fedha kwa kujitapa kabisa kuwa wameacha kuwatumikia wananchi kwa sababu walikua na Maternity Leave na huko Marekani.!! Matokeo yake wapiga kura nchi nzima welipuka kwa hasira kuwa kumbe wale wanaopigania Chama mpaka wanapata ulemavu na wengine kupoteza maisha yao wao hawana familia.
Pumba za mbavu kabisa!!
Mtu kama Nasari mwaka Kesho utashangaa Chini ya Mwenyekiti huyo atapewa tena nafasi ya kupeperusha bendera ya Chama.
Halafu chama kikikosa kura mnailalamikia Tume.

Wapinzani waanze kwanza kuungana kwa kuachiana viti kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ni lazima siasa iangalie mazingira ya eneo na itikadi za vyama.

Suala lisiwe tu kuwa ni chama gani kilichopata kura nyingi Chini ya ukawa lakini pia itikadi za vyama na muitikio wa wapiga kura wa eneo hilo.

Bila upinzani imara hii CCM kitakua chama cha wakoloni weusi wasiojali wapiga kura ,chama kisichokua na hofu yoyote ya kuwadharau na kuwagandamiza na kuwanyima haki wananchi.

CCM hata ikishinda lakini isishinde kwa Ushindi wa zaidi ya 55% nchi hii itakua mahali pazuri sana pa kuishi . CCM ikishinda kwa zaidi ya 55% kwenye serikali za mitaa ,madiwani na wabunge; kwa sheria walizopitisha nchi hii itakua kama kule Afrika ya kusini wakati wa utawala wa Makaburu. CCM ndio watakaokuwa wenye nchi na watu wa daraja la juu. Wengine wote watakua ni kama wahalifu kwenye nchi. Umma utakua umeridhia kila kitu kinachofanywa.
Yaani Bunge kukaa gizani , Uhuru wa habari kuendelea kuwa finyu zaidi, Uhuru wa kisiasa kuwa ni uhalifu mkubwa . Magereza itakua ni nyumba za watu wenye mitizamo tofauti na CCM.





Sent using Jamii Forums mobile app
Katiba mpya ndio dawa ya yote..Ila sababu watanzania waoga wanawachekea serikali..
 
Kuna mkakati wa kuanzisha ushirikiano mpya wa vyama vya upinzani nchini kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 lengo likiwa ni kuing’oa CCM madarakani, utakaojulikana kama, The United Democratic Front (DeFront) au (U-Front).

Wazo hilo lilitolewa wakati vyama 10 vya upinzani vilipokutana Zanzibar na kutoa Azimio la Zanzibar, na huenda hatua ya Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa muumini wa UKAWA kuhamia rasmi ACT- Wazalendo kumekoleza chachu ya vyama hivyo kutaka kuungana.

Wazo la ushirikiano huo linaweza kufanana na wazo la Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe la kuanzisha muungano mpya wa ushirikiano wa vyama vya upinzani, The United Democratic Front (DeFront).

Zitto alieleza kuwa ana dhamira ya kuona vyama vya upinzani na taasisi nyingine mbalimbali zikiunganisha nguvu dhidi ya CCM katika chaguzi mbalimbali.

Ushirikiano huo wa vyama unaelezwa kuwa mbadala ya UKAWA ya sasa.

Kwa mujibu wa Mwanachama mpya wa ACT, Nassor Ahmed Mazrui ambaye kabla ya kuhamia ACT alikuwa naibu katibu mkuu wa CUF, amesema ushirikiano unaotakiwa kujengwa sasa unapaswa uwe zaidi ya vyama vya siasa kutokana na hali halisi iliyopo.

“Sasa waathirika ni wengi ukilinganisha na vipindi vingine, wafanyabiashara, waandishi wa habari, wanawake na makundi mbalimbali yameumizwa; tunahitaji mabadiliko ya haraka na siyo tu kuwa na muungano wa vyama vya siasa pekee badala yake tunapaswa kuhusisha na taasisi za kiraia.

