Ewe dada mpendwa usimwangalie mtu yeyote isipokuwa mumeo

Mohamedex121

JF-Expert Member
Jan 27, 2022
1,688
3,142
Dada yangu mpendwa! Kabla hujaolewa inaewezekana ulikwishachumbiwa na watu wengine. Posa za uchumba huu inawezekana zilitoka kwa watu wachamungu, matajiri, wasomi, wanaotoka koo kubwa , wenye sura nzuri na kadhalika ambao ungependa wakuoe.

Matarajio ya aina hiyo yalikuwa jambo la kawaida kabla ya kuolewa. Lakini sasa umechagua mwenzi wako na kuwekeana mkataba wa dhati naye kuwa wapenzi katika maisha yenu yote, hivyo, sahau kabisa yaliyopita.

Lazima uyaweke pembeni matamanio yako ya zamani na usahau ofa hizo za zamani. Usimfikirie mwamanume mwingine yeyote isipokuwa mumeo na utafute amani naye. Kama ukifanya vinginevyo, utajiweka katika hali ya mashaka.

Sasa basi, umekubali kuishi na mumeo, kwa nini wakati wote uendelee kuwatilia maanani wanaume wengine? Kwa nini umlinganishe mumeo na wanaume wengine? Unapata manufaa gani unapowatazama na kuwatilia maanani wanaume wengine zaidi ya kujiweka katika hali ya mateso yasiyo na mwisho na kusababisha upate maumivu makali ya akili?

Tambua kuwa yeyote anayeyaacha macho yake huru, kila mara atapata maumivu ya neva na atanasa kwenye mtego wa wivu wakati wote.

Je, kwa kuwatazama waume wengine, kuwatilia maanani na kuwalinganisha na mumeo, utampata mwanaume ambaye hana dosari unazozikimbia kwa mumeo?.

Unaweza kudhani kwamba labda mwamaume huyo mpya amekamilika kwa sababu huzijui dosari na kasoro zake. Utafikiria kuwa ndoa yako ina mushkeli, na fikira hii inaweza ikawafikisheni mahali penye mwisho wenye hatari.

Dada yangu mpendwa! Kama unataka ndoa ya kudumu daima milele, kama hutaki mateso ya kiakili, na kama unataka muendeshe maisha ya kawaida, basi acha kuwa mbinafsi na sahau hayo matarajio yako yasiyofaa.

Usiwapongeze wanaume wengine. Usimfikirie mwanaume yeyote isipokuwa mumeo. Usiendekeze fikira hizi:

‘Afadhali ningeolewa na fulani’
‘Ningependa mume wangu aonekane kama . . . . . .’
‘Natamani mume wangu angefanya kazi ya. . .. . . . . .’
‘Natamaani….. Natamaani……. Natamaani….’

Kwa nini ujipre kifungo kwa kuendekeza mawazo hayo? Kwa nini utibue misingi ya ndoa yako? Kama lolote kati ya matakwa hayo yangefanikiwa kwa kweli, ungejuaje kwamba ungefanikiwa kuridhika zaidi?

Unao uhakika gani kwamba wake za waume hao unaofikiria kuwa ‘hawana dosari wanaridhishwa nao?

Dada yangu mpendwa! Kama mumeo anashuku kwamba unaonesha kuvutiwa na wanaume wengine, atakata tamaa na kuacha kuvutiwa na wewe. Usitaniane na wanaume wengine au kufuatana nao. Wanaume ni wepesi kuhisi kiasi kwamba hawawezi hata kumvumilia mke anayeonekana kuvutiwa na picha ya mwanaume mwingine.

Waleykum Salam
1699780419369.jpg
 
View attachment 2811365
anaweza asimwangalie mwanamume mwigine lakini yeye akaonwa na kutizamwa mathalan akiwa kazini na akakubali kuonekana
 
Mkuu wanakuskia basi?Yaani kinaingilia huku kinatokea kule,nao wanataka Haki zotee tulizokuwa tunapata zamani,kifupi Wanaume tujiandae kisaikolojia
 
MaashaAllah, ujumbe mzuri sana kwa sisi waislam, Allah ajaalie tuwe hivi kwa waume zetu

TANBIHI
Na wao wanaume wafate vile dini inasema, wawajibike,wawajali na kuwathamini wake zao, wakifanya hivyo hayo ya juu yote kutekelezeka ni rahisi sana
 
Wakisahau tunaendelea Kuwa kumbusha. Maana binadamu tumeumbwa kusahau
 
Hivi nyi mijitu mna shida gani hamsikiiiii tumekubaliana kwa sauti nguvu moja .haya hima himaaaaaa
Wote: KATAAA NDOA
 
MaashaAllah, ujumbe mzuri sana kwa sisi waislam, Allah ajaalie tuwe hivi kwa waume zetu

TANBIHI
Na wao wanaume wafate vile dini inasema, wawajibike,wawajali na kuwathamini wake zao, wakifanya hivyo hayo ya juu yote kutekelezeka ni rahisi sana
Ameen . Inshallah nasi wanaume tutajitahidi Katika wajibu wetu kwenye ndoa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom