USHAURI: Wasemaji wa Polisi kuna la kujifunza hapa, mlisema Dkt. Shika si chochote si lolote ni wa kupuuzwa!

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
TUKIO LA DR. SHIKA
Dr. shika alishikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano kutokana na tukio la kuvuruga mnada wa nyumba za Lugumi, Ambapo pamoja mamlaka lililonayo jeshi lilijiridhisha paspo shaka yeyote na kutamkwa hadharani kwamba Dr. shika alikuwa si chochote.

DR. SHIKA ANENA
Dr shika kupitia vyombo mbalimbali kathibitisha wiki iliyopita kwamba tayali kapokea tone la kwanza la mabilion ya fedha kwa ushahidi na documents!
KAULI YA B.O.T
Msemaji wa B.O.T kakanusha kwamba Hawana taarifa zozote juu ya ujio wa pesa, na hawajapokea pesa yeyote kama ilivyoelezwa na dr. shika, kwahiyo taarifa za dr. shika zipuuzwe

JE, KUNA HAJA SASA DR.SHIKA ADHIBITIWE?
Ndiyo; Kutokana na sintofahamu na taharuki inayosababishwa na kauli za dr. shika;
ipo haja sasa Jeshi la polisi lipige marufuku kwa chombo chochote cha habari kurusha au kutangaza mahojiano yeyote ya Dr. shika.
 
dr shika namuona kama msaniii

anatumika kutuvuruga tu tusiongelee ya maana kama msamaha wa lulu
zile documents ni za uongo? wanahabari wamethibisha pia pesa zilifika BOT nao waongo? kama dr. shika ni muongo; kwanini jeshi lisiwakamate wanahabr wanaomhoji na kurusha taarifa?
 
Kuna bro wangu mmoja alikuwa tapeli maarufu sana, aliniambia kitu kimoja, mjini wajinga hawaishi

Yani umeamua kumuamini dk shika kabisa?upuuzi mimi huwa siamini mtu akisema mpaka nithibitishe kwa njia zangu, si quote mtu fulani kasema nini nitasema on my own experience...hapa ndio watu mnapotapeliwa
 
Ngoja tusubirie na ile sinema ya nabii tito!
Nabii akitoka sero atatuthibitishia zaidi yale aliyokuwa akihubiri...
 
Hata wewe huna tofauti na Dr. Shika!
 
Hata mimi nasema hizo ni kiki tu. Kwani kuna utaratibu wa kila mtu awe anatangaza kipato chake? Kila mtu akitangaza hapatatosha.
 
Scam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu hamstahili hata kuwepo Jf kwa kuamini upuuzi au inawezekana upo kwenye mission
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…