Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu

Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu

Una diploma ya ualimu au wamekuajiri kwa degree ya BBA???

Umeuliza diploma ya ualimu wanalipwa shs ngapi??? Naona umeandika 500K

Maisha ni kutake risk fanya maamuzi yenye maslahi na Wewe usijekuingia kibano ukajuta hata kwanini ulikubali kwenda huko halmashauri
 
Piga chini hiyo kazi ya binafsi ,nenda serikalin karipoti Fanya kazi mwaka mmoja ingia benki chukua mkopo wekeza kwenye unachoona kitakufaaa .kazi za private zina stress sanaaa inaweza isha kesho na pia unatumika sanaa.

serikalin raha yake kama una akili mda upo wa kufanya mambo yako tena kazi yenyewe ualimu ni rahisi sanaa unashika somo lako unafundisha miaka yote hilo hilo inafika mda unakuwa kama unaimba pambiao tu maana hutumii nguvu kufundisha ,kutunga mitihan na kujua vijana wako ufanye vipi wafaulu

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Mazingira pia ni changamoto unaweza pewa ajira mkoa wa mbali na mazingira ya vijijini sana hii imezima ndoto za wengi sana .

Nashauri aangaze plan zake kama ataweza kuwa makini na uhasibu na kupata mtaji then atatoboa tu.
 


Kuna thread yangu naomba ushauri namna ya kurudisha check No serikalini nilisomea Engineering nikasema Mimi lazima Niwe tajiri kutoka familia masikini nikakataa ajira ya ualimu mwaka 2016, nikafanya kazi kwenye taasisi binafsi zinazolipa vizuri, nikajenga na nyumba freshi kumbe nilitakiwa niwekeze hata kwenye biashara Mimi sikufanya hivyo mkataba ukaisha life likanipiga kisawasawa.
Zilipotoka ajira hizi ikabidi nirudi kuomba tena na jina limetoka hapa siangalii nyuma naenda kuripoti nikapambane kurudisha check No.
Pamoja na engineering yangu nimeona bora nikawe MWALIMU tu na maisha yaendelee.
Kazi za binafsi zina changamoto sana zipo results oriented ukizingua tu huna kazi,majungu baina ya wafanyakazi nayo ni shida private wakiona unapiga hela tu utachongewa kwa boss utimuliwe.
Hapo Ni sawa na kutema big g kwa karanga za kuonjeshwa.
Fanya maamuzi usije kujutia.
Nimekushauri kutokana na yaliyonikuta.


Ulikuwa mjinga na mzembe
 
Back
Top Bottom