Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,952
- 10,037
Wananchi wa Kata ya Kivule wamefurahishwa na ushindi wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kivule Mwita Mwikabe Waitara kutokana na kuanza kutumikia wadhifa huo kwa kishindo kikubwa.
Ni wiki moja sasa kuna ukarabati mkubwa wa barabara za mitaa ya Kivule na ile itokayo Banana kwenda Kivule.
Taarifa zinasema mara baada ya kuapishwa Mwenyekiti wa mtaa huo Mwita Waitara alivamia ofisi za Manispaa kuelezea kero za wananchi wa Kivule kutokana na ubovu mkubwa wa barabara.Waitara alitaka kuona bajeti nzima ya miundombinu ya manispaa.
Kutokana na hali hiyo Waitara aliahidiwa ukarabati wa barabara hiyo na kesho yake ukarabati ukaanza.
Akikagua ukarabati huo Mwita Waitara aliwaeleza wananchi waliomzunguka kwamba hiyo ndiyo CHADEMA na kuwaambia kamwe hatalala huku wananchi wake wakitembea kwa miguu kwa ubovu wa barabara.
Diwani wa Kivule na mbunge wa Ukonga Eugene Mwaiposa wanatoka CCM lakini siku zote wamepuuza kilio cha wananchi kuhusu ubovu wa barabara.
Picha chini ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kivule Mwita Mwikabe Waitara
Kamanda Molemo na wengine, nichukue nafasi hii kumpongeza Waitara kwa kazi njema anayowafanyia watu wa Kivule. Lakini mbona yeye ameweza na huku hana hela; amepiga ambush manispaa na wametekeleza ukarabati. Sasa huku kwetu Jimbo la Ubungo mbona tukisema watu wanasema sasa Mnyika atatoa pesa mfukoni kufanya ukarabati wa barabara! Mnyika afanye kama alivyofanya Waitara huko Kivule.
Last edited by a moderator: