Asante sanaPole, unaishi wapi? Kama unaweza hama wilaya/mkoa kaanze maisha sehemu nyingine/Mpya.
Huko utafute mtu mmoja tu wakukusaidia katika biashara mfano kukutafutia vijana wa kuwaajiri katika bodaboda zako, Mtu huyu mtafutie kanisani/msikitini. Sio akusaidie biashara bali awe mwenyeji wako.
Anza maisha mapya, focus, tafuta mahusiano na mwanamke (hili lichukue muda kidogo na usihangaike na madada wa mjini), nikisema mjini simaanishi ukatafute kijijini namaanisha kuachana na wanawake wenye umjini mwingi upate mtu ambaye ni family oriented, Kila la heri na kwa hakika nitakuweka kwa maombi.
🙏Asante sana mkubwa nimekuelewa
Hehehehe[emoji16][emoji16]Za kusikia na KUAMBIWA CHANGANYA na zako
Hahaha abadili stareheUmesema kila siku lazima upoteze zaidi ya laki na nusu na umesema unakunywa kila siku iwe mchana au usiku. That means kwa mwenzi unatakiwa unywe si chini ya 4.5M ila umesema unakunywa zaidi ya 2.5M. Hapo umefanya overestimation kidogo ila kwa mwendo huu na umri wako kama unakunywa hivi hutoboi hata 25.
Unataka msaada gani wa kuacha au kupunguza. Mimi nilijaribu kunywa bia last week ikanishinda hata nusu sikufika. Mara ya mwisho kunywa nilikuwa form 3 mpaka hiyo juzi nilipojaribu kumbe pombe nimezisahau.
Kwanza achana na kampani yako ya pombe. Mwaka 2022 cut them off bakiza mahusiano ya kutafuta pesa.
Kuna mama mmoja yeye mumewe alikuwa anakunywa mataputapu.. Yaani ile ya kupindukia.. Watu wakamshauri jambo huyo mama. Akamuwekea mumewe vitoto vya panya kwenye kile chombo cha kunywea..!!! Ile anafika mwisho mwishoni jamaa akakutana na vitoto vya panya vimekufa havina hata manyoya.. Bado vyekundu.. MWANA ALITAPIKA KUPINDUKIA NA NDO UKAWA MWISHO WAKE KUNYWA POMBEHabarini humu wakuu
Nambeni ushauli kwa mazingira ninayopitia mdogo wenu wakuu
[emoji115] Mimi nikijana mdogo kabisa miaka 22 tangu nilipomaliza sec. nilianza kujitafutia maisha mwenyew namshukuru mungu alinibariki sana nikawa nipo vizur kwenye maisha kiuchumi, kufika mpaka miaka nikawa namiliki pikipik nyingi tu nikafanikiwa kununua kiwanja, mwaka jana nikannua nagari usafiri wangu.
Hapo niliponunua gari ndipo maisha yakaanza kuchange mimi nikawa mtu wa kulewa muda wote sio usiku sio mchana wala asubuhi, nikienda bar kama nina laki namaliza yote, uchimi wangu kwasasa unaenda kupotea kila ck lazima ninywe kila ck napoteza zaidi ya laki nanusu bar, ni mwaka sasa umepita kwa mwezi napoteza zaidi mil. 2 nazaidi kwenye pombe
Naombeni ushauli ndugu zangu, usiku nikilala bila kunywa silali hayo mateso ninayopata, mandoto ya ajabu kukabwa usiku pia nikinywa usiku nikishtuka pombe zimeisha huwa najilaumu sana kwann nafanya mambo hayo Hadi nahisi kujiuwa, lakini nikiamka tuh asubuhi kila kitu nimesahau naamkia kwenye mipombe.
Naombeni mawazo yenu wakubwa zangu, nimeyachoka haya maisha
Pombe za laki ni zile za Mupe Muruke😅 mkikaa kilinge cha mtu 4 au 5 lazma uzungushe round!Hizo pombe za laki kwa siku mnakunywaje jamani?
Mbona me nikienda sehemu nakunywa 3-4 naondoka
Eeh kwa mtu wa kupita pita bar lazma uelewe utaratibuYah mkuu kumbe unajua
Kwa 1500/- huwezi fikisha kiasi hicho cha pesa na huku ukiwa peke yako.. Huyu labda zile za akina Absolute VODKA, ABSOLUTE KURANT na hapo anahudumia na marafiki na michepuko yao..Hizo pombe za laki kwa siku mnakunywaje jamani?
Mbona me nikienda sehemu nakunywa 3-4 naondoka