Ushauri wenye gharama kwa Dr.Wilbroad slaa.

Ushauri wenye gharama kwa Dr.Wilbroad slaa.

ngungwangungwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
649
Reaction score
583
Dr. Ww ni kati ya watu wachache nnaowaheshimu sana hapa nchini.

Naamini toka moyoni kabisaa kuwa kile unachopigania ktk harakati zako ni mguso ulionao wa maisha yetu na vizazi vijavyo. Natapenda kukupa ushauri ambao pengine inaweza kukuwia vigumu kuuamua! Kutokana na hali halisi inayoendelea ktk Bunge LA katiba,ni dhahiri hakuna tena katiba mpya bali ni katiba ya ccm. Hakuna tena uwezekano wa upinzani kuleta mabadiliko yoyote ktk mambo yote yaliyoletwa na ccm.

Wabunge wetu wametusariti! Tuliwashauri wajitoe mapema lkn wakashindwa kuacha posho ya laki 3. Kwa maantiki hiyo,nakusihi UNG'ATUKE nafasi yako ya juu ya Chadema! Hii itakuongezea heshima kubwa miongoni mwa jamii. Baada ya bunge la katiba,ni vigumu sana kwa upinzani kuaminika kwa wananchi,naamini utapima kwa kuangalia uzito wa heshima yako na matokeo ya kura za Jana ktk kuamua namna kupiga kura.

Nawasilisha..!
 
Kwani yeye hataki hizo Laki tatu/day?
 
Kwa nini Dkt Slaa tu? Je, unashauri ang'atuke kwenye siasa, au ajing'atue Ukatibu Mkuu wa Chadema?
 
Kwa nini Dkt Slaa tu? Je, unashauri ang'atuke kwenye siasa, au ajing'atue Ukatibu Mkuu wa Chadema?
Me namshauri ajitoe ang'atuke cheo chake. Anaweza kubaki kwenye siasa km mshauri tu. Nahisi kutakuwa na matokeo mabaya zaidi mbeleni kutokana na udhaifu waliouonyesha wabunge wetu. Njia pekee ya kumfanya aendelee kuonekana lulu,ni kujitoa tu!
 
Uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze ni teke la mwisho la marehemu mtarajiwa Chadema! Kushindwa kwa Chadema Chalinze itakua ndio msumari wa mwisho kwenye jeneza la Chadema baada ya ile misumari ya awali ya CHOPA 3,KATA TATU NA ULE WA KALENGA!

Pamoja na kupigana kwao kufa na kupona ili wajinasue na balaa hili, juhudi zao zimekua sawa na kujaribu kumwongezea damu marehemu!!
RIP CHADEMA
 
Slaa nae ni mjumbe?.
Mimi nilijua slaa yuko kijijini kwao ana cooldown baada ya kipigo cha Lukaya,..oh sorry i mean kalenga?
Yeye siyo mjumbe,lkn kitendo cha taasisi anayoiongoza ku-fail,inatosha kumfanya atafakari!
 
Dr. Ww ni kati ya watu wachache nnaowaheshimu sana hapa nchini. Naamini toka moyoni kabisaa kuwa kile unachopigania ktk harakati zako ni mguso ulionao wa maisha yetu na vizazi vijavyo. Natapenda kukupa ushauri ambao pengine inaweza kukuwia vigumu kuuamua! Kutokana na hali halisi inayoendelea ktk Bunge LA katiba,ni dhahiri hakuna tena katiba mpya bali ni katiba ya ccm. Hakuna tena uwezekano wa upinzani kuleta mabadiliko yoyote ktk mambo yote yaliyoletwa na ccm. Wabunge wetu wametusariti! Tuliwashauri wajitoe mapema lkn wakashindwa kuacha posho ya laki 3. Kwa maantiki hiyo,nakusihi UNG'ATUKE nafasi yako ya juu ya Chadema! Hii itakuongezea heshima kubwa miongoni mwa jamii. Baada ya bunge la katiba,ni vigumu sana kwa upinzani kuaminika kwa wananchi,naamini utapima kwa kuangalia uzito wa heshima yako na matokeo ya kura za Jana ktk kuamua namna kupiga kura. Nawasilisha..!

Kung'atuka kwake kutaleta tija gani!? hebu nishawishi hapo labda ntakuelewa.
 
Yeye siyo mjumbe,lkn kitendo cha taasisi anayoiongoza ku-fail,inatosha kumfanya atafakari!

Kwa maana hiyo hata Kinana, Seif Shariff Hamad, na wale wa Nccr, Tlp, Udp nao wajiuzulu!? Mbona ushauri wako umepindia upande mmoja, utaepuka vipi kutiliwa shaka kuwa una agenda yako ya siri katika pendekezo lako hili.!?
 
Uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze ni teke la mwisho la marehemu mtarajiwa Chadema! Kushindwa kwa Chadema Chalinze itakua ndio msumari wa mwisho kwenye jeneza la Chadema baada ya ile misumari ya awali ya CHOPA 3,KATA TATU NA ULE WA KALENGA!

