tutaongea mengi,ukweli ni kwamba vita ya Congo,niyakufitinishwa na majirani,kibaya zaidi wanaofaulisha hizo fitina ni wacongo wenyewe,namaanisha ndani ya Congo kuna wa Congo wasaliti,wa Congo wanao wauza wa Congo wenzao kwa tamaa zao binafsi na maslahi yao binafsi,lakini swali lakujiuliza ni hili je kwa nn usaliti huu umekuwa sugu ndani ya ardhi ya Congo,jibu ni hili uzalendo wa wacongo ulishazikwa kitambo tangu enzi za mobutu seseseko,hivyo Congo ina generation ambayo neno uzalendo halimo ,yaani kisayansi ile Gene ya uzalendo haimo.ni kweli Congo ina viongozi lakini ni viongozi wa sio na uzalendo na ardhi yao,ni kweli Congo ina Wana nchi wazee kwa vijana lakini ni wananchi wasio na uzalendo na ardhi yao,ni kweli congo ina jeshi lakini ni jeshi lisilo na uzalendo na ardhi yao,ni kweli congo ina polisi lakini ni polisi wasio na uzalendo na nchi yao.hakuna nchi ambayo huwa haifitiniwi lakini tunaona linapokuja kwenye suala la nchi wananchi,viongozi na jeshi huweka tofauti zao pembeni na kuwa na sauti moja,kiongozi akisema adui na apigweee,wananchi na jeshi lote huitikia apigweee tena kwa kumaanisha kutoka moyoni wakiwa na Nia moja na ari moja ,na sio apigweeee ya mdomoni hapana.hata wapalestine tunawaona wanavyopambana kwa pamoja hata Kama bado hawaja fanikiwa lakini dunia nzima inaona wapalestine wanavyo waumiza vichwa waisrael,na hata Kama ukisimama useme wapalestine hawana uzalendo watu watakushangaa Sana,hii ni tofauti kwa ndg zangu wacongo.tatizo la congo limekuwa la muda mrefu Sana,lakini ni wao wacongo wenyewe wamekubali na kuridhika na yote. Ukweli ni kwamba wakongo kwa pamoja wakisema sasa basi inatosha,wanauwezo wa kumpiga adui yao nakumtoa nje ya mipaka,wanauwezo wa kumpiga hata wakaingia ndani ya mipaka ya adui na kumpiga,inawezekana kwa wacongo lakini ikiwa hawata geuka nyuma na kuviwazia vilivyo nyuma yao.kurudisha heshima ya kongo inahitaji sadaka ,sadaka ya kujitoa ,wacongo wa sasa wanahitaji kujitoa sadaka ili kutengeneza congo mpya yenye heshma kwa kizazi na kizazi kijacho.