Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,796
- 2,335
Rais Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo wa DRC amepata uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), wakati nchini kwake bado kunawaka moto na ebola imerudi. Je, atayamudu matatizo ya Afrika nzima ikiwa kwake bado kugumu? Wakongo msaidieni Rais Tshisekedi.
Kila siku Wakongo wanatumia midomo yao kuimba nyimbo za "nakupenda Cherie; na lingi mwasi kitoko na ngai." Huku wakikata mauno wakati nchi imegubikwa na migogoro isiyoisha tangu uhuru 1960!
Wakongo waache kabisa nyimbo hizo, badala yake waanze kutumia "midomo yao" kuimba nyimbo za mapinduzi ya kujenga nchi yao, kufanya maridhiano, kusameheana na kuaminiana kama walivyofanya Wazanzibari (serikali ya mseto) na Wakenya (handshake), japo wao walijadiliana - hawakuimba nyimbo.
Wao watumie "midomo yao" kuimba nyimbo za kumaliza tofauti zao na kuweka misingi ya umoja thabiti.
Wakongo ni ndugu zetu wa karibu, Waafrika wenzetu, majirani zetu na binadamu wenzetu; tuwasaidie kupatana na si kuchapana!