Pamoja na kupigana kwao kufa na kupona ili wajinasue na balaa hili, juhudi zao zimekua sawa na kujaribu kumwongezea damu marehemu!!
RIP CHADEMA

nape usilipe hii thread huyu juha amepest.
 
Kwa maana hiyo hata Kinana, Seif Shariff Hamad, na wale wa Nccr, Tlp, Udp nao wajiuzulu!? Mbona ushauri wako umepindia upande mmoja, utaepuka vipi kutiliwa shaka kuwa una agenda yako ya siri katika pendekezo lako hili.!?
Una hoja ya msingi,kinana hawezi kung'atuka na sababu ni moja tu ccm wamefanikiwa kwa karibu kila kitu ktk bunge la katiba. Cuf kwa upande wao,sina tatizo kwa sababu chama chao bado kimeimarika upande wa Zanzibar ambako ndiyo kina nguvu kubwa! Na huenda km mfumo wa serikali 3 hautapita,cuf kwa upande wa Zanzibar hawatakubali! Kuhusu chadema,ndo chama Kikuu cha upinzani,na suala la katiba lilikuwa ktk ilani yao! Kitendo cha kuendelea kukubali hoja za ccm ni kuonyesha kushindwa! Ndo maana nikamshauri km kiongozi mkuu wa,taasisi hiyo kubwa hapa nchini,ang'atuke ili aendelee kuaminika!
 
Ujasiri huo hana,ujsasiri wake uko kwenye yale mambo yake tu basi.
 
Slaa angerudi kwenye kanisa ampigie magoti mungu.
 
Atoke halafu afe njaa. We muanzisha mada vipi. Hiyo nafasi ndio inayo mlisha mzee slaa na watoto wake halafu unamshauri aiachie,utamlisha wewe?
 
Una hoja ya msingi,kinana hawezi kung'atuka na sababu ni moja tu ccm wamefanikiwa kwa karibu kila kitu ktk bunge la katiba. Cuf kwa upande wao,sina tatizo kwa sababu chama chao bado kimeimarika upande wa Zanzibar ambako ndiyo kina nguvu kubwa! Na huenda km mfumo wa serikali 3 hautapita,cuf kwa upande wa Zanzibar hawatakubali! Kuhusu chadema,ndo chama Kikuu cha upinzani,na suala la katiba lilikuwa ktk ilani yao! Kitendo cha kuendelea kukubali hoja za ccm ni kuonyesha kushindwa! Ndo maana nikamshauri km kiongozi mkuu wa,taasisi hiyo kubwa hapa nchini,ang'atuke ili aendelee kuaminika!

Na unawazungumziaje wale waliomo mule kuwakilisha makundi kama ya kidini, elimu n.k, nao wajiudhulu nyadhifa zao kwa kuruhusu mjadala kutekwa zaidi na wanasiasa!?
 
Unajua wewe jamaa hueleweki,Kwahiyo Dr akijiuzulu ndipo tutapata kila kitu kinachopendekezwa na upande wa upinzani? Elewa hata kama Chadema na upinzani wote wangekuwa na mapendekezo mazuri kiasi gani kama haya akisi maslah ya ccm hayawezi kupita kamwe. Halafu vipi umshauri Dr ang'atuke nafasi yake ya chama wakati mle ndani (bungeni) yumo Mwkt Mwanasheria na Mkurugenzi wa habari na uenezi wewe unadili na mtu aliye nje na tukio husika!

Je sikweli kwamba wewe umebeba ajenda zako za siri kuhusu Dr Slaa.

Eti ukishauri wajitoe halafu unasema wanabaki kwasababu ya laki tatu! Hizo ni propaganda rahisi sana utawakamata misukule ya Lb7 siyo jamii ya watu wanaojitambua.

Huwezi kulipigania jambo kwa zaidi ya miaka ishirini then uje ujitoe kwa visababu visivyo jaa hata kisoda. Jiulize mle ndani kunawatu wote wanaoheshimika kuliko wewe kama Lipumba,Mbatia,Mbowe na viongozi wa dini lakini hawajaona sababu ya msingi ya kujitoa kwasababu fursa kama hizo haziji mara mbili.

Elewa kama unavyosema hakuna mwanasiasa wa upinzani anaye heshimika kimataifa na kitaifa kama Dr Slaa na kamwe heshima yake haiwezi kushuka eti kwasababu hajajiuzulu kwa kutopitishwa kwa baadhi ya mapendekezo yaliyo kuwa yakipiganiwa na upinzani Bungeni. Yeyo mwenye mawazo kama yako ni wazo anafikiri kwa kiungo cha meya wa Dareslaam.

BACK TANGANYIKA
 
Lengo hapa ni kupata wachangiaji kwa kumtaja Dr.Wilbrod Peter Slaa,kipenzi cha watanzania.Hakuna lingine wala mantiki kwenye uzi huu.Na kweli umetupata. Tutamtetea Dr. popote na wakati wowote
 
Back
Top Bottom