Ushindi wa CHADEMA Ukonga waleta neema

Ushindi wa CHADEMA Ukonga waleta neema

Ngoja Nimuulize kamanda Thomas Nyahende kama kweli Mwita Mwikabe ndio mwenyekiti wa Kivule, pia aniambie kama huyu ndie alikuwa Raisi wa Daruso nilipokuwa mwaka wa kwanza 2005, kama ni kweli basi tuna under utilize resources, maana jamaa anauwezo mkubwa sana katika uongozi

Kwa kawaida kama u-kiongozi mzuri anzia hata ngazi ya chini watu wakiona uwezo wako utapanda tu.Hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Huwezi kuwa Manager mzuri kama haujawahi kuwa karani
 
Kwa kawaida kama u-kiongozi mzuri anzia hata ngazi ya chini watu wakiona uwezo wako utapanda tu.Hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Huwezi kuwa Manager mzuri kama haujawahi kuwa karani

Umeongea ukweli mtupu kamanda
 
Asante sana Kamanda wangu Mwita Waitara,,KAzi yako imeonekana....Ni wakati sasa wananchi waone juhudi zako na wakupatie Udiwani uwahudumie vizuri......
 
Waitara namheshimu sana na anaijua siasa pia ni shupavu saaana

nilipata hofu sana kwenye sakata la Zitto kuwa pengine ni MM3

Nimetembelea Kivule na kuhakikisha uchapa kazi wake.

Nakumbuka uchaguzi mdogo Tarime na pia alivyobadili mindset ya wakazi wa jiji la Mwanza akiwa na Zitto viwanja vya Sahara kabla ya 2010

long live comrade!
 
Last edited by a moderator:
yule MM ambaye hakutajwa ni nani? au ndo Msafiri Mtemelwa sijui?
Wewe humjui MM?

Ndiye sterling wao, katika ile filamu iliyozinduliwa hivi karibuni, inayokwenda kwa jina la İgiza ndani ya nchi ya Tanzania.

Naye si mwingine, bali ni ZZK!
 
Chizi pekee ndiyo anaweza kuiamini hoja kama hii.
Comments zako, hazifanani kabisa na İQ ya huyo uliyemweka kwenye hiyo Avatar yako.

İQ yako na İQ ya huyo uliyemweka kwenye hiyo Avatar, tofauti yake inaweza kuwa sawasawa na umbali wa kutoka duniani hadi mbinguni!
 
Waitara namheshimu sana na anaijua siasa pia ni shupavu saaana

nilipata hofu sana kwenye sakata la Zitto kuwa pengine ni MM3

Nimetembelea Kivule na kuhakikisha uchapa kazi wake.

Nakumbuka uchaguzi mdogo Tarime na pia alivyobadili mindset ya wakazi wa jiji la Mwanza akiwa na Zitto viwanja vya Sahara kabla ya 2010

long live comrade!

Waitara anatekeleza sera za Chadema kwa vitendo.Chama kimemuamini kikampa nafasi.Anakitendea haki chama kwa utendaji wake.
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo unaamini hilo limefanywa na mwenyekiti wa mtaa aliyeapishwa wiki 2 zilizopita?
Kwamba hakukuwa na mipango yoyote kabla yake?

Kwa hiyo mipango hiyo ilisubiri mpaka Waitara aende kumshika mashati Mkurugenzi?

Kwanini mipango hiyo haikutekelezwa miaka mitano iliyopita barabara ikiwa mahandaki matupu?

Waitara aliwaambia wakazi wa Kivule kwenye kampeni katika viwanja vya Mwembeni kuwa akichaguliwa kazi ya kwanza ni barabara na yuko radhi kumfungia mkurugenzi wa manispaa ofusini.

Amechaguliwa ndani ya wiki mbili barabara imekarabatiwa.Kwa hiyo wananchi wamwamini nani?
 
Wananchi wa Kata ya Kivule wamefurahishwa na ushindi wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kivule Mwita Mwikabe Waitara kutokana na kuanza kutumikia wadhifa huo kwa kishindo kikubwa.

Ni wiki moja sasa kuna ukarabati mkubwa wa barabara za mitaa ya Kivule na ile itokayo Banana kwenda Kivule.

Taarifa zinasema mara baada ya kuapishwa Mwenyekiti wa mtaa huo Mwita Waitara alivamia ofisi za Manispaa kuelezea kero za wananchi wa Kivule kutokana na ubovu mkubwa wa barabara.Waitara alitaka kuona bajeti nzima ya miundombinu ya manispaa.

Kutokana na hali hiyo Waitara aliahidiwa ukarabati wa barabara hiyo na kesho yake ukarabati ukaanza.

Akikagua ukarabati huo Mwita Waitara aliwaeleza wananchi waliomzunguka kwamba hiyo ndiyo CHADEMA na kuwaambia kamwe hatalala huku wananchi wake wakitembea kwa miguu kwa ubovu wa barabara.

Diwani wa Kivule na mbunge wa Ukonga Eugene Mwaiposa wanatoka CCM lakini siku zote wamepuuza kilio cha wananchi kuhusu ubovu wa barabara.

Picha chini ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kivule Mwita Mwikabe Waitara
Muda wa ukarabati ulishafika tu
 
Comments zako, hazifanani kabisa na İQ ya huyo uliyemweka kwenye hiyo Avatar yako.

İQ yako na İQ ya huyo uliyemweka kwenye hiyo Avatar, tofauti yake inaweza kuwa sawasawa na umbali wa kutoka duniani hadi mbinguni!

maana huko mbinguni umekuwa ukifanya safari zako za mara kwa mara ndio maana hapakupi shida! unapajua sana hata umbali wake pia unaujua..
 
Kwa hiyo mipango hiyo ilisubiri mpaka Waitara aende kumshika mashati Mkurugenzi?

Kwanini mipango hiyo haikutekelezwa miaka mitano iliyopita barabara ikiwa mahandaki matupu?

Waitara aliwaambia wakazi wa Kivule kwenye kampeni katika viwanja vya Mwembeni kuwa akichaguliwa kazi ya kwanza ni barabara na yuko radhi kumfungia mkurugenzi wa manispaa ofusini.

Amechaguliwa ndani ya wiki mbili barabara imekarabatiwa.Kwa hiyo wananchi wamwamini nani?

Ngumu sana kwa amini hii, Samahani sana lakini.
Tunapenda mabadiliko wote , ccm siitaki hata kuisikia lakini kujiingiza kwenye propaganda nyepesi kwangu mwiko.
 
Kwahiyo unaamini hilo limefanywa na mwenyekiti wa mtaa aliyeapishwa wiki 2 zilizopita?
Kwamba hakukuwa na mipango yoyote kabla yake?

Kwani lipi lisilowezekana? Mbona yawezekana hiyo mipango ilikuwepo maana hata kabla ya uchaguzi walichonga chonga sana barabara lakini si katika kiwango kizuri maana ilikuwa inashangaza ni greda kweli imepita au vipi,lakini amekuja kuchonga tena katika kiwango angalau kidogo kizuri,hata kama ilikuwepo hiyo mipango kusimamia tu hilo kutekelezeka ni kazi nzuri.

Hujasikia ya huko Musoma mwenyekiti wa wiki 2 ameuza shamba la kijiji la ekari 200 kwa 3M(kama sikosei) amewezaje hili kutekelezeka kwa muda mfupi? Na amekiri kweli amefanya hili na kavuta laki 2.
 
Back
Top Bottom