USHAURI WENU: Ameshaolewa lakini bado ananitaka, nifanyeje?

USHAURI WENU: Ameshaolewa lakini bado ananitaka, nifanyeje?

Joined
Nov 13, 2013
Posts
63
Reaction score
5
Hbr za leo ndg zangu wana JF!
Nilikuwa na mpenzi ambaye tulikuwa ktk uhusiano kwa takribani miaka 5 hivi. Nilkuwa tayari nshakuwa na maamuzi ya kumfanya kuwa mke wangu kwa kufuata taratibu zote mara tu baada ya kumaliza masomo yangu 2009.Mwaka huo ho(2009) niligundua alikuwa kwenye mahusiano na mtu mwingine.Nikashindwa kustahimili na kusitisha mahusiano naye! Mara baada ya hapo, aligeuka kuwa kama adui mkubwa kwangu kwa kunitukana matusi mengi ambayo kimsingi sipaswi kuyaweka wazi kwa ajili ya kutunza maadili, yalikuwa ni mazito sana.
Ndani ya mwaka huo huo, mwanamke huyo alienda kuungana na huyo mwanamme wake mpya na kuanza maisha kama mume na mke. Cha ajabu ndudu zanguni ni kwamba, mimi nilifuta namba zake zote na sikutaka kuwasiliana naye tena. Lakini alianza kunitumia msg za nakumic,am sorry swt, ntakupenda daima, najutia maamuzi yangu nk.Baadaye alianza kunipigia cm akitaka turudiane.
HIVI KARIBUNI ALINIPIGIA CM KUNISALIMIA, SIKU 2 BAADAYE NIKAPOKEA SMS KUPITIA CM YAKE IKISEMA: "sitaki uwe unaongea na mke wangu".
Mnanishaurije juu ya mwanamke huyo? Me tayari nina mke wangu na nampenda kweli!
 
Achana na huyo kigagula........ asikuharibie ndoa yako Mkuu! Akikutumia texts tafuta no. ya mume wake mtaarifu na muonyeshe texts hizo kwa uthibitisho
 
Hapo napo unataka ushauri mkuu? Mrudie uje kujuta zaidi ya mara ya kwanza. Piga chini huyo,mke wa mtu utampeleka wapi mkuu?
 
Mwenye macho haambiwi tazama...Wapo wengi tu wa jinsi hiyo, uamuzi unao mweyewe kuibomoa au kuijenga ndoa yako
 
Hapo Mkuu kuna kipi kilichobaki kushauriwa tena? au bado unataka kukumbukia yazamani? staki mwenzie basi kama ameomba msamaha basi msamehe na ndio mmeshamalizana tena au kuna ziada labda kwa upande wako hujamaliza kutoa dukuduku lako?
 
Fikiria mkeo angekua ana mawasiliano na ex wake..ungemshauri nn huyo ex wake?
 
hiyo hatari, lakini hukufafanua vyema Je huyo mwanamke ameolewa na huyo bwana au ni mahawara tu....
 
Kaa nae mbali huyo,atakuharibia bure mkuu,atahamishia stress zake kwako halafu ushindwe kuwajibika kwa mkeo
 
Hapo Mkuu kuna kipi kilichobaki kushauriwa tena? au bado unataka kukumbukia yazamani? staki mwenzie basi kama ameomba msamaha basi msamehe na ndio mmeshamalizana tena au kuna ziada labda kwa upande wako hujamaliza kutoa dukuduku lako?
Sikutaka kukumbukia ya zamani kabisa mkuu! Nlikuwa nshamsamehe ndio maana nikaanza pokea cm zake! Anavyozidi kuning'ang'ania ndio imenitsha! Nashukuru kwa ushauri wako!
 
Kuna mada nyingine ziko very obvious kiasi kwamba haina haja hata ya kuchangia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom