Ushawahi kuambiwa hivi na Interviewer?

Ushawahi kuambiwa hivi na Interviewer?

Kwenye interview uliza utegemee majibu lini, tatizo huwa tunakuwa waoga waoga sana hadi kuuliza maswala muhimu. Tumeaminishwa kuukiza baadhi ya maswali ni tatizo ila in reality ndio maswali muhimu, wanapaswa kujua unafuata muda na una ratiba.

Unakuta mtu anaogopa kuuliza benefits na opportunities zilizopo eti ataonekana kafuata maslahi, wao tayarivwanajua unatafuta mshahara kihalali sasa unaogopaje kuuliza vitu vingine.

Kazi yangu ya kwanza kabisa niliipata kwa kuuliza kama kuna benefits na opportunities nyinginezo job, ile namaliza tu mwenye firm pale pale akaniambia "dogo kazi umepata".

Nikiri tu kuwa binafsi sikuwa na mpango sana na ile kazi na nilikua na test tu zali so sikuwa najali sana zile kanuni za interview sijui usiulize salary n.k tangu hapo nkajua hazina maana. Na kazi usitafute ukiwa na njaa utateseka zaidi.
Ndo keshauliza sasa kajibiwa very soon,ndo anauliza hiyo very soon ina maana gani?
 
Mara nyingi wahanga wa ajira tunapotoka kwenye usaili huwa tunajiuliza maswali mbalimbali kulingana na ulivyojibu maswali kwenye usahili kwamba je utapata hiyo kazi au la.

Inapotokea Interviewer kakuambia "i will call you very soon" mara baada ya kufanya usaili je nini hasa tafsiri yake, ni kwamba ndo anakupa mkono wa kwaheri kijanja au kuna matumaini ndani ya hiyo kauli yake?

Karibuni wazoefu tusaidiane kuhusu hili.
Hapo tafuta kazi sehemu nyingine, nakuapia usitegee hapo tena na utakuja kuniambia.
 
Mkuu kama unaweza kuwa unafatilia itapendeza sana. Waajiri siku hizi wanatoa ajira kwa watu ambao wapo serious.
Kuna taasis flani ilitangaza kazi mwaka jana. Watu wakaapply na kuwa shortlisted. Kuna jamaa mmoja hakuitwa wakati sifa zote anazo. Baada ya interview watu wakapangiwa vituo vya kazi. Jamaa yule kusikia akawa kila mara anaenda kuulizia kwann hakuitwa interview na sifa anazo?
Wakawa wanasema mara hawakupokea email yake, akathibitisha kuwa email ilifika, basi wakamwambia watampigia baada ya week 2. Week zilipoisha jamaa akawafata tena kuulizia mbona hawakumchek, ikabidi wamwambie atume upya application. Jamaa akatuma. Baadae aliitwa akafanyiwa interview, alianza kazi mwaka huu mwez january wakati wale wengine wameshamaliza miez 6. So yupo kazini sasa mwez kama wa nane saiv. Na leo nimeongea nae akawa ananikumbusha huo mchakato.
Anajiuliza kama asingefatilia leo hii angekuwa wapi?
So, komaa ndugu. Fatilia, ikibidi tafuta mahusiano mazuri na HR
Kesho naenda kwenye hiyo kampuni kuulizia majibu.
 
Back
Top Bottom