musa abel jr
Member
- Oct 12, 2016
- 39
- 57
Habari nianze kwa kuwapa pole ya majukumu ya kila siku,
Naombeni ushauri ndugu zangu mimi ni kijana nimemaliza chuo 2019 katika kada fulani ya afya na nikabahatika kufaulu na nimesomeshwa na kaka yangu, sasa baada ya kumaliza chuo nikarudi nyumbani na kuanza kutafuta ajira angalau nipate hela ya kununua boxer.
Sasa bwana changamoto ikaja nimeoata ajira ya kwanza kwa mtu binafsi nikaenda mpaka kuonana naye na nikafanya vitu kadhaa sasa kaka yangu aliyenisomesha akasema rudi nyumbani huo mshahara haufai, nikarudi tu nyumbani nikaanza kutafuta nyingne nikapata huko Tarime. Nikatakiwa kwenda lakini sababu zikawa nyingi kutoka kwa huyo kaka angu na mama angu, ikapita hiyo
Sasa wiki hii nimepata ajira nyingne huko Lindi nikatakiwa kwenda lkn kaka yangu akanambia niongee na mama angu, nikaongea naye mama akarudi kuongea na kaka na kuja kunipa jibu kuwa kaka yako kasema huko kuna ugaidi mwingi ni Kusini na pia yeye anataka nifanye kazi katika hospital ili nijenge CV nzuri hata kama kwa kujitolea na mama angu pia anaafiki kwa hilo.
Kumbuka hapa nyumbani mimi ndio kama mfanyakazi wao yaani kuna kuku mimi ndo mlishaji, kuna gari hapa mimi ndio muendeshaji na kutumwa sehemu mbali mbali.
Sasa naomba ushauri juu ya haya...
1. Nifanyeje ili nitoke nyumbani?
2. Je, hawa ambao ni kama wazazi wangu wana nia njema na maisha yangu?
3. Je, nitakaa nyumbani mpaka lini?
4. Na nitapata vipi CV kwa kukaa nyumbani muda mrefu
5. Kwann wananifanyia hivi?
USHAURI WENU NI MUHIMU NDUGU