Ushauri wenu ndugu zangu pombe inanitesa

Ushauri wenu ndugu zangu pombe inanitesa

Naomba more information dada
Umelogwa sas huyu atakusaidia kwanza anajua kuangalia vyema Nini kinakusumbua halafu anasema ukweli Hana tamaa ya hela .

Jingine nimempata humu nilipokuwa na shida zangu kamjaribu ikitiki utaniambia ila Kwangu huyu ni the best aisee .
 
Watu kibao watakupa ushauri lakn u gotta know among them nan ana real life experience ya hyo kitu.
Il be honest with u, mimi nlikua chapombe wa kutupwa. Leo nna miaka 3 sober na hata ile kiu imeanza kupotea taratibu.
Kuacha haikua easy wala haikua na maushauri mob n.k., ni event ilitokea tu.
Tuluenda kulewa na masela af nlikua na baby mama (yeye hanywi), nlipoingia autopilot (wanywaji wanajua, ile mida haujitambui lakn unapiga matukio matokeo asubuh).
Asubuh nmeamka nkapewa mkanda wa matatizo nliofanya mixer ugomvi mkubwa na wife, wooi, nkasema sinywi tena! Kuanzia hapo sijawahi kuonja tena.
So kuhusu kuteseka sijui kuacha, hainaga ushauri. Utaamka siku moja utatafakari ulikotoka na unapoenda, utaacha!
 
Ukishaamuwa wewe mwenyewe basi utaacha. Vinginevyo ni uongo.
 
Wadau habari za muda huu,

Nianze kwa kusema mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30, nafanya kazi katika kampuni fulani mshahara laki 3, bado naishi kwa wazazi napanga kutoka lakini nashindwa.

Kikubwa ni unywaji wa pombe, yaani kila nikipokea kamshahara akili inanituma kunywa tuu na nikinywa napoteza mali zangu, Pesa, simu, viatu n.k.

Ushauri tafadhali hali ni mbaya. Nini nikifanye kuepukana na hali hii, maana binafsi siipendi ila najikuta tayari nipo huko na majuto ni baada ya pombe kuisha kichwani?

NB: Nimeandika kwa stress mno maana hapa nilipo nimeshapoteza laki 2 jana usiku.

Ahsanteni.
Pole, cha muhimu amua wewe kama wewe kwamba naacha pombe. Jaribu kubadilisha marafiki, jaribi kubadilisha mind set yako, Jizoeshe kuacha vijiwe vya kukushawishi kunywa, zoea vijiwe kama vya vya mazoezi, fatilia mipira either uanjani au TV watching, jioni anza kukaa kwenye kahawa draft, kwenye vioskbvya Maziwa na juice, taratibu utajikuta umeacha. Muhimu Marafiki walevi wpukana nao kabisa
 
ishi peponi ukiwa hai enjoi acha kuteseka na usiaeme pombe inakutesa jitambue wewe ni zaidi ya pombe
 
(Sina uandishi wala usimulizi mzuri)

Binafsi tangu mwanzo nilitumikishw katika ngono,
Nimeishi muda mrefu nikiwa na mgogoro mkubwa sana wa nafsi bila kujua chanzo ni nini!, mitafaruku isiyoisha, mahusiano mabaya na watu wote hadi ndugu,

Shuleni sikufanya vizuri,
Kazini nimeteseka sana,
Mahusiano mabovu, mikosi kila leo,

Mambo yalivyozidi kuniharibikia sana kutokana na tabia ya uzinzi huku sielewi chanzo ni nini,
Nikajikuta naingia kwenye pombe,

Yaani nikajikuta nna mambo mawili yanayonitumikisha, uzinzi na pombe,
Kiukweli nimeteseka sana bila kujua,
Pesa hazikai, biashara nilizoanzisha zilikufa zote ndani ya muda mfupi,

Uharibifu ulionipata ni mwingi sana,
Nilifedheheka sana ndugu zangu maana hata sikuweza kufanikisha jambo lolote la maana.
Nilianza kutembea kwa waganga kwamba nimerogwa ndio maana mikosi hainiishi,

Nikauliza hadi magwiji wa waganga humu,
Kote nikaenda, niliishia Kuliwa na kupoteza pesa, bila msaada hata tone,
Wazo likaniijia niende kwa wataalam wa nyumbani nilipozaliwa,

Nikajipanga nikaenda nyumbani, ingawa wazazi wote walishalala, ila niliamini Kuna msaada,
Ile nimefika nyumbani, nikasikia sauti ikiniambia!

"mateso yangu yote chanzo ni uzinzi"

Ingawa nilienda kwa mtaalam wa huko nyumbani lakini hakuwa na jipya lolote.

Kurudi nikaanza kufanyia kazi kuachana kabisa na wanawake nibaki na mke tu,

Ingawa mwanzoni ilikuw ngumu, hadi nikajikuta narudi kwa mchepuko wangu niliokuw nauamin kuwa huenda una kismati,

lakini cha kushangaza niliishia kupoteza laki 5 bila kufahamu, plus fedheha nyingi kwenye pombe.

Tangia hapo nikaacha uzinzi na tatizo la pombe nalo limekata,

Namshukuru Mungu, mdogomdogo naanza kuona mkono wake.
 
Umelogwa sas huyu atakusaidia kwanza anajua kuangalia vyema Nini kinakusumbua halafu anasema ukweli Hana tamaa ya hela .

Jingine nimempata humu nilipokuwa na shida zangu kamjaribu ikitiki utaniambia ila Kwangu huyu ni the best aisee .
Nilikuchek pm naona umefunga naomba nitext tafadhali mana hili kwangu ni tatizo
 
Chai ya maziwa etiee😂
Unacheza na addiction wewe,kuna jamaa yangu anapokea 400000 kwa mwezi,lakini baada ya siku mbili kashabetia zote.
Addiction inakutaka utatue KIU muda huo kwa uwezo ulionao.
 
Back
Top Bottom