Maboso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 5,164
- 5,761
Yawezekana nisiwe chochote kwako lakini si vema ukapuuzia kila unachoshauriwa. Nimekuwa shabiki wako kwa muda mrefu, si shabiki tu bali mtu ninayesupport pia kazi zako. Mie si muhudhuriaji hata kidogo kwenye show zako bali ni mnunuzi mnzuri wa kazi zako kupitia wasafi.com . Pamoja na kuwa baadhi ya nyimbo zako nilishakuwa nazo lakini niliamua kuzinunua ili tu kuweza kusupport cha kwetu cha nyumbani.
Tuachane na hayo. Kuna jambo lilinisikitisha siku chache zilizopita, Video ya wimbo mnzuri wa African Beauty. Binafsi, na ninaamini kuna wengine pia watakubaliana na mimi kuwa ile video haikuwa na maadili hata kidogo. Mie niliamua kumezea mate tu nisiseme chochote hasa baada ya kuona umejaribu kutoa hiyo ulioiita clean version.
Kilichonisukuma kuandika huu uzi ni kuhusiana na post zako za jana katika Insta Story. Diamond mdogo wangu huwa hatupambani na wazazi wenzetu namna hiyo. Diamond post za jana siyo nzuri. Zinakupunguzia sana mashabiki. Sawa yawezekana upo kimataifa kwa sasa ila kumbuka fanya yote nyumbani ndio kila kitu. Zari si mwanamke wa kumfanyia hivyo. Sawa yawezekana usijali sana kuhusu Zari lakini una watoto wewe. Hivi umejaribu kufikiria maisha ya kina Tiffa pindi atakapovunja ungo atakuwaje? Umejaribu kufikiria maisha ya hao wanao wawili wa kiume watakuwaje? Mie mwanzo nilikusifu sana ulipoamua kutokusema chochote kuhusu kuachana kwako na Zari. Ila sasa kwa ulichokifanya jana umeonekana kabisa kwamba wewe ni mpuuzi na hujatulia. Unaharibu jina lako, unaharibu heshima yako, unajipunguzia endorsement ambazo ungeweza kupata kutoka kwa makampuni yanayojitambua. Unajipunguzia mashabiki. Kabla hujafanya kitu jaribu kwanza kufikiria. Yes it is your life but hii jamii ndio imekufikisha hapo. Bila support ya hii jamii hata ungefanya kitu gani usingeweza kufika hapo. Pesa zisikufanye uanze kupata kiburi na kufanya vitu vya aibu namna hiyo.
Ninapoaandika haya natambua wazi kwamba una haki ya kufanya ukitakacho ila angalia future ya wanao. Hebu jaribu kuconcetrate kwenye kazi.