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu amesema kwa sasa majadiliano ni namna gani vyama hivyo vitashirikiana kufanya kazi pamoja baada ya azimio lile la Zanzibar.

“Inaweza isiwe UKAWA tena na kuwa kitu kingine kabisa, pengine vyama vikaamua kuongeza chama kimoja au vyote, hii itajulikana baada ya vyama kutoa mapendekezo yake na kujadiliwa kwa pamoja pindi tutakapokutana.”

Chanzo Mwananchi.

Ushirikiano mpya upinzani kuzaliwa

Huo ushirikiano wa vyama vya upinzani kisha mnamchukua kiongozi toka ccm ndio anakuwa kinara, huo ni wendawazimu kama wendawazimu mwingine. Safari hii kitendo cha kuunda umoja kisha kumteua mwanaccm kuongoza tutawakataa hapa hapa kimachomacho. Ile blunder ya Lowassa hatuko tayari tena.
 
Ukawa ulileta matokeo makubwa sana hivo ni Wazo jema kuunda ukawa yenye cdm,act,nccr,cuf wao waungane na ndugu zao.Kwa kuunganisha nguvu kutaleta msukumo mpya wenye nguvu hata polisi hawatoweza ubomoa,polisi pia waelimishwe mabadiliko hayo yanafaida kwao pia juu ya maslai yao bora,ikiwemo mishahara, makazi, vyeo ambavo ni haki yao waliyopora na wanaowatumikia Bila fadhila pia wakicheza kikokotoo kiko likizo kitarudi ambayo itakula kwao.Pia tuombe sana jumuia za kimataifa zije zisimamie uchaguzi Kama ilivo kuwa congo ili kuleta matokeo ya haki,watu wachague wawakilishi wawatakao na sio wa kupangiwa.
 
Huu utakuwa muungano au umoja wa vyama vya siasa? Vyote vinawezekana lakini vyama vitakavyo ungana au Kuunda umoja vitabaki na haki na uhuru wa kugombea nafasi mbali mbali za uchaguzi kuanzia kitongoji, kijiji, kata, wilaya hadi taifa. Katika uchaguzi wa 2015, UKAWA kwa wengi kilieleweka kuwa ni chama cha siasa. Wapiga kura wengi walighafirika kutoona jina la UKAWA kwenye orodha ya vyama vya siasa ambavyo vilikuwa na wagombea. Wapiga kura waliojiandaa kupiga kura kwa wagombea wa ukawa walilazimika kubadili maoni ya nani wa kumpigia kura. Kura nyingi ziliharika na kwa upande mwingine CCM alinufaika. Kama kutakuwa muungano mwingine uwe UKAWA au De-Front itabidi utoe elimu ya kutosha kwa wanachama wake na wapiga kura dhana, madhumuni na matarajio ya umoja huo. Pia itabidi kubadili katiba zao kutambua chombo hicho. Mchakato huu utakuwa mrefu. Kwa kuzingatia kuwa vyama haviruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara, uchaguzi wa Serikali za mitaa utakuwa kama 2015 na uchaguzi mkuu 2020 inawezekana usiwe na mabadiliko. Suluhu ni kuunda chama kipya au kubadili kati ya UKAWA na De-Front kuwa chama cha siasa. Muda upo wa kusajili na kutafuta wanachama ambayo itakuwa fursa ya kujitangaza wakati wa mchakato huu bila hivyo hali itakuwa kama 2015.
Kuunda kuwa chama kimoja ni ngumu sana kwa hulka ya wanasiasa tuliona, halafu kwa msajili huyu anayeshiriki kuua vyama sidhani kama atakisajili kabla ya uchaguzi 2020.
 
We we ndio mjinga na mpumbavu asiyejua anafanya nini humu na kwenye nchi hii na dunia kwa ujumla. Upo kama hayawani asiyejitambua kabisa.

