Ushindi wa CHADEMA Arusha: Ushauri wa bure kwa CCM

Ushindi wa CHADEMA Arusha: Ushauri wa bure kwa CCM

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
710
Tatizo lenu CCM nikwamba mmekuwa mkidhania kwamba Watanzania wote ni watu bongolala, na kwamb mkitumia nguvu kubwa ya kuwatisha na kuwapiga mkitumia hao Grreen Guards wenu, basi, watanyamaza na kuogopa kwenda kupiga kura.

Nakubali kwamba kwa kiasi kikubwa, mbinu yenu hiyo chafu imefanikiwa huko Arusha. Idadi ya waliopiga kura jana, 14 Julai 2013, ni ndogo ililinganishwa na wale waliojiandikisha. Lakini someni alama za nyakati; licha ya hilo, CHADEMA imeshinda kwa kishindo. Mmeangukia pua, pwaaaaaa! Hayo maumivu!!

Mmeipaka CHADEMA matope, mmetumia rafu zote, huku mkiwa na Jeshi la Polisi, JWTZ, Usalama wa Taifa na Jeshi la Magereza nyuma yenu. Mkaamua kuwaasi wananchi ambao wamewapa dhamana ya kuwa chama tawala.

LAKINI BADO MMESHINDWA!

Hivi mnadhani haya manyanyaso hayana mwisho? Nawasifu sana watu wa Arusha kuwa na msimamo. Wakiamua kufanya jambo, wanalifanya. Si waoga kama sehemu nyingine. Lakini nadhani Watanzania wote sasa watajifunza kutoka kwa wenzao wa Arusha. Hilo kaeni mkijua litafanyika, mtake msitake. Sasa tumefika ukomo wa uvumilivu; dawa yenu iko kwenye sanduku la kura.

CCM bado mna uwezo wa kuirejesha nchi mikononi mwenu, kwa amani, iwapo mtafanya yafuatayo:

1. Tekelezeni ahadi zenu zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya 2010. Mlichoahidi hakijatimia.

2. Elekezeni nguvu zenu kubwa, ambazo mmekuwa mkizitumia kucheza rafu, kwa shughuli za maendeleo.

3. Acheni kutumia vyombo vya dola kinyume cha sheria.


Nahitimisha hapa kwa kuwaponda kidogo, mkae mkielewa jinsi tulivyo na furaha ya ushindi, japokuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa, lakini ushindi huu wa CHADEMA ni ushindi wa WATANZANIA WOTE, kwani haki imetendeka.

Nawaponda kutumia wimbo wa marehemu Mbaraka Mwaruka Mwinshehe, "Jogoo la Shamba", kama ifuatavyo:

Hilooooo CCM!
Ulijidai wewe mbabe sana ooo!
Leo umepigwa na kijana mdogo CHADEMA!
Wewe uliona wapi jogoo la shamba CCM likawika mjini Arusha?

Utampiga nani we CCM?
Je ungepambana nami Mtanzania Mzalendo
Aibu ingekupata CCM!
 
Kipigo walichokipata arusha hawatakaa wakisahau maishani mwao kwani kimewadhalilisha sana.
 
CCM wanatakiwa wabadilike na kutambua hiki si kizazi cha zidumu fikra za mwenyekiti, wakijatambua wataachana na siasa za chuki
 
ushauri mzuri sana,nami nashauri ccm ijitenge na Nape,mwigulu,wasira kwani hawa wanapandikiza siasa za ukabila na ukanda,wamekuwa wakihubiri kuwa chadema ni chama cha kaskazini,sasa arusha iko ukanda gani? Walifuata nini arusha? Wamevuna walichopanda.
 
Sasa hivi wale wezi wote wa CCM (vigogo serikalini) wataanza kuzikimbiza hela zao walizotuibia nje ya nchi kuhofia kukamatwa na kuchukuliwa hatua baada ya ushindi wa chadema kunako 2015. Haki ya nani lazima hawa watu wachunguzwe account zao ili kujuwa walizipataje hizo hela zao kisha wachukuliwe hatua na kuwekwa museum ili raia tupate kuwatupia mawe na kuwakejeli.
 
CCM haitakiwi Arusha, Arusha niliyoikuta siyo ya leo. Kulikuwa hakuna barabara za maana lakini jamaa wamejitahidi sana kujenga hata kama ni kwa mkopo lakini hiyo haijawasaidia kuwaokoa na kipigo.
 
Naanza kwakuchangia haja hivi. Nidhahiri mhindi huendana nyakati ili kukua huanza gunzi alafu mbelewele alafu punje, na hatimae kukomaa hatuwa yakwanza, alafu unaingia kwenye mchakato ufuatao, unafaa kwa kuchemsha na kuchoma ukipenda, Ila ukikomaa atua ya pili ata ufanyaje haufai kwa yote mawili, kuchoma ata kuyachemsha, ukilazimisha utaambulia kung'oa meno na maumivu ya kichwa ukitakakujuwa ukweliwa mambo waulize waliyo pigwa chini ARUSHA nimemaliza.
 
Ukweli Umedhihirika! Chadema wameshinda na fujo hakuna. Wanachadema wanatambua ya kwamba Tanzania yenye amani ni bora kuliko fujo. Uchaguzi utakuja na utapita lakini Tanzania itabaki. CCM watambue kuwa haki ikidhulumiwa Mungu hulipa kwa njia yake yeye kwani alisema visasi vyoye atalipa yeye. Mungu ibariki Tanzania, Arusha na CHADEMA.
 
Propoganda kuwa Arusha kuna fujo zilikuwa za CCM. Wakauwa watu wetu bila sababu, wakapiga watu wetu mabomu walipotaka kuaga marehemu ,wahanga wa bomu la Nchemba, wakajaza maaskari elfu kumi na moja, wakakamata vijana wetu bila sababu, wakatumia jeshi lao za ziada la green guard kupiga na kuwaumiza wenzao bila sababu. Propaganda zote na uchafu wote haukusaidia kitu. The boomerang has re bounced. Arusha iko mikononi mwa CDM siku nyingi hawakujua.
 
Back
Top Bottom