Ushawahi fikiria hili na wewe?

LINCO

Member
Dec 16, 2015
34
13
Kuwa Rubani wa Ndege haimaanishi ndio atakuwa Rubani wa Ndoa,...Unaweza kuwa Mwanajeshi tena Brigedia lakini kwenye Ndoa ukawa Kuruta��.....Mwanasheria anaweza kusimama kwenye Chamber kwa ustadi lakini kusimama ndani ya ndoa ni zaidi ya Extended Jurisdiction!

Hizi ni ndoto tu! Na Matamanio....lakini Kiuhalisia Mke au Mume Bora huibuka kama Uyoga, naweza Leo nikawa na ndoto ya kumuoa Miss World lakini nikaishia kudondokea Katika Penzi zito la Binti Afisa wanyamapori Kitalu cha Kutunza NGIRI kule Mikumi����

Mapenzi sio Mchezo....Maprofesa wanakuna Vipara...Formula hakuna!..once U fall in Love heshimu hisia,.....Kijana unaweza Tamani kumuoa Mrembo Engineer tena under eighteen lakini ukaishia kupeleka Mahari kwa wazazi wa Msanii Bibi Cheka!,

Wapo warembo waowahi kutamba kwamba watolewa na Vijana handsome na ma-tall lakini wakaja kuzama kwenye mapenzi mazito na vibabu vistaafu Tanganyika Packers 1992,..Babu ngozi imekauka Busu mpaka apakwe Mayyonise.���� ....MAPENZI KWELI HISIA!...Huwezi jua!
 
Umenena Mkuu,haya mapenzi ni habari tatanishi kwa dunia tunayoiishi leo,usije tamka eti mi siwezi kuoa masikini/tajiri wakati hujui kesho yako ipoje na usiishi kimazoea. Hata wanawake machizi barabarani nao wana watoto na walipendwa hvohvo ktk uchizi wao lakini pia wanapenda,SO BE CARE THERE IS NO LIFE FORMULA
 
Its true . Mimi nilidhani na kuwaza kuwa one day nitaolewa na msukuma mkokoteni ( because of the True Love , I craved ) but it turned out different... Soon nakuja kuolewa na...... Aisee acha Mungu aitwe Mungu... God is the only one who knows about our future .. Glory unto Him.. Thanks..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom