Ushawahi kimbiwa na mumeo???lipo jibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushawahi kimbiwa na mumeo???lipo jibu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Dec 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,453
  Likes Received: 5,703
  Trophy Points: 280
  Mume kutoweka!

  Kwa mwanamke ambaye alikuwa na ndoto za maisha bora ya ndoa kuondokewa na mume huleta maumivu makali sana, ni janga na hasara kubwa sana kwake.
  Kuachwa mwenyewe ni badiliko kubwa katika maisha linalokuacha unahangaika mwenyewe na kujikuta ghafla unahusika kifedha, kulea watoto na kuendeleza taaluma kama si kuanza taaluma mpya.

  Kama umepitia hali hii au unapitia hali hii ya kutalikiwa au mume kufa au mume kutoweka na kukuacha wewe na watoto au hata namna yoyote basi fahamu kwamba si nina yangu kutonesha kidonda ulichonacho bali ni katika kusaidiana ili uweze kukabiliana na kushinda na hatimaye kusimama katika changamoto hii kubwa uliyonayo.

  Kumbuka hukuchagua iwe hivyo, na mume kutoweka si mwisho wa yote (end of the road), bado kuna uamuzi na chaguo wawezafanya.

  Kila mwanamke mwenye ndoa ni mjane mtarajiwa hivyo hata kama una mume bado unahitaji kusoma na kuelewa na zaidi sana kujifahamu wewe ni nani na lolote laweza kutokea.

  Inawezekana unajisikia kila kitu hakiendi, unajiona maisha ni shagalabagala, asilimia 80 ya uwezo wako na nguvu zako unatumia kutafakari emotions zako zilivyoharibiwa, ndiyo maana unajisikia kuwa confused na pia umepoteza self esteem or self image, hujiamini tena, marafiki wote wanakukwepa na unajiona mpweke na depressed and stressed.

  Hata hivyo mara nyingi ukiachwa na mume marafiki wengi ulikuwa nao hukimbia na hilo linakufanya uwe mpweke na kukaliwa na msongo wa mawazo maana hata ndugu nao hawaoni thamani yako tena.
  Umeshaanza kupata matatizo ya ajira na fedha pia.

  Kumbuka kutoweka kwa mume wako hakujabadilisha kitu chochote ambacho Mungu alikuumba kuwa, thamani yako ipo palepale, kuachwa ni uamuzi wake si wako na hiyo haiwezi kuondoa kile unastahili kuwa (worth).
  Bado wewe ni mwanamke tofauti (unique), mzuri, mrembo, mwanamke mwenye malengo, mipango kamili, mwenye talents na mawazo mazuri ya kukufanya kuwa vyovyote unataka kuwa, wewe ni mbunifu, mwanamke mwenye ndoto na mwenye uwezo wa kufanya vitu vya uhakika na tofauti duniani.

  Nakutia moyo kwamba achana na mawazo yanayoongea ndani yako kwamba
  “Huna lolote, maisha kwisha, maisha hayana maana tena, hakuna mtu anakujali tena, unataka kukata tama”

  Anza kuchukua hatua madhubuti kuwa na uamauzi mpya ili uweze kukua na kuendelea kusonga mbele katika mwelekeo sahihi na halisi kwa furaha na ujasiri.
  “Hakuna mtu anaweza kuondoa furaha yako ndani yako hadi uamue mwenyewe”

  Jaribu kufanya yafuatayo:
  Pata ushauri kwa mtu unayemwamini kama vile mchungaji wako.
  Andika kwenye karatasi hisia na kila linalokusumbua hata kama utaandika kwa machozi utajisikia kupata relief.
  Kama huna ajira tafuta ajira/kazi yoyote ya kufanya hasa ile unapenda.
  Weka malengo – long term or short term na anza kuyatimiza.

  Kubali kwamba maisha yako ni changamoto na zitazame changamoto kwa jicho la opportunities kwako kukua kiimani na kupata new skills za maisha hata kuweza kufundisha wengine.
  Kubali kwamba huna mume kwa sasa na kwamba usijiingize haraha haraka kutafuta mwanaume mwingine kuziba pengo unaweza kuingia kwenye moto mkali zaidi.

  Katika jambo gumu kama hili Mungu anaweza kukurejesha kwenye matumaini na wewe kuwa strong baada ya kuvunjika moyo.

  Tambua kwamba Mungu anaweza kutenda kazi hata katika giza nene, anaweza kujibu maombi yako na kukurejesha katika maisha mapya pole pole na baadae kujenga msingi imara kimaisha na kiroho ili kuweza kugundua baraka, hazina mpya na hata wewe kuwa mtu mpya kabisa.

  Ubarikiwe na Bwana
   
 2. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Yamekupa yapi tena wewe??!!
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata mimi najiuliza, leo Mama mia kaamkia upande gani? Kama ni kuaga mwaka sawa. Lakini wengine tuna imani mbovu, kwamba mtu akifanya mambo mengi kuliko kawaida tena kwa muda mfupi; inawezekana anaaga!:rolleyes:
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,453
  Likes Received: 5,703
  Trophy Points: 280
  inawezekana anaaga!

  mmmmmh inalilllaahi rajuin??
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Kwani mwenyewe huoni hiyo speed inatisha!! Hakuna anayejua, hata wewe huwezijua. Inshallah tutavuka salama 2009!:rolleyes:
   
 6. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  mama Mia asante sana kwa kutukumbuka. Kweli message yako ni nziro. Ubarikiwe pia.
   
 7. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  ubarikiwe na Bwana
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  @mamamia
  asante kwa ushauri wako mzuri ila umeongelea kwa wanawake walioachwa je vip wanawake walowaacha waume zao hawa wanaume unawapaushauri gani nasubiri ushauri wako
   
 9. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35

  Haswaaaaa!
   
 10. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  H… Healthy, Hopeful, Humble, Humorous, Hummus eater

  A … Appreciative, Approachable, Activist for global peace & justice

  P … Peaceful, positive, …

  P … Passionate, practical, …

  Y… Youthful, yummy, …
   
Loading...