Wadau habari za muda huu,
Nianze kwa kusema mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30, nafanya kazi katika kampuni fulani mshahara laki 3, bado naishi kwa wazazi napanga kutoka lakini nashindwa.
Kikubwa ni unywaji wa pombe, yaani kila nikipokea kamshahara akili inanituma kunywa tuu na nikinywa napoteza mali zangu, Pesa, simu, viatu n.k.
Ushauri tafadhali hali ni mbaya. Nini nikifanye kuepukana na hali hii, maana binafsi siipendi ila najikuta tayari nipo huko na majuto ni baada ya pombe kuisha kichwani?
NB: Nimeandika kwa stress mno maana hapa nilipo nimeshapoteza laki 2 jana usiku.
Ahsanteni.