Nenda kwenye post ya mtoa mada jenga hoja zako ili tuzisome.
Utushawishi ,tujue unawaza nini juu ya mwelekeo wa siasa za Nchi yetu . Eleza unachokiamini wewe .
Watu wa aina yako ndio adui wakubwa sana wa Demokrasia ya nchi hii.
Watu wasio na uwezo wa kujenga hoja za kukosoa kistarabu au kutoa hoja zao.
Watu hapa kumfurahisha mtu wala kumkomoa mtu ndio maana tumejificha humu.

Eleza kwa nini hukubaliani na hoja zangu lakini sio kuja na ushuzi kama wa mtu aliyevimbiwa mayai ya kienyeji.

Ndio maana mnashindwa kujenga vyama mbadala vyenye hoja na ukavu wa kisiasa. Haiwezekani wewe tu ndio uwe na mawazo mazuri uliyoyaficha huko kichwani kwako bila hata kutueleza kwa hoja tukaluelewa.

Mimi hoja nazijibu kwa hoja na nikiikubali naweka Like.
Na sio kawaida yangu kujibu watu wa aina yako.
Watu wa aina yako hawana tija kwa mustakabali wa taifa letu mana hawawezi kuwafungua macho watanzania wakajua jinsi wanasiasa walivyowalaghai na wasio na utu wala huruma na mtu zaidi ya matumbo yao.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria imeshaanza kutumika ila haijazuia vyama kushirikiana.
Waambie hawa jamaa wanauelewa mdogo sana wa kisiasa zaidi ya kuwa wanaharakati.
Unajua mwanaharakari anaweza tu kuibuka na kupinga jambo lolote hata kama wengi wanalikubali kidemokrasia.
Mwanasiasa ni lazima uheshimu maamuzi ya wengi.

Watu wanabaki kulalamika badala ya kujipanga mapema namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo za sheria hiyo bila kuivunja.

Ilikua ni kipindi cha vyama vya upinzani kutulia mana sheria imeshapitishwa ,na kwenda kuonana na msajili ili wakae naye kama wadau na ikiwezekana waweke kumbukumbu vizuri ili wapate mwongozo zaidi juu ya mipango yao ya kuachiana viti majimbo na kata ! Wajue mapema changamoto zilizopo. Na ikiwezekena waanze kujipanga sasa kugawana majimbo na Kata mapema kabisa.

Wanasiasa vijana wa sasa wamekua na mhemko mno mpaka wanapoteza hekima,busara na maarifa ya kisiasa.

Watabaki kulalamika tuuuu mapaka uchaguzi ufike na watakimbilia Kuchukua form na kuanza kampeni na kuanza kupigiana kampeni na kutangaza kuwa wameungana. Halo ndio utajua kuwa hatuna wapinzani bali matawi ya CCM ya kuzuia wapinzani wasiingie madarakani.
Walitakiwa baada ya sheria kupita waanze sasa kuachiana majimbo kimya kimya na kuanza kuwajulisha wananchi kuwa hawatasimamisha wagombea wawili kwenye majimbo ya vyama fulani. Ijulikane kabisa ili wakati wa uchaguzi wawe wameshamaliza kazi na kuepuka mapinangamizi.


Ama la waende mahakamani sasa ili kuomba tafsiri ya kimahakana juu ya sheria hiyo kama inakiuka katiba au vipi. Wapate tafsiri mapema ili waepuke mapingamizi mana Wapinzani wengi hua wanahongwa sana kisha wanavuruga uchaguzi mapema wakati wa kujaza form. Iliwahi kutokea kwa mmoja kule mbeya alijiapisha mwenye kwa sababu ni mwanasheria na alijua kabisa kuwa anafanya makosa.

Ukiwaambia ukweli wanatukana sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema wanalilia sana muungano ili wapate kuwachezea rafu wenzao
Safari hii bara hakuna kitu
 
Back
Top Bottom