GalileiGalileo
Senior Member
- Nov 19, 2011
- 165
- 225
Iko hivi:
Nina mpenzi wangu wa siku nyingi kama miaka 7 hivi. Hivi karibuni mapenzi yalianza kupoa na nikiri wazi kuwa mimi ndiye haswa niliyekinai na kumueleza mwenzangu kwa maneno hata kwa kumuonesha kwa vitendo. Hapa na pale nikaopoa Jimama na niseme wazi kuwa kilichonivutia kwake haswa ni huduma anazonipa kwa maana ya huduma zaidi ya mapenzi. Mpenzi wangu wa zamani akagundua hilo lakini hakukata tamaa hivyo tukawa tunaendelea kidogo kidogo na mahusiano yetu ambayo hata huyo Jimama alikuwa anajua kwani alinikuta nikiwa naye na kuahidi kuwa atamuheshimu.
Baada ya kama mwaka mzima kupita tukiendelea na mfumo huu wa maisha, nagundua kuwa huyu Jimama naye ana mzee wake tena wa siku nyingi tu ila anakomaa kuwa huyo anampa kampani ya kiuchumi tu ila Mimi ndio roho yake. Kwa kweli hali hii ilinifanya nipunguze mapenzi kwake kwa kiasi fulani. Yeye ameshindwa kukubaliana nayo na moja ya kitu anachodhani kimesababisha kuyumba kwa penzi letu ni yule mpenzi wangu wa tangu zamani akidhani kuwa mapenzi yetu yameimarika.
Balaa!
Ameamua kumfanyia jambo la ajabu sana mpenzi wangu huyu wa toka enzi kwa kununua wahuni na mmoja wapo kujifanya kuwa anampenda na anataka kumuoa. Huyu muhuni amewezeshwa gari, pesa na kujifanya ni afisa fulani wa Serikali. Huyu mpenzi wangu wa toka enzi kwa kutojua na kwa kuamini kuwa sasa amepata mwanaume atakayempenda kwa dhati akaingia mkenge na siku ya siku walipokuwa wanafanya tendo amejikuta amerekodiwa na video/ picha kusambazwa hadi kunifikia Mimi. Lengo kuu hapa nione kuwa nang'ang'ania mwanamke ambaye ni Malaya kama walivyo Malaya wengine. Hili limenisikitisha sana ukizingatia kuwa kwa sasa huyo binti amepatwa na shock mbaya hadi kulazwa hospitali.
Hapa nilipo nimejawa na huzuni, huruma, hasira na hali ya kuchanganyikiwa kiasi kwamba nafikiria kumfanyia huyu mama jambo baya!
Ushauri wenu tafadhali!