Ushawahi kukanwa? (Kisa cha kweli)

Ushuhuda mzuri kumbe kweli mpo na ndio nyie ambao mtoa uzi anawaongelea.
 
Huu ujinga unaoufanya ukiwa na nguvu zako jitahidi sana uuache kabla hujakumbwa na maradhi yoyote yale, hivi mkuu umeshawahi kwenda pale muhimbili japo jengo la moyo tu ukaona vile mgonjwa anahitaji hata mpita njia tu ampe faraja? Pale pesa sio kitu kbc aiseee
 
Isee man you got some shits in your system!
 
Tulienda kwenye bday ya mmoja wa classmate ambae alikua na urafiki na ex bf. Sasa rafiki zetu walikua wanajua kuna kitu kati yetu ila sisi tunazuga. Kufika wakamtambulisha eti unamjua S akasema hanijui hajawahi kuniona kwanza niko course gani. Na mie nikauliza kwani huyu ndo nani mbona na yeye sijawahi kumuona class. Wakaniambia huyo ndo mtu fulani nikaawambia sijawahi muona class. Sasa baadae tukaja kudate akasema eti alijihu vile makusudi sababu hakuna mtu darasani ambae alikua hanijui sasa na yeye akaona akisema ananijua ataonekana ananishobokea kama wengine wakati na mimi namjua nilimjibu makusudi simjui maana naachaje kumjua kipanga wa darasa halafu handsome
 
Sasa nadhani wewe ndo unaezungumziwa na mtoa mada
Jifunze
 
Tatizo sio pesa..ni moods..ila issue za muhimbili sidhani kama mfano wako ni valid ..kwani kusalimi na kumpa MTU faraja mwenye uhitaji vina uhusiano gani?
 
Huyu alijibu sawasawa na Mara nyingi hili hutokea maana kwa kusema tu anakufahamu yawezekana asitumike katika kukusaili au ikakuondolea favour yeyote .
 
Ukiwa na Tabia ya Kushobokea Watu hayo yatakukuta tu.., Kataa Pepo wa Ushobokaji huyo!!!
Hii inaweza changia kweli...

Zamani nilikuwa na tabia ya kusalimia sana watu ambao tulipotezana kwa muda mrefu ila nilichokuja kiona ni kuwa baadhi hujifanya wamekusahau hata umkumbushe vp atajifanya kasahau.

Nilichoamua ni nikihisi kumfahamu mtu nikaenda msalimu akijifanya hanikumbuki basi na mimi napotezea wala sipotezi muda wa kumkumbusha lolote naendelea na mambo yangu.
 
Vibaya mkuu sasa si unamwambia tu mtawasiliana hata bdy uko busy kuliko kumkana
 
Nishawahi kumkana dada mmoja wakati nipo Secondary. Yule dada nilianza kumfatilia ikatokea akahamia shule nyingine. Baada ya kama mwaka hivi na mimi nikahamia hiyo shule nikakutana nae nikataka kumchangamkia akajifanya hataki shobo na mimi so tukawa tunapishana tu. Kuna siku sijui mashetani gani yamempanda kaja class kwetu anawaambia marafiki zake ambao nasoma nao darasa moja kuwa huyo jamaa namjua nimesoma nae shule flani. Wakaniuliza nilimkana aisee mbele yake nikasema simjui na hiyo shule sijawahi kusoma kabisa.
 
Hii mara nyingi huwa wanaifanya madada, yaani unaweza usiamini. Washikaji huwa ni wachache. Hapa pia kuna kufananisha watu, mtu anakufananisha na anakukomalia kiwa ndio wewe lakini unamringia hivyo inabidi umuelezee mtu vizuri na akiwa hakuelewi au umemfananisha basi muachane salama, binafsi iliwahi nikuta nipo kwenye bus kubwa tumesimama mara dada mmoja akanigusa nikamsalimia akaonesha kunichangamkia lakini mimi sikumtambua kwa kipindi hicho, akaniuliza unanikumbuka nikamwambia hapana naomba unikumbushe, ajabu akakasirika akapanic kabisa eti kama hunikumbuki basi, nikajaribu kumsihi lakini wapi Dada hataki kabisa, nikaona isiwe tabu nikatemana nae, muda mwingine mtu unapitia mambo mengi so unatakiwa umboost kidogo mtu ili akumbuke ukiona bado na umefikia mwisho wako wa kujieleza achana nae.
 
Kuna mtoto wa dadangu alitoroka kwao akakimbilia Dar ndo tukawa tumempata tukampeleka polisi kwa sababu tulikuwa tushachukua rb na report kadhaa kufika kituon mimi dada yake na jamaa fulani dogo alitukana hatujui na jina akabadili Asee tulichanganikiwa hatukujua cha kufanya ila polisi walitumia busara wakatwambia tuondoke watajua cha kumfanya mpaka aseme ukwel dogo alikomalia hatujui sisi ni majambazi tunataka tumteke ila mwishoni alikubali na alirudi kwao
 
Ushauri wa busara watu wengine duniani wanajiona wako peponi
 
Mdingi aliwahi kuniambia 'mi sio baba ako' akaita security akawaambia mtoeni nje huyu
Nilikuwa nimemfuata kazini kwake kuhusu mambo ya shule
Niliondoka nikilia siku hiyo
Sijui ntaisahau vp hii
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…