Wananchi wa Kata ya Kivule wamefurahishwa na ushindi wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kivule Mwita Mwikabe Waitara kutokana na kuanza kutumikia wadhifa huo kwa kishindo kikubwa.
Ni wiki moja sasa kuna ukarabati mkubwa wa barabara za mitaa ya Kivule na ile itokayo Banana kwenda Kivule.
Taarifa zinasema mara baada ya kuapishwa Mwenyekiti wa mtaa huo Mwita Waitara alivamia ofisi za Manispaa kuelezea kero za wananchi wa Kivule kutokana na ubovu mkubwa wa barabara.Waitara alitaka kuona bajeti nzima ya miundombinu ya manispaa.
Kutokana na hali hiyo Waitara aliahidiwa ukarabati wa barabara hiyo na kesho yake ukarabati ukaanza.
Akikagua ukarabati huo Mwita Waitara aliwaeleza wananchi waliomzunguka kwamba hiyo ndiyo CHADEMA na kuwaambia kamwe hatalala huku wananchi wake wakitembea kwa miguu kwa ubovu wa barabara.
Diwani wa Kivule na mbunge wa Ukonga Eugene Mwaiposa wanatoka CCM lakini siku zote wamepuuza kilio cha wananchi kuhusu ubovu wa barabara.
Picha chini ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kivule Mwita Mwikabe Waitara

Ahsante sana kamanda Molemo kwa taarifa hii nzuri na yenye kuamsha ari.
Nampongeza kwa dhati kabisa Mwenyekiti wangu wa Mtaa wa Kivule kwa namna alivyoanza kazi za kuwatumikia wananchi mara moja baada ya kuchaguliwa kuwaongoza, hakusubiri mkurugenzi ajitafutie posho ya kumuapisha.
Na huu ndio mwelekeo kwa wenyeviti wangu wote wa mitaa tuliyoshinda Jimbo la UKONGA kufanya kazi kwa bidii, kwa kushirikisha wananchi lakini kwa ubunifu wa hali ya juu ili kutimiza matarajio ya waliowachagua.
Kazi yangu ni kuhakikisha kuwa nafuatilia hatua kwa hatua kutendaji na utekelezaji wa majukumu ya kila mwenyekiti wa mtaa anayetokana na Chadema katika jimbo la UKONGA na kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora kwa wananchi.
Picha chini ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kivule Mwita Mwikabe Waitara
Hili ni Jembe kama hautaki unaacha.
![]()
Last edited by a moderator: