Ushauri wenu: Nilimuahidi, nifanyaje?

Miaka mi4 umemtumia weeew mpaka uliposema fyokonyoko naona mwingine,huoni aibu? Umechezea hisia za mwenzio na mwili wake pia for 4 years then unakuja kulalamika anadai ulichomuahidi. Mlipe asepe faster we chalii niadje buana
 
We timiza, kama ulikuwa na nia kwanini hukutimiza kabla hajaolewa? Umesubiri kaolewa ili upate kisingizio!!!
 
Achana nae broo...hiyo ni hatari licha ya kuwa,ulimuahid...kumfungulia saloon kwanza kutaendeleza enzi lenu istoshe ameshaolewa
Ataachana naye vipi wakati anamfuata mpaka ofisini? Bro umesema una uwezo, lipa deni block mawasiliano. Akikufuata tena hapo anataka mengine.
 
Kisheria hakufanyi chochote maana mkataba wenu hauna mashahidi.Ni sawa na unapomuahidi mkeo kuwa mwakani utamnunulia gari usipofanikiwa hawezi kukufanya lolote.Ama ukaenda kanisani pesa unayo ila ukagoma kutoa sadaka hakuna kosa kwa kuwa hakuna mkataba na kama mkataba haupo basi hakuna sheria na kama sheria haipo basi uko huru. Ila nakushauri umwite sehemu mkae faragha muongee kwa kirefu mpe kilichopo then kingine mpigane tarehe ila unaonekana bado unamtafuna tu na hana ujanja amaa kweli mapenzi noma.
 
Hivi wewe kama mke wako aliahidiwa huko nyuma na jamaa utakubali huyo jamaa atimize ahadi aliyo muahidi mke wako.
Mfano tu.

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
 
Mpe 2m yake yani ukae nae 4yrs na ahadi usitimize sio sawa kabisa
 

Kama ni hivyo timiza ahadi! Mtie noti yake atajua mwenyewe afungue saluni Au akanunue maandazi, baada ya hapo mwambie asikuzoee utamuitia mwizi akija ofisini Kwako.
 
Mfungulie saloon acha visingizio, we si uliahidi ukiwa na mke sasa mtimizie nae akiwa na mme.....
Wakati unaahidi huku ukiwa na ndoa we hukuangalia mustakabali wa ndoa yako?
 
Haikuwa mipango ya Mungu
presumption of marriage 2yrs amlipe miaka yote si amempotezea mda? Na kusababisha kuolewa na mwanaume asiempenda?

Wewe uoni ameolewa kwa stress?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…