Ushimen: Ebu ngoja leo niwape mawazo machache ya kujikwamua

Habari mkuu ushimeni,naomba pia maeneo ya kuuza mayai ya kisasa,au biashara ya mayai ya kisasa kwa dodoma
Hii biashara sina uzowefu nayo, ingawa mayai naona kwawingi yakiuzwa sokoni na kuna baadhi ya maduka watu wamefunguwa kwaajili ya kuuza mayai kwa jumla na rejareja.
 
Pole na hongereni kwa kuwa wenye afya njema. Na kwapamoja tuwaombee wale wote ambao wakati kama huu hawana nafasi ya kusoma haya tuliopata pumzi ya bure na tukayasikia, kuona, kusoma na kuchangia. Kwakuwa Mungu wetu ni mwema, basi yote kwake ni mema pia.

1. Ungekua Dom ningekupa wazo/location ya biashara ya chipsi dume, na ninahakika hapa ungeweza kupata faida isiyo punguwa 10 elfu per day, kwa mtaji usio zidi elfu 300.

2. Pia ningeweza kukupa wazo/location ya biashara ya majeneza ambapo ungeweza pata faida isiyo punguwa 100 elfu kwa kila wiki kwa mtaji usio zidi elfu 1,200.

3. Na ningekupa wazo/location yenye ungefanya biashara ya matunda kwa mtaji usio zidi 400 kwa kupata faida isiyo punguwa 12 elfu daily.

4. Alafu ninge kupa wazo/locations kadhaa ya kufanya biashara ya shoe shine/kusafisha viatu kwa mtaji usio zidi 100 elfu na ukapata faida isiyo punguwa 5 elfu kila kukicha.

Ebu ngoja nimalizie kwanza hii whatever-Vant, then kesho nitakuja na mawazo mengine kwenye muendelezo.
Fafanua namba mbili mkuu
 
Back
Top Bottom