Ushawahi pitia kama hii single father?

Ni ngumu kwa sana kwa mama wa kambo kumpenda mtoto asiye wake. Hii kitu sikia tu kwa wengine. Tena mbaya zaidi ukute huyo mama wa kufikia hana mtoto. Naanza kukuelewa mkuu. Story saingine ikiwa nusu ni rahisi mtu kuhukumu

Mara nyingi inatokea ikiwa mwanaume hana maokoto
Ukiwa na maokoto mwanamke atakupenda na kizazi chako chote
 
Wakati bado unajitafuta mlee mtoto kwa misingi mizuri ya kimaadili na kimila hakiisha unamuasa kila upatapo nafasi kuhusiana na maisha hasa kujiheshimu na bidii, lakini yote ya yote mpe msingi wa dini hii itamsaidia hata kama atakuja kukengeuka huko mbeleni basi awe na msingi wa dini utakaomsaidia kujikwamua

Sijajua we ni imani gani ila Biblia inasema mlee mtoto katika njia impasayo nae hataiacha hata atakapokuwa mzee

Kila la heri
 
Brother hauna mzazi yoyote ambaye yuko hai ?
Kama bibi yake yuko hai jaribu kumpeleka akapate maradhi mazuri, huyo mtoto una mduhurumu vitu vya msingi baadae atakuja kukulahumu huyo 🥹
Wapo lkn nimewaambia subilin kwa sasa sina changamoto ambayo binafsi ninaona nimtoe dogo ila kama kunamabadiliko yakitokea nitafanya hivyo tunaishi vizuli kabisaa kwa furaha na amani tele
 
Mkuu ulianza kukaa naye akiwa na miaka mingapi?
 
Hakikisha yupo huru kukueleza kama atakutana na changamoto huko nje.

NB: Hiyo bond uliyotengeneza na bintiyo ni ngumu mno kuishi na mke na mkawa kama mlivyo sasa labda umpeleke mahali.

Mama wa kambo akija,kazi ya kwanza itakuwa ni kukufitinisha naye sasa utachagua nani abaki.
 
Baki na mwanao.
 
Good life lakini it is better ukawa na dada wa Kazi hapo nyumbani kwa ajili ya kufanya shughuli mbili tatu hapo nyumbani .
 


Unajiweza sana, usikaribishe matatizo Nyumbani kwako. Kama una ndugu binti mkubwa hata wa kumsaidia kusoma course kama cherehani, mlete amchangamshe Dogo, Mambo ya kuoa waachie Vijana wa kinondoni maana hawanaga mda na malezi ya watoto.
 
Dah hongera mkuu,Kwa ishu ya kuamka kusoma inabidi uzoee tu,good stuff.
 
Boss,wewe una tatizo,Mazingira unayolea huyo mtoto ni mazingira hatari sana,kwa umri wake.Kama una ndugu au rafiki ambaye ana stable family mpeleke, Au mpeleke kwa bibi mzaa baba au hata mjomba au shangazi.

Maana naona kuo umeshindwa na kwa namna fulani huwamudu wanawake.Utamuharibu mwanao kuwa makini usijemfanya Mke na wewe ukawa ndio abuser number one.
 
Umeongea kama mwanaume na baba🤛
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…